Kwani Makonda? Makonda ni Makonda

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
218
230
Anaandika Mo Mlimwengu.

Kila zama huwa zina nyakati zake. Siku zote lila na fila havitangamani na mwenda tezi na omo marejeo ngamani. Maandishi haya ya wahenga yanafanya Makonda aendelee kuwa suluhisho la watanzania.

Makonda ni mwanasiasa wa kisasa ambaye kajitofautisha na viongozi wengi sana katika nchi hii. Huenda mimi siyo mfuasi wake lakini mchawi lazima apewe sifa zake. Makonda ni mchezaji ambaye huenda kwenye kikosi cha watu 11 hana ushirikiano na wenzake lakini usipompanga huwezi kupata matokeo unayoyataka ya ushindi wa kikosi kizima. Kocha mzuri anaamua kuchagua kipaji chake kuliko sifa zake zingine ambazo hazitaathiri ushindi wa kikosi kizima.

Hii ndio inafanya nione Rais wetu ni kocha mzuri ambaye anaelewa mchezaji wake ampange katika nafasi gani? Kutokana na mahitaji ya mchezo husika. Kuna wakati anakupanga ili kulinda matokeo ambayo yameishapatikana, kuna wakati anakupanga ili ulinde mpate suluhu na kuna wakati anakupanga ili uwavuruge wapinzani watoke kwenye mchezo halafu anaongeza mshambuliaji matokeo yanapatikana kiulaini.What a coach?

Uongozi wa Makonda umejikita zaidi upande wa wananchi. Yuko tayari kugombana na viongozi wenzake kwa maslahi mapana ya wananchi. Kwa hili kwanini wananchi wasimpende? Kwanini wananchi wasione yeye ni kimbilio lao. Kwa hili kajipanbanua vizuri na wananchi wanamuelewa na kumuelewa. Ni mtu wa kutaka matokeo haijalishi atatumia njia ya mkato ambayo haijzoeleka kwa watu wengi. Lakini njia hizo hizo ndio zinazofanya awe kipenzi cha wananchi ambazo mimi na wewe tunaweza kuzipinga.

Hii imepelekea kila mtu aamini shida yake wakuitatua ni Makonda tu. Kuna dogo mmoja nilikuta kadisco chuo fulani kwa uzembe wake lakini anaamini ni Makonda anayeweza kumrudisha masomoni. Ndio maana hata watu wengine tuliona wakimpelekea kero za kufarakana kimahusiano ya mapenzi. Tujiulize kwanini wanampelekea yeye na siyo viongozi wengine? Jibu ni kwamba wanaamini atatatua hapo hapo pasipokuzungushana kama wafanyavyo wengine. Ndani ya ofisi za umma issue ya kutatuliwa siku moja unaweza kuzungushwa hata mwezi na hakuna anayejali. Watu hawawajibiki ipasavyo kwenye nafasi zao.

Kuna makundi ya watu wanaomkubali Makonda na kuna makundi ambayo hawamkubali Makonda. Lakini ukiangalia makundi ambayo hayamkubali kwa asilimia kubwa wanaona kama anawazibia ridhiki zao au ni ile dhana ya kutomkubali mtu hata kama hajakutendea chochote. Watanzania walio wengi wanampenda na wanamuombea kwa Mungu. Ndio maana hata baada ya uteuzi wake kuwa RC vyombo vyote vya habari vilimjadili yeye. Utasema amekuwa demoted au kawa promoted ila kwa Makonda hata akipewa nafasi yeyote anaifanya at the maximum.

Kwa sasa Makonda ni kijana ambaye ni mwanasiasa maarufu na pendwa kuliko mtu yeyote. Viongozi walijizolea ushawishi wakiwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini Makonda amekuwa kivutio kwa watu wengi kabla ya kuingia kwenye eneo hilo. Kwa kipaji chake na kipawa chake ukimpa wizara yeyote ataitendea haki. Makonda ni risk taker ambaye ana uthubutu wa kuzungumza yale ambayo hatujazoea kuona yakizungumzwa kwa uwazi.

Mlimwengu mimi ninamtakia heri kwenye nafasi ya Ukuu wa Mkoa wa Arusha. Arusha ni mkoa wa kimkakati ambapo kuna shughuli za kitalii, uchimbaji wa madini, migogoro ya wakulima na wafugaji na migogoro ya wananchi na mbuga za hifadhi. Ninaamini ataenda kuitendea haki na kuifanya Arusha watu waijue zaidi. Mwisho niseme Makonda ni Makonda na hicho ndio kinafanya watu wampende.

Photo credit: clouds tv

#mlimwengumimi
#makondakazini
 
Attachments

  • FB_IMG_1712578192806.jpg
    FB_IMG_1712578192806.jpg
    44.4 KB · Views: 7

Takataka
 
Mkuu, umeeleza sawia kabisa

Ukitaka usipendwe na wasomi wezi wa nchi hii, basi shughulika na kero za wananchi

Utachukiwa na kuandikwa vibaya kwenye kurasa za wasomi wezi hao mpaka basi

Makonda piga kazi, acha wasomi wezi wapige kelele!
 
Ndio ukweli wenyewe
 
Duh. Utafanya watu waanze kujiteka huko Arusha ili waseme ni yeye.

Subiri uone.
 
Siasa ni kusaidia wananchi sasa kama huwasaidiii unategemea nini

Mkuu wa Mkoa anafanya kazi kama.waziri/mbunge anaingia front kuliko wabunge wenye majimbo yao.

Mkuu wa mkoa anapiga left na right, Kuna muda utafika Rais hatokua na option zaidi ya kumpa madaraka makubwa zaidi MAKONDA.

MUDA utasema
 
Back
Top Bottom