Habari za mida hii GT...niende kwenye mada
Katika kujikwamua na maisha ya kawaida huenda ukajikuta unaingia benki na hivyo kufanya mawasiliano na afisa mikopo...
Picha linaanza ambapo huanza kukupigia hesabu za mkopo wa muda mrefu mfano miaka 9...
Tatizo linaanzia pale ambapo mnakubaliana kabisa mfano unaomba 12m kwa makato ya 300,000/- kwa muda wa miezi 50,
Mnakubaliana Kila kitu ..
Sasa hapa ndo watumishi hupigwa.
Moja huenda ukapewa pesa zote yaani 12m ila jumla ya pesa utakayolipa wanakuwekea 30m badala ya 15m
Au wakakupa pesa pungufu ya uliyoomba mfano wakakupa 9m badala ya 12m na jumla ya makato 30m.
Sasa ukikutana na hali hii fanya yafuatayo.
1.Mwambie afisa mkopo wako akupe mkataba akikataa force akupe maana ni haki yako
2.Ukipata mkataba angalia mapungufu yalipo
3.Ukikutana na mapungufu ,Anza na afisa mkopo wako ,mweleze mapungufu yalipo.
4.Endapo hajaelewa nenda kwa HR wako mweleze ,endapo hajaelewa nenda kwa mwajiri
Au
5.Nenda BOT kwa wakazi WA dar au mwanza waeleze changamoto Yako,ni waelewa sana na wanatatua changamoto hapohapo na tatizo lako litaisha
NB:WATUMISHI WENGI SANA WANAUMIZWA KWA STYLE HII NA WANALIPA MADENI WASIYOSTAHILI.