Clever505
JF-Expert Member
- Jul 27, 2020
- 1,162
- 2,178
Mimi sio mpenzi sana wa kufatilia mpira, huwa nacheki games muhimu tu ambazo zinazungumzwa sana mitandaoni. Sasa kuna baadhi ya vitu natamani kuvijua. Kwa sababu humu kuwa wakongwe wa haya mambo naamini nitapata kuelewa.
Huwa najiuliza maswali haya,
_ hivi wale linesman huwa hawaruhusiwi kumshinikiza refa wa kati kutoa kadi? Nauliza hivo kwa sababu siku moja nilienda uwanjani kuangalia mechi ya fainal ya mapinduzi kati ya singida na mlandege nilikaa upande ambao nilikuwa namuona kwa ukaribu kaseke, jamaa alikuwa anamfokea sana linesman mara kwa mara. Ndo nauliza haiwezekani refa huyu akaenda kumwambia refa wa kati ampe kaseke kadi kwa ukosefu wa nidhamu?
_ kipa akionyeshwa kadi nyekundu huwa anatolewa mchezaji mmoja wa ndani, je ikishatokea hivo then kipa akafanya kosa lingine anaonyeshwa nyingine red au inaanza tena njano ndo ifate red?
_ Huwa naona mfano ikitokea mechi imeenda sare then dakika za mapenati zinakaribia wanaingizwa kwa haraka wachezaji maalumu kwa ajili ya kupiga penalty ama kipa, je ni kwamba wakati penalt zinaendelea hairuhusiwi kuingiza mchezaji!, Kama hairuhusiwi ni kwa nini iwe hivo wakati hizo penati zipo ndani ya muda wa mechi?
_ Mpira unapotoka kwenye uwanja kwa nini huwa unarushwa na si kuwekwa chini ukapigwa Kama faulo?
_ Mpira wa kurushwa ukiingia golini, goli linahesabika?
_ Mfano likipigwa shuti moja kali linaonekana ni on target kabisa na kipa anaonekana kabisa ameshalala upande mwingine then likambabatiza refa na kwenda nje hapo maamuzi gani huwa yanafanyika.
_ Mara kadhaa nimeona refa akifunika tuta wachezaji huwa wanamzonga sana kulalamikia maamuzi hayo. Je yale malalamiko yalishawahi kumfanya refa abadili maamuzi? Kama sivyo, wachezaji kufanya hivo huwa ina faida gani ikiwa inajulikana wazi maamuzi hayatabadilika?
_ Ikitokea tatizo lolote litakalosababisha mechi isiendelee, muda huo kuna timu inaongoza mfano magoli mawili na mechi ikapangwa kurudiwa siku nyingine. Mechi itaanza palepale ilipoishia nikiwa na maana kwamba kama ilikuwa dk ya 55 itaanza palepale au inaanza upya?
_ Mchezaji akionyeshwa kadi nyekundu hachezi mechi tatu zinazofata kama sijakosea. Ikitokea kadi nyekundu akaipata kwenye mechi ya mwisho wa msimu, hiyo adhabu atakuja kuitumikia msimu unaofuata au msimu ukianza unaanza upya na kila kitu?
_ Mchezaji akitolewa anaweza akaingia tena?
_ hivi ni lazima timu iweke mfumo ule wa 4 4 2 au 5 3 2 ? Timu ikiamua wachezaji wote wacheze tu bila mpangilio inaruhusiwa? Yaani wanaamua wote wanakaa golini kwao kulinda goli tu hadi dk ya mwisho.
_ Ikitokea mfano timu kufikia dakika ya 70 wameshafungwa 8 bila na wanahisi wakiendelea zinaweza kufika hata 12, wakiamua mechi iishe tu wamekubali kufungwa, wanaruhusiwa kufanya hivo?
Kwa leo ni hayo tu wataalamu.