Kwanini wamarekani weusi hulalamika wanapouawa na wamarekani weupe, Ikiwa wao wenyewe pia huuana?

Wa salaam wanajamvi.

Swali langu ni hili: Kwanini wamarekani weusi hulalamika wanapo kojolewa na wamarekani weupe, Ikiwa wao wenyewe hunyeana?

Hivi punde kumetokea mauaji ya kijana mweusi huko marekani yaliyofanywa na afisa wa polisi (ambaye ni mzungu) . Na kila mtu analijua hilo. Ila cha kushangaza zaidi ni pale tunaona watu wengi weusi kutoka pande mbalimbali za ulimwengu wakilaani tukio hilo.

Mbona haya manung'uniko hayashiki hatamu pale wamarekani weusi wanapo uana wao kwa wao.?

Hivi mnajua kuwa vifo vinavyotokana na mauaji ya watu weusi(wenyewe kwa wenyewe kuchomana "Visu" & "Risasi") ni vingi kuliko vile vinavyotokana na mauaji na watu weupe(wazungu kuua watu weusiy)?

Kwa nini kifo kinacho sababishwa na mzungu kionekane kina mzizi wa "Ubaguzi wa Rangi".?

Ninawaomba wamarekani" weusi" wapunguze kuendekenda ubaguzi wa rangi. Waamini kuwa kufa kwa mmarekani mweusi hakusababishwi na ubaguzi wa watu "weupe" bali ni mitazamo yao isiyo sahihi, pia wazingatie maisha ya watu weusi yaliyoangamia kutokana na watu weusi.

Kama kweli wanamaanisha wanaposema #BlackLivesMatter, basi waniksikie nisemavyo, huenda wakanielewa kabla hakuja kuchwa.

YMCMB Headquarters.
Sijui ni infiority complex au? maana mauaji yakifanywa na mtu mweupe dhidi ya mtu mweupe tunayapuuzia tu japo ni umwagaji damu ya binaadam mwenzetu, au mtu mweusi akiua mtu mweupe haistui sana ila mtu mweupe akiua mtu mweusi tunakimbilia kujadiri rangi, mimi nadhani tujikite kulaani mauaji ya watu suala la rangi lisiingizwe hata kidogo
 
Ingawa sijaelewa mantiki ya mtoa mada.....lakini sidhani kama hata anaelewa malalamiko ya hao wamarekani weusi juu ya mauaji hayo.........

Habari za kuuana wao wao ni vitu vya kawaida kwenye jamii yoyote hasa hiyo ya huko ulaya ambapo silaha zimezagaa kama njugu......

Mzizi wa tatizo ni polisi ambaye ni mwana usalama ambapo anatakiwa kulinda usalama wa raia na mali zao.....matokeo yake yeye ndio amekuwa tishio la huo usalama hasa kwa watu wetu weusi........

Unaweza ukaniambia kuwa kulikuwa na ulazima gani kumfyatulia risasi mtu ambaye tayari mmeshamdhibiti na yuko chini ya imaya yenu kama vyombo vya usalama.........

Kulikuwa kuna ulazima gani wa kumfyatulia risasi mtu ambaye umemuamuru akupe leseni yake...!!??

Mauaji wanayofanyiana watu weusi wao kwa wao hakuhalalishi kuwa wao ndio watendewe hivyo hivyo na vyombo vya usalama.........

Ingawa inafahamika kuwa mkoa wa Mara ni mkoa ambao mauaji ni vitu vya kawaida lakini hiyo haifanyi polisi kuwatendea wakaazi wa huko kwa kuwa wao wanapenda kuuana......
 
Huyu original poster nae si mtu mweusi? Ni tatizo wewe tena ni snitch mkubwa, hayo mauaji wanauana wenyewe yanapingwa sana na yanazidi kupungua, na imesababishwa na hali za maisha wengi wao wanaishi as a result if unfair treatment ya us government towards them tokea enzi.
Polisi wanapaswa kuwalinda sio kuwaua pasipo sababu alafu hakuna hatua zinachukuliwa.

Nyie house nigas ndio tatizo.
 
Ni sawa kulalamika na kupaza sauti pale walipo ona mweusi mwenzao amefanyiwa yasiyo haki, ila naona kama hao hao wamarekani weusi wanatumia nguvu kubwa kupaza sauti kwenye mauaji yanayo husisha "interracial" zaidi kuliko yale mauaji ambayo wanafanyiana wao kwa wao (ambayo ni mengi zaidi).
You have to walk in their shoes to understand. It's hard to understand if you have never been there.
 
