Askofu Mwanamapinduzi ametoa hotuba mda mchache uliopita akiyasema haya uliyoyaandika hapa.Mtu mmoja aliwahi kuniambia usemi unaosema tujifunze kwa makosa hauko sahihi kwani kuna makosa hayatakupa muda wa kurekebisha chochote.
Ni kwa sababu ya hiyo dhana namuona Ruto alikuwa na nafasi nzuri sana ya kuimbwa na historia kama Rais aliyejali wanyonge kwa kupunguza matumizi ya wakubwa.
Bahati mbaya amechelewa maana kwa vyovyote atakavyofanya sasa itaonekana ni kwa sababu ya presha ya wananchi.
Hayo mambo aliyoyaamua yapo sana hata hapa kwetu yaani bunge kujadili mafao ya wake za viongozi wakati tuna waalimu ambao wanalipwa laki tatu na nusu na watu duni wengi tu.
Naomba Serikali zetu zitumie hili saga la Kenya kujifunza kuachana na matumizi ya kijinga yasiyoendana na uhalisia wa maisha ya watu wanaowaongoza.
Zaidi ya hayo naomba watawala wetu waachane na machawa na wasifiaji wavae uhalisia wa maisha ya watu wao na shida zinazotesa watu na wasiwachukie wakosoaji maana mkusanyiko wa wakosoaji wengi ndio huzaa uasi.
Tatizo nikuwa sisi ni Maiti, watawala wana uhakika kuwa maiti haziwezi kufufuka na kudai haki zao!