Wadau amani iwe kwenu,
Kama kichwa kinavyosema hapo juu naomba kujua ni expansion ya namna gani inafanyika pindi ukipika mchele?
Unaweza ukaweka mchele robo sufuria lakini baada ya kuiva unakuta sufuria imejaa? Je, ni nini kinafanyika?
Mnaweza kuona ni swali la ajabu kuwahi kutokea ndani ya viunga vya JF lakini nimejiuliza sana leo bila mafanikio
Hili limekuja wakati nikiwa nakula wali leo, sasa nikajaribu kulinganisha punje ya wali ulioiva na ya mchele ambao bado haujapikwa, Cha kushangaza punje zote zinalingana ukubwa, kama kujaa kwa sufuria ni kutokana na expansions ya mchele, nilikuwa natarajia nione punje ya wali ikiwa kubwa kama ya maharage lakini sivyo, punje ya wali na ya mchele zote zinafanana kwa ukubwa.
Je, hii inatokana na nini?
Jamani uwezo wangu wa kufikiri uliishia hapo, naombeni mnijibu kwa ustaarabu.
NB. Mimi sio mzawa wa Koromije, vyeti ninavyo Ila hili limenishinda.....