Kwetu Kakola na Msalala

Kwa taarifa yako wanaohusika si wabunge wa msalala na nyang'hwale tu bali hata mbunge wa jimbo la Busanda anahusika Kwa sababu barabara inayotoka geita inapita jimbo la busanda kabla ya kuingia jimbo la msalala.
 
Na pale Nyakagwe jirani na Bulyanhulu pakoje sasa? Tulikuwepo huko miaka ya themanini.
Nyakagwe ipo mkuu ila same issue is happening,hakuna miundo mbinu wala mpangilio.serikali wanakusanya mapato kwa wachimbaji wadogo wadogo ila bahati mbaya hakuna mrejesho wa pesa hizo kwa wananchi kufanyiwa maendeleo.
 
Kwa taarifa yako wanaohusika si wabunge wa msalala na nyang'hwale tu bali hata mbunge wa jimbo la Busanda anahusika Kwa sababu barabara inayotoka geita inapita jimbo la busanda kabla ya kuingia jimbo la msalala.
Asante sana kaka kwa kunielewesha,tuwaombe sasa watufanyie kazi.hata kama serikali haina pesa,wawekezaji hawa wakibanwa vizuri mbona barabara inakuwa sawa?hata lami tutapata,mgodi wa geita,bulyanhulu na buzwagi wote wanahusika na hili.ila sijui ugum uko wapi
 
Hivi ukiwa unatoka segese ,nyasubi, hadi kijiji kimoja,kinaitwa ntobo,barabara Ina hali gani kwa sasa?nakumbuka siku za nyuma hali ikua mbaya sana.
 
Picha, nmesoma shule ya Kakola darasa la kwanza na nilipanda mti mwaka 98,vp kampuni ya Tanzoro bado ipo?
Weka picha
Kampuni ya Tanzoro iliondoka miaka ya 2004 kama sijakosea.
Mwenye kampuni yule (George) mzungu alifariki, na kisha mkewe (Rose) binti wa kitanzania aliamua kubadili kampuni na kuiita Tanrose. Hili alishirikiana na aliekua muhasibu wa iliokua Tanzoro, ili kufanikisha zoezi lao la kudhulumu mali za marehemu George.
Baada ya hapo mgogoro mkubwa ulitokea kati ya watoto wawili wa marehemu George (Tanzoro) kuingilia kati ufedhuli ule, pia nakumbuka walisaidiwa na ubalozi wa nchi aliokua akitokea marehemu George, kwakua ilisemekana George alipeleka documents za Kampuni, Accounts na Urithi kule ubalozini kwao kwakua alianza kutokua na imani na mkewe Rose.
 
Nimewahi kufanya kazi Na Barrick baadaye Accacia ,duuuuhhhh jamaa wanaondoka na utajiri wetu mpaka huruma.
Ila ACCACIA si wakulaumiwa kwani ni wafanyabiashara tu na kazi yao ni kuona kampuni inapata faida.Wakulaumiwa ni Mkapa na wengineo
Kabla haijaitwa Barrick......
Ilikua ikiitwa Kahama Mining Cooperation Limited (KMCL).
Hapa ndipo nilipo shuhudia alicho pewa mkapa kama zawadi siku ya ifunguzi wa uzalishaji.
Ufunguzi huu nakumbuka ulifanyika ndani ya moja ya ghala la kuhifadhia madawa wakatiule likiwa bado jipya........
Na kisha baada ya Mkapa kupewa kile kilicho itwa zawadi...... Nakumbuka kilifungashwa na mmoja wa wakubwa wa kitengo cha ulinzi kwa jina la John Bwana, na kisha aliibeba zawadi ile kwenye sanduku madhubuti (safe box)...... Haooooo wakalipeleka kwenye uwanja wa ndege pale Bulyanhulu, tena zawadi ile ikiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
 
Kampuni ya Tanzoro iliondoka miaka ya 2004 kama sijakosea.
Mwenye kampuni yule (George) mzungu alifariki, na kisha mkewe (Rose) binti wa kitanzania aliamua kubadili kampuni na kuiita Tanrose. Hili alishirikiana na aliekua muhasibu wa iliokua Tanzoro, ili kufanikisha zoezi lao la kudhulumu mali za marehemu George.
Baada ya hapo mgogoro mkubwa ulitokea kati ya watoto wawili wa marehemu George (Tanzoro) kuingilia kati ufedhuli ule, pia nakumbuka walisaidiwa na ubalozi wa nchi aliokua akitokea marehemu George, kwakua ilisemekana George alipeleka documents za Kampuni, Accounts na Urithi kule ubalozini kwao kwakua alianza kutokua na imani na mkewe Rose.
UMENIKUMBUSHA mbali sana... nilikuwaga Process plant, kati ya wale waanzilishi....

Nimekaa Kakola kijijini then camp
 
Kabla haijaitwa Barrick......
Ilikua ikiitwa Kahama Mining Cooperation Limited (KMCL).
Hapa ndipo nilipo shuhudia alicho pewa mkapa kama zawadi siku ya ifunguzi wa uzalishaji.
Ufunguzi huu nakumbuka ulifanyika ndani ya moja ya ghala la kuhifadhia madawa wakatiule likiwa bado jipya........
Na kisha baada ya Mkapa kupewa kile kilicho itwa zawadi...... Nakumbuka kilifungashwa na mmoja wa wakubwa wa kitengo cha ulinzi kwa jina la John Bwana, na kisha aliibeba zawadi ile kwenye sanduku madhubuti (safe box)...... Haooooo wakalipeleka kwenye uwanja wa ndege pale Bulyanhulu, tena zawadi ile ikiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Nilikuwepo.... ilifanyika karibu na portable water plant.... NDO TUKAPEWA MAKAVU LIVE NA MKAPA KWAMBA WATANZANIA TUACHE WIVU KWA WAWEKEZAJI...

Na John bwana alivyokuwa anajipendekeza kwa wazungu, balaa
 
Hivi ukiwa unatoka segese ,nyasubi, hadi kijiji kimoja,kinaitwa ntobo,barabara Ina hali gani kwa sasa?nakumbuka siku za nyuma hali ikua mbaya sana.
Kuanzia Manzese, Ntobo, Segese, Lunguya, Ilogi, Bugarama hadi Kakola..... Pote barabara niya hovyo kabisa.
Jaribu kufikiria, kama kutokea manzese (lami) ambapo ni njiapanda ya kuelekea Kakola kutokea kahama ni umbali wa 75 kilometers, hapo gari hutumia masaa mawili hadi masaa mawili na nusu....
 
Nakumbuka kwenye kibasi kakola..... enzi za DASH8
Nimekumbuka siku nilipo ng'oa mzigo pale kibasini, kisha nikaenda kupanda nao DASH-8..... Mzigo hauja pandisha majini..... .... Ilibidi ndege igeuke na kutua kwa dharura huku wakidhani kwamba ndege imetekwa....
Na hapo ndipo ilipo anzia sheria ya kwamba..... Yeyote anae taka kumpandisha mdada kwenye ndege ya kampuni, lazima athibitishe kwamba ni mkewe....
Hatari sana DASH-8......
 
Ahahahahaaaa kumbe ndo weweee..... aiseeee.... dunia kijiji
 
Back
Top Bottom