linguistics
JF-Expert Member
- Jun 22, 2014
- 4,713
- 4,369
Sio 90% ni 100% maana hata wewe yashakukuta. Manesi ndo wanafanya km utaratibu wao wa kazi kunyanyaza wagonjwa.Mimi hata sishangai ninauhakika Wa 90% aliyoyasema huyo mama yaweza kua kweli Mimi nilikutwa na hii kitu nimeenda kujifungua ktk hosptali ya wilaya moja nimeshaingia labour room kabisa nasikia kusukuma mtoto nesi ananiambia niinuke niende wodini imagine?
Namwambia nesi mbona nahisi kusukuma mtoto? Akanijia juu Mimi ndo nasema ndo nesi huyo!! Nilitoa chozi la uchungu bahati nzuri humo ndani alikuwemo nesi mwingine mwanafunzi ndie aliyenisogelea kunisaidia aisee sitaisahau siku hii maana nilimwita sana Yule nesi anisaidie humo humo labour lakini wapi!!
Namshukuru sana Yule mwanafunzi maana alinihudumia vizuri kuliko huyo mzoefu kazini haya mambo yapo jamani kuna manesi ni wakatili kuliko simba pia nilishuhudia Dada mmoja akijifungua na mtoto kudondokea chini kutoka kitandani kwani Yule Dada aliita manesi mpaka koo lilimkauka wapi hawatokei hadi nimehisi machozi nikikumbuka haya mambo.