Kwanini kwenye mitihani hairuhusiwi kushirikiana?

Engineer Hassan

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
477
503
Hili swali nimekuwa nikiuliza mara kwa mara ila nashindwa kabisa kupata jibu la kuridhisha kabisa.

Mimi navyoona labda kungekuwa na utaratibu wa kuruhusu wanafunzi waweze kuingia na reference zao mbalimbali kwenye vyumba vya mitihani kwa sababu hata huko kazini wanapoenda huwa wanabeba documents kwa ajili ya reference maana kuna wengine wanakuwa vitu wanajua ila uwezo wa kukumbuka unakuwa ni mdogo kwa hiyo mwisho wakifanya mtihani wanaonekana hawajui kumbe vitu kuvijuwa wanavijuwa sema uwezo wa kukumbuka unakuwa ni mdogo.

Pia nashauri wanafunzi waruhusiwe kufanya mitihani kwa kushirikiana ili iwajengee mazoea ya kufanya kazi kama teamwork maana hata kazini kaI hufanyika kwa teamwork hasa kazi zetu hizi za uhandisi. Sasa kama huyu mtu ukimjengea mazoea ya ubinafsi tangu ngazi ya awali hata huko mbeleni kufanya kazi kwa ushirikiano pia inakuwa sio kwa ufanisi mkubwa kivile

Halafu mwisho siku nia ya kumpika/kumfundisha mwanafunzi ni kwaajili ya kumtengenezea mazingira ya kujua vitu na kuweza kufanya kazi kwa ushirikiano na wafanyakazi wenzake na wala si kumfundisha mwanafunzi ili umpime uwezo wake wa kukariri.
 
Mwanafunz anatakiwa kufanya mtian mwenyew ili kupma uwezo wake yeye kama yeye na pia kiwango chake cha uelewa
 
Wakifanya kwapamoja utajuaje nan aliparticipate ful na nan alitegea? Itakua ngumu kutoa judgement ya mmoja mmoja na kama team work hua zinatolewa sana tu darasan, kuanzia primary group works kibao, secondary pia zpo plus presentation chuo ndo usiseme, yan mtu akiwa mbinafsi au akishindwa kufanya team work hlo ni tatzo lake bnafsi sio kwasababu alifanya mtihan peke ake
 
Kuhusu kuingia na materials, open test znafanyishwaga na still watu wanafeli, yan kama hujui ni hujui tu, huon mtu anaingia kwenye mtihan na four figure bt hajui kuitumia? Kama hujasoma/hujui swal utaishia kupekua hayo material uloingia nayo had muda utaisha huna la maana ulilofanya
 
Hairuhusiwi kwa kuwa Certificate za kuhitimu Masomo hazitolewi kimakundi, Cheti kinatoka kwa Jina lako
 
Hivi Mimi sielewi,kwanini kiongozi sifa yake ni kujua na kuandika,harafu dreva anaetakiwa kumuendesha kiongozi huyo inabidi awe amefika form four?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…