Habari zenu.
Mimi ni Raia mwema ambaye huwa siegemei upande wowote wala sio mkereketwa wa chama chochote cha siasa hivyo hata kwenye uchaguzi kura yangu huwa siangalii chama wala jina la mtu bali mimi huwa naangalia sera nzuri na historia nzuri ya mgombea anayehitaji kupewa kura ya uongozi.
Na bila kuficha uchaguzi uliopita nilivutiwa sana na Ndugu. JPM kutokana na sera zake nzuri kipindi cha kampeni na hata historia yake nzuri ya uchapaji kazi kipindi cha nyuma ni moja ya vitu vilivyonivutia kumpa kura yangu ya uraisi. Hivyo kura yangu ya uraisi ilienda kwa Jpm na Ubunge nilimpa wa CUF
Hayo yote ni kulingana na sera zao nzuri ambazo zilinivutia hivyo nikawapa kura yangu bila ya kuangalia chama chochote
Lakini hivi majuzi baada ya Jpm kufanya mambo ambayo ni kinyume na Ahadi zake ambazo alizitoa kipindi cha uchaguzi imenipa hasira na hivyo bila kuwa mnafki nimekuwa nikimkosoa pale anapokosea na mazuri huwa namsifia
Lakini kila nlipomkosoa kuna vijana humu walikuwa wakinirushia maneno makali kama
"WEWE NYUMBU TU"
"CHAGADEMA HILI"
"JPM WANYOOSHE"
"DJ MBOWE KAKUTUMA?"
"KILAZ.A WA CHADEMA"
Na chama nikapewa kabisa. Lakini nnachojiuliza ni nani anapaswa kumkosoa rais anapokosea?
Kwa nini kila anayemkosoa sizonje awe ni chadema tu?
Kwai hamna wana ccm na wanacuf wanaoisoma namba?.
Inamaana yanayoendelea yanawaumiza wanachadema peke yao? Wana ccm mnataka mtuambie kuwa nyie mna maisha mazuri sio?