Kwanini taifa la Venezuela ni maskini licha ya kuongoza kuwa na mafuta mengi duniani?

crankshaft

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,414
3,394
Kwa mujibu wa tafiti, taifa la Venezuela ndilo lina hifadhi kubwa ya mafuta duniani ikifuatiwa na mataifa ya middle east kama Saudi Arabia, Iran,n.k

Wakati haya mataifa kama Saudi Arabia yakiwa na ukwasi mkubwa kutokana na rasilimali hiyo ya mafuta, kwa nini hawa Venezuela ni maskini na hatuoni wakiwa na jeuri ya pesa kama wenzao Saudi Arabia na waarabu kutokana na utajiri huo wa mafuta?
 
Kwa mujibu wa tafiti, taifa la venezuela ndilo lina hifadhi kubwa ya mafuta duniani ikifuatiwa na mataifa ya middle east kama saudi arabia, iran,n.k

wakati haya mataifa kama saudi arabia yakiwa na ukwasi mkubwa kutokana na rasilimali hiyo ya mafuta, kwa nini hawa venezuela ni maskini na hatuoni wakiwa na jeuri ya pesa kama wenzao saudi arabia na waarabu kutokana na utajiri huo wa mafuta??
Kwani Tanzania Ni mfano Kwa Venezuela?
 
Hao jamaa walikua vizuri sana kiuchumi enzi the Chaves back in the days. Economic sanction ndio imewapoteza vibaya
 
Nigeria ni ya pili kwa kuzalisha mafuta duniani ya kwanza Saudi Arabia.

Dubai ina mkojo wa punda lakini tajiri kuliko Nigeria.

Nakupa mfano wewe nipe jibu.

Tanzania nchi pekee yenye kuzalisha Tanzanite duniani, lakini India nchi ya kwanza duniani yenta tanzanite nyingi kwanini?.
Wachimbaji wa Tanzania na wauza wa India wapi matajiri?.
 
... tatizo nchi inaongozwa na madikteta wasio na maono zaidi ya ufisadi chini ya lichama lenye mrengo mfu wa kijamaa lazima nchi ichakae vibaya!

Una macho huoni? Mifano iko miguuni pako bado huelewi? Aaaghrr!
 
Kwa mujibu wa tafiti, taifa la venezuela ndilo lina hifadhi kubwa ya mafuta duniani ikifuatiwa na mataifa ya middle east kama saudi arabia, iran,n.k

wakati haya mataifa kama saudi arabia yakiwa na ukwasi mkubwa kutokana na rasilimali hiyo ya mafuta, kwa nini hawa venezuela ni maskini na hatuoni wakiwa na jeuri ya pesa kama wenzao saudi arabia na waarabu kutokana na utajiri huo wa mafuta??
U communist, kama anavyoujaribu Tanganyika .
 
Kwa sababu limekuwa likiongozwa na watu wajinga wajinga kwa muda mrefu sana.
 
Hao jamaa walikua vizuri sana kiuchumi enzi the Chaves back in the days. Economic sanction ndio imewapoteza vibaya
Hawakuwa vizuri, Chavez hakujenga uchumi endelevu wa nchi na wala hawakufanya uwekezaji wowote wa maana nje ya sekta ya mafuta crude, hiyo nchi karibia kila kitu wanaagiza kutoka nje, hadi mafuta yao wenywe refined!. Kiongozi mwenye akili siye anayewagaia watu nyumba, chakula na mahitaji mengine bila kuwa na mpango wowote wa kuwafanya wajitegemee wenyewe kupitia kazi za mikono yao.
 
Nigeria ni ya pili kwa kuzalisha mafuta duniani ya kwanza Saudi Arabia.

Dubai ina mkojo wa punda lakini tajiri kuliko Nigeria.

Nakupa mfano wewe nipe jibu.

Tanzania nchi pekee yenye kuzalisha Tanzanite duniani, lakini India nchi ya kwanza duniani yenta tanzanite nyingi kwanini?.
Wachimbaji wa Tanzania na wauza wa India wapi matajiri?.
Nigeria sio ya pili kwa kuzalisha mafuta Duniani. Taarifa yako sio sahihi.

Lakini pia Saudi Arabia sio ya kwanza, ni ya pili ya kwanza ni Marekani.

Nigeria hata top 10 ya nchi kubwa za kuzalisha mafuta haipo.
 
Back
Top Bottom