Lissu awe Mwenyekiti CHADEMA na Lema awe Katibu

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,168
10,793
Sijaandika kama naota au nimekurupuka,

Japo CHADEMA chini ya Mbowe huwa hawapokei kabisa ushauri wowote ule, mwisho wa siku hawaendi mbali, na hawarudi nyuma kuangalia walipodondokea.

Mbowe ni fisadi anayetumia mwanya wa CCM kuwa hivi tunavyowaona, Mbowe hana tofauti na mchungaji Lusekelo, au Mnganga wa kienyeji ambao unapokuwa na shida una watumaini wataleta msaada fulani kumbe ndio wanakupiga hapo hapo.

Tumesema sana na sijawahi kukata tamaa kuona chama kinageuka, huyo Lowassa hana chochote kipya

Mbowe..well japo idea zake za kibiashara zimeifikisha chadema ilipo, abadilike sasa na awaze kuwakomboa watanzania. Ukiwa mpinzani nchi hii hautakiwi kulala kwa amani wakati tunaona nchi inakoenda.

Mabifu na magomvi ya ndani ya vyama mmeishaona hayana tija, wako mnaaosema tulipata kura nyingi, lengo halikuwa hilo..ilikuwa kuingia Ikulu. kama kura nyingi tunaweza kuwapigia hata leo kwa tukio lingine lolote lile, mnadhani na kushangilia ruzuku imeongezeka wala haiwasaidiaa nyie ni Mbowe na familia yake na watu wake.

Basi imefika muda wa kupiga UTURN, kuacha siasa za matumaini na kujipa moyo. CHADEMA ili ifike mbali na ishike dolla, Mwenyekiti awe Tundu Lissu na Katibu awe Lema.

Tutaona siasa tamu za kusisimua na so hizi za kumchekea huyu jamaa
kama kawaida mtatukana, mtabisha maana wengine kwenu Mbowe ni mtume!

Lissu is a perfect match ya kupambana na huyu wa sasa sio kuwa hana kasoro hapana, anaweza kwa wakati huu na nyakati hizi wakati CHADEMA inasikika sehemu chache tu.

Katibu wenu sijui anaitwa nani vile? Ebu mpeni Lema

Mkimaliza hayo shikamaneni na wapinzani wengine, mmemaliza nguvu zenu nyingi sana miaka mitatu kupambana na wasiotakiwa kupambana nao

Lazima gharama ya aibu ambayo CHADEMA imeingia na ku experince kwa maamuzi 'yale' lazima yalipwe na maamuzi THABITI ya kukiokoa

CCM ni janga jamani hivi janga hili kwanini linachekewa?

wabe
 
Pamoja na kujaribu kuimarisha upinzani, elimu ya uraia pia inahitajika ili wananchi wafahamu wajibu wao kama Raia kwamba wanalo jukumu la kwanza kabisa la kutafuta maendeleo yao na serikali ni mdau muhimu and not otherwise!

Siasa za kutoa mategemeo mfu kwamba wapinzani wakiingia mambo yatabadilika na kwamba chama kilichopo madarakani ndio kiini cha matatizo ni siasa za kilaghai!

Hii mind set ya kutegemea serikali kwa kila kitu ndio adui yetu mkubwa ambaye hata tukibadili serikali ngapi, mambo yatakua Yale Yale kwakua serikali haiwezi kufanya kila kitu, nakumridhisha kila MTU!
 
Hii nakubaliana nayo! Japo ukitaka kutoa ushauri usimtusi unayemshauri kama kina mbowe!! Ukweli pamoja na shida zote za mbowe lakini amemwaga jasho jingi kukijenga chama hiki. Hakuwahi kununulika, ni mstaarabu kupita kiasi!!na hii haifai kwa utawala usio wa kistaarabu kama huu. Alifaa kwa kipindi cha mstaarabu mwanademokrasia Jakaya Mrisho Kikwete. Hafai kwa gume lililo katika jumba jeupe!! Umepatia kuhusu hiyo timu!! itammudu!!!
 
Kati yao hakuna anayefanya hata biashara ya sabuni za kutengeneza mitaani.

Hawana hela wala ushawishi. Huwezi endesha chama kwa posho za ubunge.

Lowassa tu ndo anajua hela na ana hamu ya kushika ikulu.

Wote tupa huko kijijini wawe wajumbe ya vijiji.
 
Sijui kama huyo lisu et al unamtakia mema, mtafutie chama kingine
 
ww ufipa# unasema hakuna hata kati yahao ww utaka nan ayefaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…