Kwanini Tiketi za UDART/MaxMalipo hazioneshi kiasi cha nauli kilicholipwa?

Mkuu Barbarosa mleta mada ana hoja ya msingi hao Dart et al..wanategemea mawazo na ushauri kutoka kwako na kwangu ili waboreshe huduma vizuri tafadhali usibeze ushauri wake ni wa muhimu.


Wanahitaji ushauri ndiyo, lkn siyo kila ushauri, kuna mambo mengine ni common sense tu, mtu hawezi kujenga mradi wa mabilioni na kutumia Wahandisi na Wachumi waliobobea halafu ashindwe kuona kwamba kwenye tiketi hakujaandikwa bei wakati tayari ameshakwambia kwamba yuko kwenye majaribio ni kwa nini usisubiri amalize hatua ya majaribio ndiyo kama hilo halijarekebishika ndiyo uanze kulalama?

Au maana ya majaribio haieleweki?
 
Barbarosa
Mimi siitaji mafanikio ya kijinga kama uliyofundishwa wewe, that's so y mpaka leo unasubiri kufanikiwa inabidi ufanye jitihada uonane na wanajf live ndipo kauli zako utaziweka kwenye indoor boxer!!.
 

Attachments

  • 1463653491176.jpg
    1463653491176.jpg
    35.5 KB · Views: 45
Ndugu mradi bado uko kwenye majaribio hivyo kuna mambo mengi bado hayajakaa sawa kuweni na subira angalau mjaribu kukosoa baada ya miezi mitatu, watu kama ninyi sidhani kama mtakuja kufanikiwa maishani kwani mmejikita zaidi kwenye negativity klk positivity!

We jamaa unajifanya unaipenda nchi kuliko watu wote ,mzalendo we we,wengine sio wazalendo, sasa bila kusema izo kasoro wahusika watajuaje, acha ujinga wako wewe,,,,,yaan siasa zimemaliza akili yako aisee, huruma Sana, jamaa ameeleza vizuri nakuomba wahusika wayafanyie kazi,wewe unamponda,
 
Kwani ukiandika kiingereza ndiyo kuna kitu umebadilisha? Mabasi yako kwenye majaribio hata mwezi hayamaliza na hata DART wenyewe wamesema wako kwenye majaribio au hauelewi maana ya majaribio?

Kwani Wazungu wenu huwa kwanini wanafundisha Kiingereza chao lkn hawawapi akili zao?
Majaribio ni majaribio kila kitu kinajaribiwa kama kiko sawa au unafikri ktk DART yoote wewe tu ndiyo umeliona hilo??

We ni mjinga hakyamungu, siasa zimemaliza akili yako, umu kuna wazalendo na nchi kuliko wewe, bila watu kueleza changamoto wanazokutananazo ktk uho usafiri wa mwendo kasi, wahusika watajuaje ili warekebishe mambo yaende vizuri,
 
Siku nyingine jaribu kuwa na subira na uvumilivu hiyo ndiyo siri ya mafanikio maishani na siyo kutaka kila kitu kiende jinsi unavyotaka wewe kwa kuwa tu wewe unataka hivyo hata pale ambapo tayari umekwisha ambiwa kwamba wako kwenye majaribio!
Kwaiyo kipindi hiki wapo kwenye majaribio ht tukimuona mtu Ana hujumu kwa namna moja au nyingine watu wasiseme au au kutoa ushauri,
 
Kwaiyo kipindi hiki wapo kwenye majaribio ht tukimuona mtu Ana hujumu kwa namna moja au nyingine watu wasiseme au au kutoa ushauri,
Mkuu, ndio maana nikamua kumpuuza, Barbarosa hajitambui, mtu yeyote anayekosoa chenye mahaba yake, huyo ni adui, haitakii mema nchi na sio mzalendo. Kaazi kweli kweli.

Vv
 
Tiketi inaonyesha ulipotoka ila sehemu unapoenda haionyeshi. Sio kweli kwamba haionyeshi sehemu zote mbili.
Usisahau kuna insurance wakati wa ajali nao ni wadau katika suala la tiketi. Ila tatizo lingine hizo tiketi hazioneshi sehemu ulipotoka na unapokwenda.
 
Watu wote waliofanikiwa maishani wana tabia moja ambayo huwatambulisha nayo ni
,,subira na uvumilivu"
sasa wewe umeshaambiwa kwamba mabasi yako kwenye majaribio na wala mwezi mmoja hayajamaliza kwanza hata nauli zenyewe ndiyo wameanza kutoza baada ya kuwa yanachukuwa watu bure na ni swala la muda tu kabla hawajalifanyia kazi, na ndiyo maana wamesema wako kwenye majaribio au hilo neno labda halieleweki maana yake?!

Sasa kama unashindwa kuwa na ,,subira na uvumilivu" kwa jambo ambalo tayari umekwisha ambiwa kwamba liko kwenye majaribio unawezaje kufanikiwa maishani?
Kwa maana mambo yote maishani yanafanana, na yanahitaji ,,subira na uvumulivu"

Hujielewi..hivi basi linakuwaje kwenye majaribio huku limebeba watu tena wamelipa nauli!? Ikiwa utaona ni sawa haya! Je kwa nn watoe risiti feki kwa fedha halali!? Ni majaribio ee!? Haya, bosi wako kazini anakurudishiaje nauli uliotumia ambayo haionekani!? Eti majaribio...waache wizi mara moja! Hizi nauli zilishalalamikiwa ni kubwa, na sasa hawaziandiki kwenye risiti, unahisi nn hapo?
 
