Lissu: Tutaandamana kwa sababu ni halali, Polisi wawachukulie hatua hao wanaosema watavunja amani

Nyakijooga

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
256
458


Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, Tundu Lissu amesema maandamano yaliyotangaza na Chama hicho kupinga vitendo vya utekaji Nchini yako palepale Septemba 23 2024.

"Hii habari ya kuingia barabarani Watu wanaizungumza visivyo kabisa, kwani tangu lini kuingia barabarani ni haramu Nchi hii?, sheria ya Nchi hii inasema ni haki kuandamana na ukiandamana ni haki kupewa ulinzi na Polisi na ukihitaji msaada sheria inasema unapatia msaada na Polisi, kwani Watu wanafikiria kuandamana ni haramu? nani aliyesema ni haramu?" amesema Lissu.

"Kwahiyo habari ya kwamba mtaandamana au laah!, tutaandamana kwasababu ni halali, tunataka matendo, Wahalifu wakamatwe, Watu wameua, wanachukua Mtu kwenye basi wanaenda kumuua na imeshatokea mara nyingi, mnataka wafe wangapi ndio tuseme sasa inatosha?, kwahiyo maneno
matupu hayatoshi"amesema Lissu

"Tunataka uwajibikaji, na Maaskofu wetu wamesema wanataka uwajibikaji, sheria haisemi mambo ya kuomba kibali, Polisi wakawashike na kuwachukulia hatua hao wanaosema watavunja amani lakini hawawezi kusema sisi tusitumie haki yetu ya kuandamana kwasababu Wahalifu watakuja kuharibu wawakamate Wahalifu" amesema Lissu.

"Kuhusu hofu ya kutopewa kibali, sheria ya Nchi hii inasema tunatoa taarifa tu haisemi tuombe kibali, taarifa tutatoa lakini kusema kwasababu Nchimbi amesema tu aah nilipopigwa risasi mie Magufuli alilaani, alisema watafutwe, wametafutwa?, mnataka wauawe wangapi?, watekwe nyara wangapi ndio tuseme hapana tena?" amesema Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akiongea baada ya Kongamano la tano la Ekaristi Takatifu Kitaifa lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaaam leo September 15,2024.

Pia Soma ~ Kauli ya Albert Chalamila akigusia Maandamano ya CHADEMA kwa mafumbo, adai yanaweza kuahirishwa
 
Walio ihalibu hii,nchi ni, ccm na,ni,waoga sana ila,siku yaja watatafuta mashimo kama paka shume
 
Back
Top Bottom