Kwanini maeneo mengi ya biashara ya chakula huwa wanishindwa kudhibiti nzi?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
45,346
63,912
Kwenye maeneo mengi ya biashara za vyakula hasa migahawa ya ukubwa wa kati na midogo pamoja na sehemu nyingi za nyama huwa kunakuwa na nzi wengi sana waliojaa kila mahali.

Yani mtu unakula chakula na mkono mmoja huku mwingine una kazi ya kufukuza nzi!

Kama wewe sio mvivu na hupendi nzi, kwa wale wavivu wa kufukuza nzi wao huwa wanaachia tu nzi na kula nao chakula pamoja.

Hawa wanaouza vyakula katika haya maeno kipi huwa kinawashinda kutumia sabuni kali na zenye harufu kali kufutia meza zao, kudekia, kuosha vyoo pamoja na kuoshea vyombo ili kudhibiti nzi??
 
Wanazuilika, hotel kubwa nyingi wanazodumisha usafi nzi huwa hakuna kabisa au wachache sana.
Ni gharama kubwa kuwaondoa kwa kufanya hayo mazingira kuwa safi muda wote.
Inaonesha hao nzi hawajawa tatizo kwa wateja walio wengi hivyo hakuna ulazima wa kuingia hizo gharama.
Biashara ni ujanja, inategemea umelenga wateja wa aina gani.

Wewe utakuwa ulijichanganya kwenye hoteli zisizoendana na standard zako.i
 
Kwenye maeneo mengi ya biashara za vyakula hasa migahawa ya ukubwa wa kati na midogo pamoja na sehemu nyingi za nyama huwa kunakuwa na nzi wengi sana waliojaa kila mahali. Yani mtu unakula chakula na mkono mmoja huku mwingine una kazi ya kufukuza nzi! Kama wewe sio mvivu na hupendi nzi, kwa wale wavivu wa kufukuza nzi wao huwa wanaachia tu nzi na kula nao chakula pamoja.

Hawa wanaouza vyakula katika haya maeno kipi huwa kinawashinda kutumia sabuni kali na zenye harufu kali kufutia meza zao, kudekia, kuosha vyoo pamoja na kuoshea vyombo ili kudhibiti nzi??
Una uhakika kuwa hao ni nnzi? Wasije akina Mshana wakakucheka hapa bure 🤔🤸😄

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Yoda na agenda zake ambazo ni ndoto za mchana kwa shithole countries.

Mi nashangaa, mbona majumbani hamna nzi? kama wapo wawili au wa3 tu, labda ukikaanga samaki wanaruka ruka huko nje baada ya muda wanapotea.
 
Wanazuilika, hotel kubwa nyingi wanazodumisha usafi nzi huwa hakuna kabisa au wachache sana.
Nikweli mkuu lakini pia si kweli.

Iko Hivi hoteli hizo kubwa Unakuta sehemu ya kupikia/kuangalia chakula ni sehemu nyingine na sehem ambayo wewe unaptengewa msosi na kuanza kula.

Sasa ukihitaji kujua Hilo nenda wanakopikia na kuoshea vyombo ndo utajua hujui.

Cha msingi sana hakikisha chakula chako ni Cha moto tu inatosha.

Muda mwingi Nzi ni kipimo Cha kuwa chakula chako ni salama hata ukichemsha Sasa.

Mfano ukienda bucha lolote ukakuta hakuna Nzi hata mmoja kwenye nyama hiyo.

Fanya maamzi ya kutokununua hapo.
Mara nyingi hutumia chemical mbaya sana hata za maiti kutunza Ile nyama isiharibike mapema ama kufukuzwa Nzi.
 
Back
Top Bottom