Tokyo40
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 2,065
- 1,925
I think siyo kweli, unachosema. Kama umesoma kwenye Chuo kikuu chenye hadhi yake naamini siyo rahisi uwakute hao walio kufundisha wewe, unless umepitia hizo zinazo jiita university colleges na msurulu wa Degree za online. Hizi ndo zile zilizo wapa PhD akina mama Lwakatare and others.
Vyuo vya miaka miwili Marekani, "community colleges", walimu wengi hawana Ph.D.
Hivi ni vyuo vya serikali na vipo katika kila jimbo. Ukimaliza unapata shahada ya AA, "Associate Degree".
Vyuo vingine vinawaajiri meneja wa zamani wenye uzoefu katika masoko fulani ya makampuni ya kimataifa kama Pepsi Asia au Samsung South Africa katika somo la "international business management" katika vyuo vyao.
Wanataka kuwafundisha wanafunzi kazi watakazofanya na mtu aliyofanya hiyo kazi, nje ya "theories".
Ukihitimu na M.F.A, unaweza kufundisha kama mtu mwenye Ph.D. Hamna degree juu ya hapo kwa masomo ya "arts, design, theatre and dance".
Lakini upo sahihi, asilimia kubwa ya vyuo vikuu vya daraja la kwanza, walimu wana Ph.D katika fani zao, lakini siyo lazima ili ufundishe.
Harvard, Princeton na Yale wanawaalika wafanyabiashara maarufu wa dunia kuja kufundisha chuoni kwa muda mfupi. Wengi hata chuo hawajamaliza kama Steve Jobs, Ted Turner, David Kurp na Bill Gates.