Maalim Seif Shariff Hamad Rais Zanzibar, maandalizi ya kutangazwa yaiva

Umoja wa mataifa ukimuuliza shein unakatalia ikulu kuna biashara gani unafanya atajibu nn wakati anajua alishindwa?
 
Mbona CUF wamesusia shughuli za sherehe za mapinduzi?
Wanajisusia wenyewe kama Seif atatangazwa kabla ya siku hiyo
 
Sasa hili gazeti la mawio huu waliotuandikia hapa ni uongo wa wazi wazi
 
KAMA
Maalim seif Jabali la siasa za upinzani Zanzibar
Mungu ampe haki yake tu kwakweli he deserve it
NAONA KAMA NIKO HURU AU HARUFU TU. Hili ni gazeti la udaku, tuayapokee kwa tahadhari hasa vile kuna vibwagizo ndani ya makala vinavyopingana. ISIJE KUWA KAMA MATANGAZO YA DTV MIAKA ILE!
 
Hivi hawa ccm wanaong'ang'ania hata umeya tu wa ilala na kinondonwakati wamezidiwa madiwani na UKAWA ndio watakubali kuiachia nchi ya Zanzibar? Nitakuwa wa mwisho kuamini hili.
Nimeipenda, ni ukweli uaouma!
 
Labda ngamia apenye katika tundu ya sindano
atakuaje rais huku uchaguzi ulivurugwa? nani amtangaze wakati zec haikumaliza kuhesabu kura ikafuta uchaguzi!!. hapa suluhisho ni kurudia uchaguzi hatangaziwi seif wala baba yake seif ushindi. ccm hawatakubali uhuni.
 
THANKS THE INTELLIGENT HON.DR.MAGUFURI,SALUTE!!!
..""utajijengea heshima kubwa isiyo na mfano DUNIA NZIMA""
IBRAHIM MO AWARDS WAITING.

Hivi mtaendelea kufikiri kwa kutumia mgongo hadi lini? Magufuli ana lipi alilofanya katika mgomgoro huu hadi atunukiwe hiyo tuzo?Nafikiri anayepaswa kushukuliwa ni Mh.Maalim Seif Sharif Hamad,pamoja na kucheleweshwa ushindi wake,bado amekuwa mvumilivu na kuendelea kushiriki kwenye mazungumzo na wale waliopora ushindi wake.Ni busara zake tu zilizotufikisha hapa,vinginevyo hii nchi ingekuwa imezalisha wakimbizi na maelfu kupoteza maisha.Mungu ampe maisha malefu Mh. Seif.
 
Ila yule dokta naye jamani aone aibu kukalia nafasi isiyo yake vinginevyo anaudhalilisha udokta wake. Kwani nani alimwambia kushindwa ni kufa?
ukiangalia kwa harakaharaka utaona kikwazo ni Dr. Shein. lakini kwa taarifa yako shein yupo tayari hata leo kumuachia madaraka Seif. Tatizo ni mfumo wa CCM na yeye kawekwa pale na mfumo. mfumo ni nouma japo wanatakiwa waone hata aibu na waheshimu maamuzi wa wazanzibar
 
Kwa ccm kuachia Zanzibar itakuwa tukio la kufungua Mwaka kama walivyomshinikiza Jecha afanye yake imekuwa tukio la kufunga mwaka
 
Mhhh hiyo avatar yako ni jipu. Pia nakuunga mkono sio zamani ni wakati wa kampeni
Haina tatizo hiyo mkuu. Ina maana yake nzuri tu, tatizo wewe umeifikiria kwa maana ya tunda la mti wa katikati. Kwa hiyo unataka kusema hata Matombo nayo ni jipu?
 
Dr. hana tatizo yeye yuko tayari kwa lolote na anawaunga mkono wapemba wenzake shida iko kwenye chama chake.
Ila mimi namuona hana tofauti na Lolaa Bagbo wa Ivory coast ambaye naye baada ya kushindwa akagoma kutoka mpaka jumuiya ya kimataifa ilipoingilia kati. Tatizo la Zanzibar ni kuwa ile ni sehemu ya Tanzania hivyo jumuiya ya kimataifa haiwezi kuingia moja kwa moja. Huo ndio ujanja Tanganyika ilioutumia kuimeza Zanzibar kwa kuiondolea utambulisho wake kimataifa hivyo kubaki koloni lake na kutokuwa na maamuzi yake ya nje. Imebaki nchi kwa jina lakini haina soverenite.
 
Hizo ni propaganda tu au drip hakuna lolote mbona munatubabaisha mazungumzo ya ikulu hakuna anayoyajua aulizwa maalim SEIF mwenyewe sio hao wasio waaminifu
 
Maalimu-Seif-Hamad-620x308.jpg

  • USHINDI wa Maalim Seif Shariff Hamad katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, ungali salama.
  • Ushindi huo kutangazwa kabla ya Zanzibar kufikia kilele cha maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi.