We jamaa unajifanya unaipenda nchi kuliko watu wote ,mzalendo we we,wengine sio wazalendo, sasa bila kusema izo kasoro wahusika watajuaje, acha ujinga wako wewe,,,,,yaan siasa zimemaliza akili yako aisee, huruma Sana, jamaa ameeleza vizuri nakuomba wahusika wayafanyie kazi,wewe unamponda,

Hajielewi, anafikiria wanaopinga hili ni ukawa na ule mrdi ni wa chama chake!
 
Hivyo wewe chill and relax rudi baada ya miezi 3 kwa sasa shukuru angalau hata mabasi yapo na yanafanya kazi!

Eti rudi baada ya miezi mitatu watakuwa wameshashiba siyo?
Zile siku za majaribio kazi yake ilikuwa nini?
 
Nimepita leo Daraja la Mwl Nyerere, tiketi zao ziko clear, zinaonyesha kiwango halisi cha gharama za kuvuka na aina ya gari.

Vv
 
Hili swala jana alilizungumzia mkurugenzi wa maxmalipo, wamesema wameshapata malalamiko na swala lipo mezani, linafanyiwa kazi. Hizo ni changamoto tu, kila ikija changamoto ni wajibu wao kuifanyia kazi coz wapo kwenye transition period.
Ni kweli wako kwenye transition period. Ila inabidi tujiulize kwa suala la msingi kama kiwango cha nauli kwenye ticket, kinakosekanaje? Mtengeneza hiyo system ya ticket alikuwa na idea gani kichwani kama gharama ya tiketi yenyewe si miongoni mwa parameters anazohusisha kwenye system yake?
 
Lingine ambalo limeshtua leo hii ni hili;

Ukikata tiketi na kwenda kupita kwenye vile vyuma kuna mtu una mkuta anachukua na kuipitisha/ana scan kuonesha umepita, lkn isipo_scan anakwambia pitia upande huu, akimaanisha upande usio na vyuma vya kukuruhusu kupita.

Sasa basi, moja kwa moja uki_scan inaonekana kwenye system na isipo_scan inaonekana kuharibika hivyo kuna nini kinachopelejea hizo tikiti zengine zisisome?

Au ndio kutengeneza pesa mapema kabla hawajastuka?

**Binafsi nilikataa a_scan nika_scan mwenyewe na ikakubali!!.


NOTED.
Mkuu hii kitu mi ilinitokea jana nikitoka ubungo kuja kimara waliscan ilikuwa inagomagoma ndo wakanambia pitia upande mwingine ila sikujua makusudi yao ila mi nilifikiria labda mashine huwa zinagomahoma na nilikuwa na haraka sikufatilia zaidi kwann iwe hivyo..

HILI NI JIPU TUNAOMBA MAMLAKA HUSIKA NA TRA WAFUATILIE KWA UMAKINI .
 
Piga utume , na kituo ulichokatia pia useme. ...otherwise tutaona ni story za kutuchangamsha humu.
Mkuu mi ilinitokea jana pale ubungo maji pindi najiandaa kupanda gari kuja kimara wahusika wafuatilie kwa umakini kuna mapato yanapotea mengi sana afu yaweza kuta ni vituo vingi vinavyofanya hivyo..!!
 
_hivi wagonjwa wa akili nao mmo humu jf..!!

Ulifundishwa na wazazi wako watu wanaofanikiwa hawakosoi jambo?

Au shule uliyopitia umeambiwa ukianzisha biashara TRA watakupa machine na karatasi zake kwa ajili ya majaribio?
& na POLE SANA!!
Akili zao wamempa Knana
 
Mimi naona ni mapungufu na sehemu ya changamoto tu, mradi ndiyo kwanza umeanza hata mwezi hauna hivyo tulipaswa tuwaache DART wafanye kazi yao angalau baada ya kuanzia miezi 3-6 ndiyo tuanze kukosoa, kwani watu wenyewe bado wako kwenye majaribio na sidhani kama wewe peke yako ndiyo utakuwa umeliona hilo!

Hivyo wewe chill and relax rudi baada ya miezi 3 kwa sasa shukuru angalau hata mabasi yapo na yanafanya kazi!
Kuwa kwenye majaribio sio sehemu ya phase ya huu mradi. Siku ulipozinduliwa ndio umeshaanza. Hakuna sehemu yoyote kwenye mkataba wa uendeshaji wa huu mradi unaosema "kutakuwa na muda XXX wa majaribio". Hata hivyo, nani kasema mradi ukiwa kwenye majaribio, watu wasitoe maoni yao kwenye mapungufu. Bila ku-pin point mapungufu hiyo dhana ya majaribio itatekelezeka vipi? Mtoa mada, katoa maoni yake na kuomba wahusika washughulikie hilo sasa hapo tatizo ni nini? Wewe ni mmoja wa wale wanaotaka kusifiwa tuu 24/7
 
Back
Top Bottom