Msishangae wakuu, ikiwa mtu akaanza mada bila hata kutoa salamu.
Habari zenu wakuu,
Unajua ugumu wa maisha umetufanya tubuni mbinu mpya ya kujipatia ridhiki. Jamani jamani naomba niweke wazi kitu hiki kinachonipa wasiwasi ndani ya Taifa letu.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la ndugu zetu omba omba wasiokuwa na vigezo vya kuomba omba barabarani. Hawa nao tuseme wamefoji taaluma hii? Au ndio ugumu wa maisha? Kuna jamaa mmoja mitaa ya Upanga pale yaani yeye ni mzima kabisa lakini maisha yake amewekeza katika kuombaomba pesa vitoto vidogo vya shule ya msingi Diamond.
Ukipita na mitaa ya mjini kati utakutana na ombaomba wanaotumia hadi smartphone, yaani leo nimechoka kabisa wengine wanawatumia watoto wadogo na kila mtoto jioni anatakiwa akabidhi hesabu yake ya mapato ya siku nzima.
Tulitazame tatizo hili kwa jicho pevu jamani, ikiwezekana wale wote wasio walemavu wala matatizo yoyote wakamatwe na kisha watafutiwe kazi za kufanya, maana hii ni aibu kwa Taifa na ni mfano halisi wa jamii yenye watu wavivu kabisa.
Ila kama wameachwa ili kuwa vivutio kwa watalii hapo sawa, maana kupitia wao watautangaza ujinga wetu, uvivu na upungufu wa maarifa na pia tutapata fedha nyingi za kigeni toka kwa watalii wanaokuja kushangaa omba omba wazima kabisa wasiokuwa hata ulemavu wowote.
Asanteni.