MAAZIMIO YA UVCCM KWENYE KONGAMANO LA MIAKA 60 YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
🗓️21Aprili, 2024
📍Zanzibar
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wameanzimia mambo yafuatayo katika Kongamano la UVCCM kuelekea Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1. Vijana wa Chama cha Mapinduzi kwa Umoja wetu na dhati ya Mioyo yetu tunampongeza sana Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kazi nzuri anayoifanya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 202-2025 na Uongozi wake umezidi Kuimatisha Muungano.
2. Vijana wa Chama cha Mapinduzi kwa Umoja wetu na dhati ya Mioyo wetu, tunampongeza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kazi kubwa anayoifanya ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025 na Uongozi wake umeendelea kuimarisha Muungano.
3. Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Vijana wenzetu wote walio Wazalendo tunaahidi kuendelea kuulinda Muungano wetu na kuzilinda serikali zake zote kwa gharama yoyote.
4. Sisi Vijana Wazalendo wa Taifa hili, tunaahidi kuwa, tutaendelea kuwa watiifu kqa Viongozi wetu na kuendelea kuwa nguvu kazi uhakika kwa nchi yetu, Tukiendelea kutoa elimu ya Muungano kwa Vijana wenzetu ili tuweze kurithisha kizazi hadi kizazi kwa maslahi ya Taifa letu, Afrika na Dunua kwa Ujumla.
Maadhimio haya yamesomwa kwa Niaba ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwegelo (MNEC)
Awali kabla ya kusoma maadhimio hayo Komredi Jokate alisema "Makongamano haya tunayoyaandaa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ni fursa ya kuendelea kujifunza na kuepuka kulishwa matango Pori kuhusu Muungano wetu na kutupa Fursa ya kutambua kuwa Muungano wetu ni tunu na lazima tuulinde kwa wivu Mkubwa"
Imetolewa na;
Idara ya Uhamasiahaji na Chipukiz UVCCM Taifa.

- KulindaNaKujengaUjamaa
- MuunganoWetu
- Miaka60YaMuungano.