Madaktari bingwa wafanikiwa kumpandikiza binadamu moyo wa nguruwe

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,053
164,360
Sijajua kama hapa Tanzania itakubalika labda Moshi.
--

Moyo wa nguruwe wapandikizwa kwa binadamu nchini Marekani​

A3BF3318-FEA3-4A3B-89F8-F0FCF8DA0CC3.jpeg


Katika picha hii iliyotolewa na Chuo cha kikuu cha Tiba cha Maryland, timu ya upasuaji inaonyesha moyo wa nguruwe tayari kupandikizwa kwenye mgonjwa

Kwa mara ya kwanza duniani, nchini Marekani, Madaktari wa upasuaji wamefanikiwa kupandikiza moyo kutoka kwa nguruwe aliyebadilishwa vinasaba hadi kwa binadamu mgonjwa, Chuo Kikuu cha tiba ya Maryland kimesema.

Operesheni hiyo ilitekelezwa siku ya Ijumaa. Ilionyesha, kwa mara ya kwanza, kwamba moyo wa mnyama unaweza kuendelea kufanya kazi kwa binadamu bila usumbufu wowote, Chuo Kikuu cha Maryland kimeongeza.

David Bennett, 57, ambaye alipokea moyo wa nguruwe, alitangazwa kuwa hastahili kupokea upandikizaji wa moyo wa binadamu. Sasa anafuatiliwa kwa karibu na madaktari ili kuhakikisha kiungo kipya kinafanya kazi vizuri.

"Yaani yalikuwa mambo mawili kwa binadamu huyo, ima kifo au upandikizaji wa moyo wa nguruwe. Nataka kuishi.

Ninajua ilinigusa sana, lakini ilikuwa chaguo langu la mwisho, "mkazi wa Maryland alisema siku moja kabla ya upasuaji wake, kulingana na chuo kikuu cha matibabu. "Siwezi kungoja niweze kuamka kitandani mara tu ninapokuwa mzima," David Bennett, ambaye amelala kitandani kwa miezi michache iliyopita na kutumia mashine inayomfanya aendelee kuishi.

Nguruwe aliyebadilishwa vinasaba
Mamlaka ya Madawa ya Marekani (FDA) iliidhinisha operesheni hiyo jioni ya siku ya kuamkia Mwaka Mpya. "Haya ni mafanikio makubwa ya upasuaji na ambayo yanatuwezesha kupata suluhisho dhidi ya uhaba wa viungo, " amebaini Bartley Griffith, aliyefanyiwa upandikizaji wa moyo wa nguruwe.

Nguruwe ambao moyo hutoka umebadilishwa vinasaba ili kutozalisha tena aina ya sukari ambayo kwa kawaida iko kwenye seli zote za nguruwe na ambayo husababisha kiungo kukataa kufanya kazi mara moja. Marekebisho haya ya jeni yalifanywa na kampuni ya Revivicor, ambayo pia ilitoa figo ya nguruwe ambalo madaktari wa upasuaji walifanikiwa kuunganisha kwa mishipa ya damu ya mgonjwa aliyekuwa mahututi huko New York mwezi Oktoba.

Takriban Wamarekani 110,000 kwa sasa wako kwenye orodha ya wanaosubiri kupandikizwa viungo na zaidi ya watu 6,000 wanaohitaji upandikizaji hufa kila mwaka nchini humo.
 
Hili limejadiliwa sana na Mashekh wakubwa duniani baada ya wataalamu kusema wanataka kufanya jaribio hili

Lakini pia 1969 kulikuwa na International Islamic Conference in Malaysia na walikuwa na mjadala kuhusu organs kuwekewa binadamu kutoka kwa mnyama awe domestic au wild na je ni Halal au non Halal

Haya mambo yamejadiliwa sana Mkuu ingawa najua wengine wanafanya kama kejeli lakini sisi tunajua kuwa kwa nguruwe hairuhusiwi kabisa hata kama ni desperate
 
Ni nchini Marekani

Source: BBC Dira ya Dunia

Sijajua kama hapa Tanzania itakubalika labda Moshi.
Hiyo ni kama medical trial na aliepandikizwa huyo moyo ni mgonjwa tayari wa moyo na anaweza kufa siku yoyote.

Pili, kabla hao madaktari hawajafanya huo upasuaji na kupandikiza huo moyo wa nguruwe waliomba kibali maalum kutoka serikalini na waliporuhusiwa ndo wamefanya hivyo.

