Hakika tutakumbuka daima Faru John, kwani umetutoka kimazingara na wakati bado tunakuhitaji hapa Duniani. Ni vigumu kuamini kama umetutoka basi salamu zetu zikufikie popote pale ulipo.
Ewe Faru John huko ulikokwenda ukibahatika kukutana na Mwalimu, mwambie bado tuna mkumbuka Sana, tunakumbuka busara zake, ujasiri wake na maono yake kuhusu hii klabu yetu.
Mwambie lile Gari alilo liacha hapa klabuni sio salama tena kusafiria. Madereva makondacta na wapiga debe wamekuwa jeuri kweli kwa abiria.
Ukibishana nao tuu hawakushushi kituoni kwako, watasafiri na wewe umbali mrefu kisha utashushwa eneo usilo lijua na kupotezwa huko na kuwa mwisho wako wa uhai au wakutese vikali sana .
Mwambie sio tuu binadamu wanao fanyiwa ufilauni huo hata wanyama pia nao sasa wanafanyiwa hivyo hivyo. Mpe Ukweli jinsi wewe ulivyo potea na jinsi tunavyo kutafuta mpaka sasa bila mafanikio.
Ukiwa ndani ya gari abiria hatutakiwi kuongea, kukosoa au kutoa maoni yetu juu ya mwendo kasi wa gari hili na usalama wetu. Ukimwambia dereva spidi mbona Kali hapo mbele kuna kona dereva anajibu jeuri yeye kafuzu na hajaribiwi.
Gari tunaliona linarudishwa nyuma kwa spidi kali ukiuliza kwa nini utaambiwa gari linaenda mbele kama hutaki kusafiri shuka na mizigo yako hupewi na hata nauli hurudishiwi.
Mwambie mwalimu hapa ninapo ongea nimejificha chini ya buti la gari ili wasinione nikiongea hawa wapiga debe wakanipoteza. Gari lipo spidi kali abiria wamechoka njaa Kali lakini dereva hataki kusimama tule na hatujui anaenda wapi.
Najua itamsikitisha Sana mwalimu kusikia habari hii juu ya Gari alilo tuachia linavyo tumika vibaya. Ila msisitizie asinitaje kuwa ni mimi nimempa taarifa. Madereva wenyewe hawa hatuwaamini wengi wanatumia vilevi wanaweza kukugonga na gari kwa makusudi.