Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
519
1,246
Maandamano ya CHADEMA yanaendelea Mbeya sasa hivi


Tundu Lissu:

- Tutaandamana mpaka tutakapopata Katiba mpya, mfumo mpya wa uchaguzi, mpaka tutakapowaondoa madarakani hawa wanaotunyonya.

- Hatuandamani kwa sababu tunataka kujifurahisha, au kufanya mazoezi, tunaandamana sababu tuna hasira na hiyo hasira ndiyo itakayoleta mabadiliko. Tunaandamana kwasababu njia za mazungumzo zimekataliwa, mlango mmoja ukifungwa mingine lazima ifunguliwe kwahiyo njia ya maandamano ni njia ya shinikizo kwa wale waliokataa meza ya mazungumzo.

Akijibu kuhusu madai ya Makonda kuwa CHADEMA ndio waliokataa maridhiano Lissu amesema, Mimi kwenye maridhiano sijauona Makonda nimemuona kinana, Mzanzibari Spika na wengine kwenye maradhiano. Hawa ndio wanaweza kuzungumza kimejadiliwa kitu gani na tumeshindwana kwenye kitu gani, sio Paul Makonda.

Akijibu kuhusu Makonda kusema amewakimbia kwenye Mdahalo Lissu amesema, "Sisi tutakaaje na mhalifu yule, sisi tutakaaje na muuaji yule, kuteka watu nyara, kuvamia vituo vya televisheni kama clouds tutakaaje na mtu anayepaswa kuwekwa gerezani? Na haya ni kwa uthibitisho wa mambo aliyofanya na anayotuhumiwa kuyafanya, ndio maana Wamarekani wamempiga marufuku kwenda Marekani, ni mhalifu, hatuwezi kukaa na jambazi. Watanzania wajue kwamba hatuwezi kukaa na jambazi.

Mwabukusi

Wanatuambia wamebinafsisha bandari lakini ukweli ni kwamba wameziuza. Tutaendelea kupiga kelele na kukataa mikataba hii sababu mikata hii taitendei haki kama Watanganyika.

Swala la bandari halijaisha mahakamani, mahakama ilisema imefungwa mikono, mahakama ilisema sheria imekiukwa, sisi tunataka mikono ifunguliwe na bandari isrudishwe kwa watanganyika. Suala hili halijatulia bado bado kwani tumekata rufaa, hata wao hawajatulia ndio maana wamewadanganya watanzania kuwa wamefanya maerekbisho. Mimi nawauliza kama wamefanya marekebisho watuambie lini IGA ilienda bungeni ambao bunge, ikatambua unquestionable terms zote katika wizara husika, lini zilifika mbele ya baraza la mawaziri na kufanyiwa kazi, lini zilikwenda bungeni na kufanyiwa kazi, na lini zilikwenda Dubai kujadiliwa na kusaniwa? Hawasemi ukweli, jambo la bandari bado sana kuisha.
 
Asante sana

Screenshot_2024-02-20-10-53-52-1.png
 
Jana RC wa mbeya Juma Omera ameyaita maandamano ya CDM kuwa ni ya kutafutia Kiki.

Akashauri kuwa wananchi mkoani humo kujifanyia shughuli zao badala ya kwenda kwenye maandamano hayo.

Nafikiri alikuwa anajidanganya sana maana yeye pia ni binadamu kama wengine tu.

Tupo hapa Mbalizi tunamsubiria mwenyekiti wetu taifa ili tuanze kupandiaha kilima na kuingia jijini.
 
Jana RC wa mbeya Juma Omera ameyaita maandamano ya CDM kuwa ni ya kutafutia Kiki.

Akashauri kuwa wananchi mkoani humo kujifanyia shughuli zao badala ya kwenda kwenye maandamano hayo.

Nafikiri alikuwa anajidanganya sana maana yeye pia ni binadamu kama wengine tu.

Tupo hapa Mbalizi tunamsubiria mwenyekiti wetu taifa ili tuanze kupandiaha kilima na kuingia jijini.View attachment 2909824
Ebanaeeeeeee......

Mutu ananuna anakuwa piritoni anapasuka.....

Mbeya Shikamoo ni MTITI

Ndagafijooooo...
 
Hayo ni matembezi kama ya meimosi tusitarajie chochote
Maandamano gani mnaandamana na polisi
 
Back
Top Bottom