Lowasa na Sumaye: wako Upinzani wenye mamlaka wanawatuhumu badala ya kuwachukulia hatua? Wanawaogopa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,884
Najiuliza sipati jibu ili kuhitimisha jambo moja kuliko kurudiwa kila siku.

Sasa Lowasa na Sumaye wako upinzani ambako rais anasema ananguvu za kuwashughurikia na katoa mamlaka zote ziwashughurikie vilivyo.

Tena wakati wa kampeni alisema anafungua mahakama ya mafisadi awafunge watu kama kina Lowasa.

Nashindwa kuelewa serikali na vyombo vyake kwanini hawakamati hawa mawaziri wakuu ili wajibu tuhima za ufisadi? Na hawa mawaziri wakuu hawana kinga yoyote kama za marais.

Naomba wale wote tunaosema hawa ni mafisadi tukafungue kesi mapema ili wafilisiwe kabisa
 
kwa jinsi tunataka tuone watu wakiwajibishwa kwa huu ujambazi, tunataka katiba mpya itakayowafungwa mawaziri wakuu na marais wastaafu kwa ujambazi waliofanya wakiwa madarakani.
 
Ccm hawajawahi kuwa serious na hili jambo ni sanaa na siasa za kujitafutia umaarufu wa kisiasa bila kugusa hiki kiini hatuwezi kutatua.
 
Wezi ni ccm wenyewe ..!! Si umeona hata rais amewaita wezi wajadiliane... ? Teh teh teh teh... Eti wajadiliane na wezi ambao hawana lessen teh teh teh
 
Mi naomba washitakiwe hawa watu
Ila wasiposhitakiwa ktk utawala huu ambao unajipambanua kuwa unachukia ufisadi nitaamini kuwa hawa watu ni wasafi ila tatizo ni chama walichokuwa
 
Lowassa na Sumaye wamefanya dealsna Mkapa na Kikwete. Magufuli kashasema marais wastaafu hawagusi.

Kwa hiyo zaidi ya maigizo huwezi kuona wanaguswa.
 
Lowassa na Sumaye wamefanya dealsna Mkapa na Kikwete. Magufuli kashasema marais wastaafu hawagusi.

Kwa hiyo zaidi ya maigizo huwezi kuona wanaguswa.

Hahahaaaa.

Sasa kama Lowassa na Sumaye wamepiga sana dili na Mkapa, unaliongeleaje suala la wao kuhamia CHADEMA na mmoja wao kupewa fursa ya kuipeperusha bendera yao kwenye uchaguzi mkuu ilhali ni wao wenyewe ndo waliosema kuwa yeye [Lowassa] ni fisadi?
 
sasa unataka na wao watoboe siri za mabalaza ya mawaziri kipindi wao wakiwa madarakani eeehe?
 
Hata shetani yuko duniani anafanya maovu lakini Mungu hamchukulii hatua kali. Hii haina maana kwamba Mungu hana uwezo wa kumchukulia hatua.

Lowassa na Sumaye kuendelea kuwa upinzani bila kuchukuliwa hatua na serikali ni mtaji mkubwa sana wa kisiasa kwa CCM.
 
Hakuna sehemu ambapo CHADEMA walipoteza muelekeo kama si tu walipomkubali Lowassa, bali na kumpa kugombea urais hapo hapo.

Hata kanisani huwezi kuingia leo hata mafunzo ya katekisimu hujapitia, kesho unakuwa Papa.

Hususan kama una mawaa kamaya hawa mabwana.

Mara miahata wangemfanya Lowassa kama walivyomfanya Sumaye tungesema wanawabadilisha mafisadi watubu dhambi zao na kujenga upinzani, pengine hata kuchukua siri za ufisadi walioufanya.

Ile kumpa Lowassa nafasi ya kugombea urais ilikuwa kama kusema CHADEMA haina uwezowakutoa viongozi ni kama fisi wanaongojea mkono wa CCM uanguke ili wao wapate nyama.

Mimi sikushangaa sana lakini,kwa sababu ingawa sina imani na CCM, nilishasemakwamba upinzani nao unaenda arijojo.
 
Wezi ni ccm wenyewe ..!! Si umeona hata rais amewaita wezi wajadiliane... ? Teh teh teh teh... Eti wajadiliane na wezi ambao hawana lessen teh teh teh
Yaan wanatia aibu...mwizi amekuibia miaka yote hiyo na bado wanaoperate bila leseni bado unambembeleza mkae mezani.CCM wanafanya maigizo tu kama kawaida yao.
 
Hakuna Mungu wala Shetani.

Matatizo yetumengi sana yanaanzia na imani za kuwapo Mungu na Shetani.

Bila kuondokana na imani hizi matatizo yetu mengi sana hayataisha.
 
Waswahili wana msemo wao"UKIJUA HILI NASI TUNAJUA LILE",ndo kiburi cha Lowassa na Sumaye.
 
Reactions: bht
Kwa hili napingana na wewe.

Mungu angekua na uwezo wa kumchukulia hatua shetani angekua amechukua vinginevyo na yeye anafurahia anayoyafanya shetani kwa maana hiyo mungu amebariki matendo ya shetani.

Haiwezekani mtu afanye mambo ambayo unajitanabaisha wazi kua huyapendi na unayachukia sana kisha umuache tu ayafanye wakati unadai una uwezo wa kumzuia asifanye, basi unafurahia anayoyafanya au huna uwezo wa kumzuia asifanye.
 
Chadema haina tofauti na ccm!

Fukuza Sumaye na Lowasa ili tujue kweli hiki chama cha Chadema ni brand new!
 
Hakuna Mungu wala Shetani.

Matatizo yetumengi sana yanaanzia na imani za kuwapo Mungu na Shetani.

Bila kuondokana na imani hizi matatizo yetu mengi sana hayataisha.

Ukiona mtu yoyote anakimbilia mambo ya mungu na shetani ujue uwezo wake wa kufikiri umefika kikomo na hana namna hivyo anaamua kuhamisha matatizo yake kwa kitu kisichokuwepo au kisichoonekana ili akwepe lawama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…