Taarifa zinasema viongozi wa kitaifa, wakiwemo marais wastaafu Zanzibar, ambao wamekuwa wakikutana na Maalim Seif, Ikulu ya Zanzibar, wanakaribia kukamilisha utaratibu wa kuwezesha kiongozi huyo kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo.

“Hili halina utata wowote. Nakuhakikishia wanakaribia kuona mantiki na kuelewana; utaratibu wa kumtangaza Maalim Seif utatolewa wakati muafaka,” amesema mwanadiplomasia kutoka moja ya mataifa ya Ulaya.

Amesema kwa kadri anavyofahamu, maendeleo ya mazungumzo hayo yanayomhusisha pia Rais Dk. Ali Mohamed Shein, katika siku za karibuni, yamejikita katika kupata uhakika kuwa serikali mpya itaundwa kwa kuzingatia matakwa ya sheria na katiba.

Lakini amesema, hata suala hilo halijawa tatizo kwa kuwa mfumo wa kuunda serikali umesukwa vema katika Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

“Kama unavyojua mfumo wa serikali utakuwa uleule wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kwa matokeo ya uchaguzi vyama vya CCM na CUF ndivyo vitaunda serikali mpya,” alisema.

Mwanabalozi huyo aliulizwa na mwandishi jinsi anavyoona hali ya kisiasa kwa sasa na hasa kuhusu mgogoro uliotokana na uchaguzi.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari ndani ya CCM, Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano, hakutakuwa na uchaguzi wowote bali utakuwepo utaratibu wa kumtangaza mshindi.

Chanzo katika CCM kimesema, “Hili liko wazi, mshindi wa uchaguzi ule ni Maalim Seif wa CUF ambaye naweza kusema amefanikiwa kusimamia ushindi wake huo na hoja zake hazishindiki. Nakwambia atatangazwa siku chache zijazo.”

Kiongozi huyo ambaye aliomba asitajwe jina gazetini, amemsifia Maalim Seif kwa kubaki mtulivu wakati wote akijadiliana na viongozi wenzake ambao wote ni kutoka CCM.

Katibu Mkuu huyo wa CUF na mwanasiasa ambaye amekuwa akilalamika kuhujumiwa mara zote akigombea urais, amekuwa akishiriki mazungumzo na marais wastaafu.

Marais hao ni Ali Hassan Mwinyi, Dk. Salmin Amour Juma, Amani Abeid Karume na Dk. Shein. Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi naye amehudhuria mazungumzo hayo.

Dalili za kuwepo muafaka katika majadiliano zimeonekana hivi karibuni pale Dk. Shein, aliyekuwa akigombea urais kwa mara ya pili, na Maalim Seif walipokutana na Rais mpya wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika nyakati tofauti.

Wote walisikika wakisema majadiliano yao yanaendelea vizuri, lakini Dk. Magufuli akieleza waandishi wa habari nje ya ofisi yake Ikulu baada ya kukutana na Maalim Seif kuwa, “amenihakikishia wanaendelea vizuri na nimemtaka wakamalize majadiliano yao na apige kazi.”

Dk. Shein alipotoka nje ya maongezi na Dk. Magufuli aliwaambia waandishi wa habari kuwa mazungumzo yanaendelea vizuri na yatakapomalizika, watatoa taarifa kwa umma kuwaeleza maafikiano yaliyofikiwa.

Taarifa zilizopatikana baadaye zinasema moja ya mambo ambayo Dk. Shein alitakiwa kuyafanya baada ya hapo, ni kukutana na Kamati Maalum ya NEC-CCM, kuwaeleza maendeleo ya vikao na viongozi wenzake vinavyofanyika Ikulu.

Jumapili iliyopita, MAWIO lilielezwa kile kilichotokea katika kikao kilichofanyika Ofisi Kuu za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar kilichoandaliwa kwa ajili ya Dk. Shein kutoa taarifa yake.

Katika kikao, Dk. Shein “alitoa taarifa yake na taarifa yenyewe kujadiliwa vizuri” mpaka kikao kilipomalizika yapata saa 9.30 alasiri.

Dk. Shein aliondoka na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kumaliza kikao.

Lakini baada ya viongozi hao wakuu kuondoka ukumbini, baadhi ya wajumbe waliobaki walianza kudai kuwa hawakubaliani na mapatano na kwamba wanataka uchaguzi urudiwe.

Gazeti hili limeambiwa baada ya Dk. Shein kuondoka Kisiwandui, Balozi Seif alifuatana na baadhi ya viongozi kwenda Ofisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi, iliyoko Amani, ambako walifanya mjadala ulioibua kilichoitwa “kauli za chuki” zikimlenga Maalim Seif.

