Kimemeta
Senior Member
- Dec 27, 2017
- 181
- 233
Maana ya Mfungo wa Kikristo
Mfungo kadiri ya mafundisho ya Kikristo sio kushinda njaa, Mfungo ni mazoezi ya kiroho. Mkristo hafungi kuacha uzinzi, uongo, ulevi n.k, katika kipindi cha Kwaresma tu na kuendelea na mambo hayo baada ya Kwaresma, la hasha. Mkristo anatumia kipindi cha Kwaresma kujizoeza kuacha mambo hayo katika maisha yake yote.
Mkristo anafunga kula sio ili ashinde njaa na kula kile chote ambacho angekula mchana wakati wa jioni, la hashaa. Mkristo anafunga kula au kunywa au kwenda kwenye starehe ili kile ambacho angekula au kunywa au kustarehe awape maskini wahitaji na kwa kufunga hivyo ajenge mazoea ya kuwapa maskini na wahitaji badala ya kufuja yeye mwenyewe katika maisha yake yote.
Kufunga ni toba, ni kumrudia Mungu kwa kuwa na kipindi kirefu cha tafakari na baada ya hapo kuamua kuishi hayo mazoea. Mfungo kikristo ni mazoezi ya kiimani ili baada ya hapo tuendelee kuishi hivyo na sio kuacha baada ya siku 40 na kurudia dhambini.
Wakristo tusije fika mahali tunafanya "vunja jungu". Kwamba nafanya madhambi yote kabla ya Kwaresma halafu Kwaresma naacha. Baada ya Kwaresma narudia madhambi kama kawaida hapana, huu sio mfungo wa Kikristo.
Hii ni tafakari yangu kuhusu mfungo.