Kwako Mbwana Mshindo mtangazaji wa habari za michezo pale Channel ten

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,783
17,304
Ndugu Mbwana Mshindo salamu zipate, popote pale ulipo najua pengine upo humu unasoma hii ujumbe.

Wewe ni mtangazaji mzuri mno, hukosei kosei, maneno yanatoka safi kabisa na una flow vizuri hongera sana.

Ila unapokosea katika kutangaza pale jambo likaenda mrama usipanick na kuloose confidence kabisa ukatoka nje ya mood, take it easy ndugu mshindo kila mtu anakosea relax.

Mfano, habari ya juzi kati umekaribishwa kwenye michezo ndugu yangu pale mwanzo tu ukakosea basi ukatoka kabisa kwenye mood wakati ni jambo la kawaida tu.

Wewe ni Mtangazaji mzuri sana, unapowasilisha taarifa ya michezo ukiwa nyuma ya kioo unasound good sana hukosei kabisa wala kutetereka.

Ni hayo tu, uko vizuri sana mkuu.

Kisa Mwaipyana nakusalimia dada yangu kama upo humu nitafute.
 
Back
Top Bottom