Kwa kuzingatia aliyoyasema Dk. Shein, baadhi ya viongozi walionekana wakifuta machozi kwa kilichoelezwa ni “kutoamini kwao kuwa CUF itapishwa kuongoza serikali mpya.”

Akijibu hoja ya kurudia uchaguzi ambayo wananchi wengi wameonesha kuipinga, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Umma wa CUF, Ismail Jussa Ladhu amesema kurudia uchaguzi siyo chaguo la wananchi.

Aliwaambia waandishi wa habari mgogoro wa Zanzibar ni wa kutengeneza, uliolenga kuchanganya wananchi na kuwapora ushindi wao. Ametaka wananchi wapuuze kauli za kurudia uchaguzi.

“CUF inawahakikishia Wazanzibari kwamba haitotetereka; itasimamia kwa dhati maamuzi waliyoyafanya kwa njia za kidemokrasia kupitia uchaguzi mkuu na italinda chaguo lao la Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani wao,” alisema Jussa.

Amepongeza wananchi kwa kuonesha “ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa na kuendelea kutunza amani na utulivu wakati wakisubiri matokeo ya kazi kubwa waliyoifanya tarehe 25 Oktoba ambayo inaashiria ujenzi wa Zanzibar Mpya.”

Source: MAWIO
 
Last edited by a moderator:
Mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim SEif Shariff Hamad Seif rais Zanzibar, maandalizi ya kutangazwa yaiva.

USHINDI wa Maalim Seif Shariff Hamad katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, ungali salama.

MAWIO limeelezwa kuwa ushindi huo utadhihirishwa kabla ya Zanzibar kufikia kilele cha maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi.

Taarifa zinasema viongozi wa kitaifa, wakiwemo marais wastaafu Zanzibar, ambao wamekuwa wakikutana na Maalim Seif, Ikulu ya Zanzibar, wanakaribia kukamilisha utaratibu wa kuwezesha kiongozi huyo kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo.“Hili halina utata wowote.

Nakuhakikishia wanakaribia kuona mantiki na kuelewana; utaratibu wa kumtangaza Maalim Seif utatolewa wakati muafaka,” amesema mwanadiplomasia kutoka moja ya mataifa ya Ulaya.

Amesema kwa kadri anavyofahamu, maendeleo ya mazungumzo hayo yanayomhusisha pia Rais Dk. Ali Mohamed Shein, katika siku za karibuni, yamejikita katika kupata uhakika kuwa serikali mpya itaundwa kwa kuzingatia matakwa ya sheria na katiba.

Lakini amesema, hata suala hilo halijawa tatizo kwa kuwa mfumo wa kuunda serikali umesukwa vema katika Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

“Kama unavyojua mfumo wa serikali utakuwa uleule wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kwa matokeo ya uchaguzi vyama vya CCM na CUF ndivyo vitaunda serikali mpya,” alisema.

Mwanabalozi huyo aliulizwa na mwandishi jinsi anavyoona hali ya kisiasa kwa sasa na hasa kuhusu mgogoro uliotokana na uchaguzi.

Mgogoro wa sasa Zanzibar ulitokana na uchaguzi mkuu kufutwa kiubabe na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.
Jecha alifuta uchaguzi kwa tangazo lililorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) mchana wa Oktoba 28.

Wakati huo tayari Jecha alikuwa ameshatangaza kura za majimbo 33, akibakiza majimbo 21 tu.

Mwandishi alilenga kupata msimamo wa Jumuiya ya Kimataifa kuhusu kauli tata za viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, Waride Bakari Jabu aliwataka wana-CCM kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio aliosema utafanyika “wakati utakapowadia.”

Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari ndani ya CCM, Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano, hakutakuwa na uchaguzi wowote bali utakuwepo utaratibu wa kumtangaza mshindi.

Chanzo katika CCM kimesema, “Hili liko wazi, mshindi wa uchaguzi ule ni Maalim Seif wa CUF ambaye naweza kusema amefanikiwa kusimamia ushindi wake huo na hoja zake hazishindiki. Nakwambia atatangazwa siku chache zijazo.”

Kiongozi huyo ambaye aliomba asitajwe jina gazetini, amemsifia Maalim Seif kwa kubaki mtulivu wakati wote akijadiliana na viongozi wenzake ambao wote ni kutoka CCM.

Katibu Mkuu huyo wa CUF na mwanasiasa ambaye amekuwa akilalamika kuhujumiwa mara zote akigombea urais, amekuwa akishiriki mazungumzo na marais wastaafu.

Marais hao ni Ali Hassan Mwinyi, Dk. Salmin Amour Juma, Amani Abeid Karume na Dk. Shein. Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi naye amehudhuria mazungumzo hayo.

