Kwanini TBC hawarushi matangazo ya madawa ya kulevya?

martini enock

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
635
273
Shalooom watanzania popote mlipo,
Awali ya yote nikipongeze chombo cha habari Clouds Tv kwa kutuletea habari za madawa ya kulevya.
Kuna maswali kama mawili yananisumbua sana;

Kwanini TBC television 1 kwenye kampeni za uchaguzi mkuu walikuwa wakirusha matangazo. Kwenye vita hii Kubwa ya madawa ya kulevya hairushi kwanini?

Je, Kampeni za uchaguzi mkuu zina uzito mkuu
Kuliko kampeni za madawa ya kulevya?

Naomba kusaidiwa kwa maswali haya.
Asanteni sana.
 
Leo hii mkutano wa tatu na waandishi wa habari umerushwa Live na vituo binafsi vya TV ikiwemo Clouds TV, cha ajabu TV ya serikali ambayo ni TBC haionyeshi mkutano huo. Hii ni ajabu sana ukizingatia kuwa mheshimiwa Raisi ametangaza vita kali sana dhidi ya madawa haya. Je TBC haiungi mkono vita hii?
Leo ndiyo siku ya kwanza Kamishna wa madawa ya kulevya akianza kazi, Je TBC kwa nini hairushi hili tukio live?
 

Wanasubiri Wabunge wawapitishie ' Bajeti ' yao Kwanza.
 
Nape kakataa
 
Hawana fungu la madawa ya kulevya ,yaani wameshtukizwa na hii kampeni tusubiri mwakani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…