Huyu original poster nae si mtu mweusi? Ni tatizo wewe tena ni snitch mkubwa, hayo mauaji wanauana wenyewe yanapingwa sana na yanazidi kupungua, na imesababishwa na hali za maisha wengi wao wanaishi as a result if unfair treatment ya us government towards them tokea enzi.
Polisi wanapaswa kuwalinda sio kuwaua pasipo sababu alafu hakuna hatua zinachukuliwa.

Nyie house nigas ndio tatizo.
Kwa kuwa mimi mweusi unatarajia nitetee jambo lolote ambalo linafanywa na mtu mweusi hata kama haliClick akilini mwangu?
 
Ingawa sijaelewa mantiki ya mtoa mada.....lakini sidhani kama hata anaelewa malalamiko ya hao wamarekani weusi juu ya mauaji hayo.......

Ingawa inafahamika kuwa mkoa wa Mara ni mkoa ambao mauaji ni vitu vya kawaida lakini hiyo haifanyi polisi kuwatendea wakaazi wa huko kwa kuwa wao wanapenda kuuana......

Kinachonisibu akilini mwangu ni kuona mambo 2 yanachukuliwa kwa uzito Tofauti.

Kwanza: Mauaji ya watu weusi kwa weusi.
Piki: Mauaji ya watu weupe kwa weusi.

Nayaelewa malalamiko yao, ila swali ni Kwanini mauaji wa wao kwa wao hawayachukulii kwa uzito sawia kama mauaji haya ya Jana....?

Wenyewe wana ka'msemo wanasema #BlackLivesMatter. Kwamba maisha ya watu weusi yathaminiwe. Sasa najiuliza tu, wazungu wanaanzaje kuheshimu maisha ya watu weusi ikiwa wao(weusi) ndio wanao ongoza kuuana wao kwa wao!?
 
Sijui ni infiority complex au? maana mauaji yakifanywa na mtu mweupe dhidi ya mtu mweupe tunayapuuzia tu japo ni umwagaji damu ya binaadam mwenzetu, au mtu mweusi akiua mtu mweupe haistui sana ila mtu mweupe akiua mtu mweusi tunakimbilia kujadiri rangi, mimi nadhani tujikite kulaani mauaji ya watu suala la rangi lisiingizwe hata kidogo
Sawa kabisa!

Kinacho takiwa ni kwamba kulaani mauaji ya aina yote katika misingi sawia.

Hili suala la kutumia jitihada nyingi kulaani mauaji ya Blacks yanayo fanywa na white enforcers..... na kupotezea mauaji ya Blacks by Blacks ni ujinga ulio pitiliza na usio na msingi.
 
Nadhani sina la kukupinga kwa unayo yasema. Nimaanishacho ni kuwa :- waache unafiki.

Unajua, watu weusi(Marekani) kujifanya kuthamini maisha ya mtu mweusi mwingine pale anapo uawa na mtu mweupe ni unafiki wa hali ya juu. Ikiwa wao kwa wao huuana kwa wingi mno.

Kwa nini hawathamini maisha yao, hata wawe wanauana kwa wingi, achilia mbali suala la kuuawa na law enforcers.

Waanze kwa kupaza sauti mauaji ya wao kwa wao nami ndipo nita waunga mkono wanapo paza sauti za mauaji yatokanayo na law enforcers.
Tatizo sio kuuawa na mweupe, Bali issue ni polisi mweupe
 
Wa salaam wanajamvi.

Swali langu ni hili: Kwanini wamarekani weusi hulalamika wanapo kojolewa na wamarekani weupe, Ikiwa wao wenyewe hunyeana?

Hivi punde kumetokea mauaji ya kijana mweusi huko marekani yaliyofanywa na afisa wa polisi (ambaye ni mzungu) . Na kila mtu analijua hilo. Ila cha kushangaza zaidi ni pale tunaona watu wengi weusi kutoka pande mbalimbali za ulimwengu wakilaani tukio hilo.

Mbona haya manung'uniko hayashiki hatamu pale wamarekani weusi wanapo uana wao kwa wao.?