Tatu, huyo nguruwe si nguruwe hawa tulozoea wa kuliwa kitimoto bali alipandikizwa maabara kwa ajili ya kujaribiwa katika upandikizaji yaani "genetically modified pig" hivyo si nguruwe wa kawaida.

Hivyo huyo mgonjwa baada ya kushindwa kumpata donor ambae yupo "healthy" ili kumsaidia kuendelea kuishi akaamua kukubali hiyo "experiment" ambayo ameambiwa haina uhakika wa kudumu yaani "guarantee".

Hitaji la viungo vya kupandikiza kama moyo ni kubwa sana nchini Marekani na mwaka jana pekee watu 3,800 walifanyiwa upasuaji wa moyo, na hiyo ni taarifa kutoka United network for Organ Sharing ambayo ni sehemu ya mfumo unosimamia upandikizaji wa viungo kwa mtu yoyote nchini Marekani.

Daktari bingwa wa upasuaji na mtaalam wa magonjwa ya moyo alofanya upasuaji kwa mgonjwa mzee David Bennett anaitwa Dr Muhammad Mohiuddin.

Dr Mohiuddin ndie alisimamia zoezi la kumtengeza nguruwe wa maabara na pia ni mtaalam wa upandikizaji wa viungo kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu yaani "animal-to-human transplant".
 
Hili limejadiliwa sana na Mashekh wakubwa duniani baada ya wataalamu kusema wanataka kufanya jaribio hili...
Mwaka jana watu 41,354 walipandikizwa viungo mbalimbali na khasa figo.

Lakini watu wengi walofanyiwa pandikizi ya animal- to - human transplant wengi viungo hivyo vimekuwa vikiwakataa.

Ndo Dr Mouhiddin na wenzake wakaamua kujaribu kuondoa cell yenye sukari ambayo waligundua ndo inokuwa ya kwanza kufanya "rejection" baada ya upandikizi.

Hivyo kwa kuwa huyu nguruwe tayari alikwishaandaliwa kwa ajili hiyo (moyo wake kutumika kupandikiza) ndio wakafanya marekebisho kwenye gene yake na wakaondoa hiyo kitu cell yenye sukari.

Jamaa wa "Food and Drug administration" ambao ndo husimamia upasuaji wowote nchini Marekani ndo wakaruhusu huu upandikizaji kwa huyu mzee ambae alipewa kibali cha huruma chaitwa "compassionate use emergence authorization" ambapo mgonjwa mwenye hali ya kuelekea kufa kwa kukosa kiungo mbadala huruhusiwa.
 
Madaktari wa Baltimore Marekani wamefanikiwa kupandikiza moyo wa Nguruwe kwa Binadamu ambaye amekua akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo ambao ulifikia kutishia uhai wake lakini sasa kapata tumaini jipya baada ya kuwekewa moyo wa Nguruwe aliyebadilishwa vinasaba.

Ni kupandikiza kwa kwanza kwa mafanikio ya moyo wa nguruwe ndani ya mwili wa Mwanadamu ambapo upasuaji huo uliochukua dakika 480 (saa nane) ulifanyika Baltimore siku ya Ijumaa na sasa Mgonjwa mwenyewe aitwae David Bennett Sr. wa Maryland anaendelea vizuri kiafya, wamesema Madaktari wa upasuaji katika Chuo Kikuu cha Maryland Medical Center.

"Moyo huo wa Nguruwe unafanya kazi kama kawaida, tumefurahi lakini hatujui kesho utatuletea nini kwani hili halijawahi kufanywa kwa Binadamu”

Habari hii imekuja ikiwa ni miezi miwili tu imepita toka Madaktari wa New York Marekani watangaze kufanikiwa kupandikiza figo ya Nguruwe kwa Binadamu.
Chanzo:milard Ayo
 
Hizi Ni Habari Njema Sana Kama Waliopandikizwa Viungo Hivyo Wakiishi Kwa Muda Mrefu,kwani Watatupa Imani Na Wengine Maana Wahitaji Wa Viungo Hivyo Ni Wengi Sana,so Far Nguruwe Ni Wengi Majumbani Mwetu ,kwaio Gharama Zitashuka Na Upatikanaji Utakuwa Rahisi Tofauti Na Human Hearts Na Tutaokoa Maisha Ya Wengi.
Jina La Bwana Lipewe Sifa.
 
Back
Top Bottom