Kwanini hakuna anayeondoka/hama CCM, bila ya kukataliwa na CCM??

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Hili swali nimekuwa nikijiuliza na sipati jibu, mpaka leo hii hakuna hata mtu mmoja ambaye amewahi kuhama CCM kujiunga na Chama kingine kwa hiari, yaani akaamua tu mwenyewe kwamba CCM haiendani na kile anachokiamini basi akahama, ni mpka apale anaponyimwa kitu fulani chenye maslahi binafsi kwake!

Nikianzia na W.Slaa lkn siyo kwa umuhimu kwani kuna wengi waliohama kabla yake, W. Slaa aliondoka CCM tu na kuhamia chadema baada ya kuondolewa kwenye kura ya maoni hivyo kama asingeondolewa angebakia CCM, E. Lowasa, huyu Lowasa alikuwa CCM mpaka dakika ya mwisho alivyoshindwa kupata nafasi ya kuwa Mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM ndo akahama CCM, Sumaye naye ni kama Lowasa, Lembeli huyu naye hivyo hivyo baada ya kusoma alama kwamba CCM walikuwa hawana nia ya kumsimamisha Ubunge akahamia chadema, Kingunge baada ya kuona Mgombea aliyemtaka ameshindwa kupitishwa na CCM, akahama Chama!

Haya Wema Sepetu, huyu alikuwa CCM kwa mujibu ya maneno yake mwenyewe kwani binafsi nilikuwa sijui kama Wema ni CCM, mpaka pale aliposhitakiwa kujihusisha na Madawa ya kulevya na kwa maneno yake mwenyewe CCM imemtelekeza akaamua kuhama Chama na kwenda chadema, hivyo sababu ya kuhama kwake ni kesi yake ya madawa ambapo annalaumu CCM kutokumtetea, lkn siyo Sera wala Itikadi ya CCM iliyomuhamisha!!

Sasa ukiangalia wote hawa, najifunza jambo moja kwamba kinachowaondoa CCM siyo itikadi au Sera za CCM, bali ni ulaji na ubinafsi, kwamba walitaka CCM iwafanyie jambo fulani imeshindanikana sasa wameamua kuondoka, hivyo basi maadamu kilichowakimbiza CCM siyo msimamo wa Kiitikadi isipokuwa maslahi binafsi hata huko walipokwenda maslahi binafsi yatawaondoa pia, hivyo ningekuwa Chama ambacho hawa wamekimbilia ningejiuliza haya maswali na kutowawapa nafasi ya Uongozi hawa watu kwani hakuna wanachosimamia isipokuwa maslahi, na kama ulikuwa unatafuta ushahidi wa hili ni W. Slaa kilimuondoa CCM ndicho kwa namna moja au nyingine kilichomuondoa chadema na zaidi, na itakuwa hivyo kwa kwenda mbele kwa wote hawa akina Wema, Lowasa, Sumaye &Co.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…