Hivi mnajua kuwa vifo vinavyotokana na mauaji ya watu weusi(wenyewe kwa wenyewe kuchomana "Visu" & "Risasi") ni vingi kuliko vile vinavyotokana na mauaji na watu weupe(wazungu kuua watu weusiy)?

Kwa nini kifo kinacho sababishwa na mzungu kionekane kina mzizi wa "Ubaguzi wa Rangi".?

Ninawaomba wamarekani" weusi" wapunguze kuendekenda ubaguzi wa rangi. Waamini kuwa kufa kwa mmarekani mweusi hakusababishwi na ubaguzi wa watu "weupe" bali ni mitazamo yao isiyo sahihi, pia wazingatie maisha ya watu weusi yaliyoangamia kutokana na watu weusi.

Kama kweli wanamaanisha wanaposema #BlackLivesMatter, basi waniksikie nisemavyo, huenda wakanielewa kabla hakuja kuchwa.

YMCMB Headquarters.

Two wrongs don't make a right. The problem is not whites killing blacks, the problem is law enforcement officers charged with upholding said law killing minorities at disproportionate rates. Black on Black crime is indeed crime, the job of law enforcement is to fight said crime not killing innocent people. By the way even "criminals" have rights too, there should be no reason for anyone to be killed unless the life of an officer is in mortal danger, which is not the case in many of these cases we are seeing. Whatever happened to tasers!?

We can say its not racism but when a you see videos of white men walking the streets with rifles and guns meant for war and not even get arrested albeit in some states it is legal to carry arms openly, yet on the other hand a 12 years old black boy gets shot within two seconds of an officer arriving on the scene for playing with a TOY gun (mind you Ohio is one of these open-carry states), you have to wonder if there is not a bias out there.

Are there problems within the black community? Yes, but that's where government institutions and law enforcement are supposed to work with the community to solve those problems not to add to them.
 
Halafu cha kushangaza wamarekani weusi hujiona bora zaidi kuliko watu weusi kutoka Africa na huwa wanawabagua. Hubweteka na kujiona wako juu wanasahau kuwa ni watumwa.
 
Halafu cha kushangaza wamarekani weusi hujiona bora zaidi kuliko watu weusi kutoka Africa. Hubweteka na kujiona wako juu wanasahau kuwa ni watumwa tu.
Binadamu wote wanafanana na tabia zao ni moja... Hata wewe huwa unawaona wapemba ni watu tofauti haswa pale wanapotoa rafudhi... utasikia Mpemba huyo kana vile wewe ni bora zaidi yake
 
Binadamu wote wanafanana na tabia zao ni moja... Hata wewe huwa unawaona wapemba ni watu tofauti haswa pale wanapotoa rafudhi... utasikia Mpemba huyo kana vile wewe ni bora zaidi yake
Binadamu wote hawafanani na tabia zao si moja. Halafu hilo swala la wapemba unanisingizia.
 
Binadamu wote hawafanani na tabia zao si moja. Halafu hilo swala la wapemba unanisingizia.
Kama Ubishi basi umepitiliza duh Binadamu hawafanani? naosha mikono juu yako...

Huo ni Mfano tu nimekupa regard watu unaowaona Wamarekani weusi kujiona zaidi ya Wausi wanaotoka Africa... ni hivi

Binadamu yeyote au hata Viumbe hai alomost vyote vikifanana huwa vinaelewana iwe Maua,Miti,Majani,Ndege,Wanyama,Wadudu n.k Sema sometimes kunakuwa na Matabaka ndani yake kutakuwa na wanaoelewana na wasioelewana so kwenu mkizaliwa saba watatu wakawa ni albino basi nyie mlio weusi mtajiona ni bora zaidi ya hao albino, Mhindi wa Africa akifika India ataonekana sawa na mhindi wa India ila akijitambulisha Ametoka Africa basi wakati huo huo atadharaulika kwa namna moja au nyingine, Mzungu wa Armenia akienda England anadharaulika pia, Even Wadudu wanyama ni the Same tuna asili ya ubaguzi piga ua..

So usisangae kuona nigga anamdharau nigga wa Africa kuna sababu Nyingi kwani wao wamezaliwa kwenye System yao ambayo imepangika na akijua wewe umetoka kwenye System mbovu Africa na umeenda kuwachukulia fursa kwao hakika atakuwa anakumind tu... Acha Kushangaa We Komaa tu waislam husema Mtumikie kafiri upate....
 
Back
Top Bottom