Dalili za kuwepo muafaka katika majadiliano zimeonekana hivi karibuni pale Dk. Shein, aliyekuwa akigombea urais kwa mara ya pili, na Maalim Seif walipokutana na Rais mpya wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika nyakati tofauti.

Wote walisikika wakisema majadiliano yao yanaendelea vizuri, lakini Dk. Magufuli akieleza waandishi wa habari nje ya ofisi yake Ikulu baada ya kukutana na Maalim Seif kuwa, “amenihakikishia wanaendelea vizuri na nimemtaka wakamalize majadiliano yao na apige kazi.”

Dk. Shein alipotoka nje ya maongezi na Dk. Magufuli aliwaambia waandishi wa habari kuwa mazungumzo yanaendelea vizuri na yatakapomalizika, watatoa taarifa kwa umma kuwaeleza maafikiano yaliyofikiwa.

Taarifa zilizopatikana baadaye zinasema moja ya mambo ambayo Dk. Shein alitakiwa kuyafanya baada ya hapo, ni kukutana na Kamati Maalum ya NEC-CCM, kuwaeleza maendeleo ya vikao na viongozi wenzake vinavyofanyika Ikulu.

Jumapili iliyopita, MAWIO lilielezwa kile kilichotokea katika kikao kilichofanyika Ofisi Kuu za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar kilichoandaliwa kwa ajili ya Dk. Shein kutoa taarifa yake.

Katika kikao, Dk. Shein “alitoa taarifa yake na taarifa yenyewe kujadiliwa vizuri” mpaka kikao kilipomalizika yapata saa 9.30 alasiri.

Dk. Shein aliondoka na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kumaliza kikao.

Lakini baada ya viongozi hao wakuu kuondoka ukumbini, baadhi ya wajumbe waliobaki walianza kudai kuwa hawakubaliani na mapatano na kwamba wanataka uchaguzi urudiwe.

Gazeti hili limeambiwa baada ya Dk. Shein kuondoka Kisiwandui, Balozi Seif alifuatana na baadhi ya viongozi kwenda Ofisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi, iliyoko Amani, ambako walifanya mjadala ulioibua kilichoitwa “kauli za chuki” zikimlenga Maalim Seif.

Kwa kuzingatia aliyoyasema Dk. Shein, baadhi ya viongozi walionekana wakifuta machozi kwa kilichoelezwa ni “kutoamini kwao kuwa CUF itapishwa kuongoza serikali mpya.”

Akijibu hoja ya kurudia uchaguzi ambayo wananchi wengi wameonesha kuipinga, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Umma wa CUF, Ismail Jussa Ladhu amesema kurudia uchaguzi siyo chaguo la wananchi.

Aliwaambia waandishi wa habari mgogoro wa Zanzibar ni wa kutengeneza, uliolenga kuchanganya wananchi na kuwapora ushindi wao. Ametaka wananchi wapuuze kauli za kurudia uchaguzi.

“CUF inawahakikishia Wazanzibari kwamba haitotetereka; itasimamia kwa dhati maamuzi waliyoyafanya kwa njia za kidemokrasia kupitia uchaguzi mkuu na italinda chaguo lao la Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani wao,” alisema Jussa.

Amepongeza wananchi kwa kuonesha “ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa na kuendelea kutunza amani na utulivu wakati wakisubiri matokeo ya kazi kubwa waliyoifanya tarehe 25 Oktoba ambayo inaashiria ujenzi wa Zanzibar Mpya.”

Ni msimamo wa CUF kuwa Maalim Seif alishinda uchaguzi kwa zaidi ya kura 25,000.

Kwamba CUF ilipata viti 27 vya uwakilishi. Kwamba CCM ilishindwa kupata kiti kisiwani Pemba. Kwamba CUF ilitwaa viti tisa Unguja.

Chanzo: Mawio
Sisi akina Tomaso tupo, huwa hatuamini mpaka hili litokee!, yaani inchi iliyopatikana kwa njia ya mapinduzi, kukabidhiwa kwa makaratasi!, yaani kwa mara ya kwanza, sehemu ya JMT inayoitwa Zanzibar, ambayo siku zote imekuwa ikitawaliwa kwa mabuvu, leo watatumia voting kukabidhi madaraka, badala ya vetting?!, bado siamini!. Yaani yule Sultani aliyefurushwa na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, leo anarejeshwa kwa jina jipya la demokrasia!, mimi bado siamini hadi hili litokee!, Wazanzibar sio watu wa kuwaaminia sana kivile!, mimi ni type ya wale watu ambao hata akiambiwa it is over, kwetu it is not over until it is over!, tunasubiri!

Heri ya Mwaka Mpya
Pasco
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom