Lipumba: UKAWA imepoteza lengo kwa ujio wa Lowassa, wabunge wahongwa kumkubali

Mpuuzi kabisa wewe! Watu wanajadili sukari kilo moja kuuzwa bei ya kitoto cha mbuzi, Waziri kutuhumiwa kufanya biashara na wizara yake halafu hajafukuzwa anakuja kufukuzwa kwa kuonja pombe, watu wanajadili suala la wanafunzi 78002 kutimuliwa chuo UDOM Wewe unakuja na habari za Prof wa economics ambaye HANA mbele wala nyuma! Wewe ni nyumbu wa serengeti kwa kuwa nimeambiwa wa manyara wana walau kiakili kidogo
Reality is an illusion to many small minded laggards who find it too hard to see even if given a telescope.
 
H
Huyu jamaa akiongea mambo ya uchumi wa nchi nakuwa upande wake ila kwa alioyaongea leo siungi mkono hoja.
Huwezi kumuunga mkono Prof kwa kuwa na wewe ulininuliwa! Kwani mtu akinunua shamba ananunua na mazao yake. Lowasa aliinunua chadema na Ukawa na wabachama wake na washabiki wote
 
Hivi ule utafiti rwanda alimaliza au bado? Wenye taarifa tupeni basi tujue huyu mchumi anamawazo gani
 
wanafunzi waende nyumbani kwanza, kuliko kuendeleo kukaa chuoni bila ya masomo, alafu hoja ya kuwa wanaangaika mtaani ni uongo kwani kipindi yupo chuoni hawapikiwi kila mtu anatumia ela yake kutoka mfukoni either ya mkopo au kwa wazazi wao, unaposema wanaenda kujiuza kipindi hiki walipoambiwa warudi nyumban si kweli, pengine labda ni tabia zao tuu na si kuwa wanatafuta hela,
Isee hadi nakuonea huruma !!? ndo maana siku hizi siingii JF kila mara , this is new generation of GT!!
 
Sourse please! Kama kweli Prof kayasema hayo basi TAKUKURU na vyombo vingine vya dola viwashughulikie hao wote waliotoa na waliopokea hizo rushwa, pamoja na wale waliokusudia kuhujumu mtandao wa mawasiliano wa uchaguzi. Wafikishwe haraka kwenye mahakama ya mafisadi mara itakapofunguliwa mwezi Julai.
 
Na Chotipembe Ntuguja.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesikitishwa na mwenendo wa UKAWA kwa sasa.Akihojiwa na mwandishi wetu amesema "Ndugu mwandishi UKAWA ilikuwa na lengo kuu moja tu,kudai katiba iliyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba na tulijimbanua na hata nafsi zetu ziliamini hivyo, kosa kubwa tuligeuka kokoro kuwaweka waliopinga katiba ya wananchi mbele kwa kifupi ujio wa Lowassa na kundi lake umeondoa maana ya UKAWA".

Mwanasiasa na mchumj huyo nguli pia anasema alipata shida kwani alishuhudia matumizi makubwa ya hela ambazo zilielekezwa kuwalipa wabunge na viongozi wengine wa UKAWA ili wamuunge mkono Lowassa awe mgombea uraisi "Mimi binafsi nilishangaa mmoja wa wenyeviti wenza wa UKAWA akinishawishi kuwa nichukue hela hizo ambazo yeye alikiri kupokea ili kupozwa na hili kwangu lilinifedhehesha kwani sikuelewa mantiki ya kulipwa pesa na nikaamua nikae pembeni kwani wimbi hilo lilikuwa ngumu kulizuia".Aidha Prof.Lipumba ameeleza kuwa ni ngumu kwa Mh.Lowassa kuzungumzia katiba ya Warioba kwani baadhi ya wajumbe wa iliyokuwa tume ya katiba mpya walishawahi mara kadhaa kuwaeleza jinsi gani mwanasiasa huyo na wengine waliokuwapo CCM walivyokuwa na misimamo mikali." Ninachoweza kukuambia huwezi ukawaweka hawa watu mstari wa mbele halafu ukategemea watakemea ufisadi au kutetea mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba".

Prof.Lipumba alimweleza mwandishi kuwa moja ya mambo niliyoambiwa na mmoja wa viongozi wa UKAWA huku akijigamba akinishawishi "Prof. nakuhakikishia kuwa hatujakurupuka tuliwasiliana na Lowassa miaka kadhaa iliyopita na sasa mpango umekamilika tunakwenda kushika dola,Huyu mtu amejipanga ana wataalamu kutoka amerika na ulaya ambao wamebobea kuendesha propaganda na kuhujumu mitandao,sisi nia yetu tushinde au tuunde serikali ya umoja wa kitaifa kama Kenya na pia wamarekani wanataka yeye ndiye awe raisi" niliyatafakari(Prof.Lipumba) maneno yale nikajiuliza kwanini huyu mtu anatamani uraisi hivi?kwanini awape hela viongozi na wabunge wa UKAWA?Kwanini kulikuwa na makubaliano ya siri na mtu wa CCM?.Profesa Lipumba alimalizia kwa kusema kumbe yawezekana siri nyingi za mazungumzo ya UKAWA yalikuwa yanavuja.

Nawasilisha taarifa hiyo kama ilivyokuja.Tujadili kwa upendo.
siasa zngne bana!huyu lowasa hamuoni kama mnampaisha badala ya kumchafua!?nikamtazamo kangu tu bwanamkubwa!
 
UKAWA wataishia kupiga kelele miaka yote lakini Ikulu hawataingia kamwe mpaka watakapowafukuza mafisadi kutoka CCM. Huwezi umwita mtu fisadi akiwa upande mwingine halafu mtu huyo huyo na kwa kinywa chako wewe mwenyewe ukamwita ni msafi kwa sababu tu yupo upande wako. Kwa sasa historia ndiyo inayowahukumu UKAWA kwa kuwa walikula matapishi yao. Mungu hamfichi mnafiki fungu lake.
 
Kesi hii itakuwa nyepesi sana. Yaani tuna mashahidi wa nguvu kuanzia Prof. Lipumba, Prof. Kikwete na Dr. Slaa.
 
Nasikia Prof. Lipumba kagonga mwamba kurudishwa ktk nafasi yake ya uenyekiti huko CUF

Na kama ni kweli anayasema haya (japo siamini kama haya yametoka kwa Lipumba kweli zaidi ya propaganda mufilisi za kutoka Lumumba), basi itakuwa ni hasira na sasa anaanza ku create stories zisizokuwa na kichwa wala miguu!!

Which is which sasa kwa sababu hata yeye ilisemekana alilambishwa karibu zaidi ya TZS 3bn na watawala wa CCM ili kui surrender nafasi ya uenyekiti taifa CUF kwa lengo la kuwachanganya UKAWA wapoteane na wapoteze attention ya uchaguzi na CCM wapate agenda?

Atuambie sasa kwamba dau la Lowassa lilikuwa dogo na akazidiwa na dau la watu wa "kitengo" Kikwete/CCM na kuamua kuchukua lao!!

Hii kitu ni kama hai sound wala kuingia ktk akili za watu wenye akili timamu na kubwa...eti eeh!!??
 
Na Chotipembe Ntuguja.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesikitishwa na mwenendo wa UKAWA kwa sasa.Akihojiwa na mwandishi wetu amesema "Ndugu mwandishi UKAWA ilikuwa na lengo kuu moja tu,kudai katiba iliyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba na tulijimbanua na hata nafsi zetu ziliamini hivyo, kosa kubwa tuligeuka kokoro kuwaweka waliopinga katiba ya wananchi mbele kwa kifupi ujio wa Lowassa na kundi lake umeondoa maana ya UKAWA".

Mwanasiasa na mchumj huyo nguli pia anasema alipata shida kwani alishuhudia matumizi makubwa ya hela ambazo zilielekezwa kuwalipa wabunge na viongozi wengine wa UKAWA ili wamuunge mkono Lowassa awe mgombea uraisi "Mimi binafsi nilishangaa mmoja wa wenyeviti wenza wa UKAWA akinishawishi kuwa nichukue hela hizo ambazo yeye alikiri kupokea ili kupozwa na hili kwangu lilinifedhehesha kwani sikuelewa mantiki ya kulipwa pesa na nikaamua nikae pembeni kwani wimbi hilo lilikuwa ngumu kulizuia".Aidha Prof.Lipumba ameeleza kuwa ni ngumu kwa Mh.Lowassa kuzungumzia katiba ya Warioba kwani baadhi ya wajumbe wa iliyokuwa tume ya katiba mpya walishawahi mara kadhaa kuwaeleza jinsi gani mwanasiasa huyo na wengine waliokuwapo CCM walivyokuwa na misimamo mikali." Ninachoweza kukuambia huwezi ukawaweka hawa watu mstari wa mbele halafu ukategemea watakemea ufisadi au kutetea mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba".

Prof.Lipumba alimweleza mwandishi kuwa moja ya mambo niliyoambiwa na mmoja wa viongozi wa UKAWA huku akijigamba akinishawishi "Prof. nakuhakikishia kuwa hatujakurupuka tuliwasiliana na Lowassa miaka kadhaa iliyopita na sasa mpango umekamilika tunakwenda kushika dola,Huyu mtu amejipanga ana wataalamu kutoka amerika na ulaya ambao wamebobea kuendesha propaganda na kuhujumu mitandao,sisi nia yetu tushinde au tuunde serikali ya umoja wa kitaifa kama Kenya na pia wamarekani wanataka yeye ndiye awe raisi" niliyatafakari(Prof.Lipumba) maneno yale nikajiuliza kwanini huyu mtu anatamani uraisi hivi?kwanini awape hela viongozi na wabunge wa UKAWA?Kwanini kulikuwa na makubaliano ya siri na mtu wa CCM?.Profesa Lipumba alimalizia kwa kusema kumbe yawezekana siri nyingi za mazungumzo ya UKAWA yalikuwa yanavuja.

Nawasilisha taarifa hiyo kama ilivyokuja.Tujadili kwa upendo.
Anasema alikataa pesa alizoshawishiwa kuzichukua, mbona hatwambii jinsi alivyo ondoka kwenda rwanda siku alipo jiondoa cuf?
 
Kwa sasa huwezi kusikia hata kidogo mtu wa UKAWA anazungumzia UFISADI. Je, mtu anayekuwa bubu kutamka neno UFISADI anaweza kuongoza nchi?
 
Back
Top Bottom