Timu zote ambazo zilikuwa na wachezaji kwenye time ya Taifa baadhi ya mechi ziliahirishwa, Azam, Simba na Yanga wote walikuwa na viporo, tofauti tu ni kwamba kiporo cha Yanga kilichezwa mapema kipindi kile ameenda Tanga kucheza na Mgambo ilibidi hats kiporo chake na African sports ilibidi akimalizie kulingana na ratiba ilivyokuwa imekaa pamoja na ratiba ya African sport. Viporo vya Azam na Simba vilichelewa sababu ni ratiba ilivyokaa.
Kuhusu Simba kucheza mechi nyingi ugenini katika mzunguko wa kwanza, ni kweli ni nyingi lakini si asilimia 90. Simba kacheza mechi saba nje ya Dar, bado mechi tano, mechi Tatu haijarishi ni nyumbani au ugenini lakini zitachezwa Taifa.
Kwa mechi alizocheza nje ya Dar hadi sasa ni chini ya asilimia 60.