kamanda mbigi
JF-Expert Member
- Feb 8, 2017
- 1,241
- 1,546
Msimu wa matamko umerudi......
Sawa Mkuu, ajari haina kinga hata seatbelts hazina haja kwani hata kufa ni mpango wa Mungu, hata trafiki tunawalipa mishahara ya bure. Na kama utasema ni kupunguza basi ukiongeza tu mbinyo zinakwisha kabisa. Nenda VETA kidogo kwa kodi ya mwezi mmoja tu ya udereva, utaelewa ninachomaanisha.Acha ubishi usio na maana.
Uko sahihi kabisa.Na mimi nilikuuliza makusudi tu, nilitaka uniambie kuwa walipita barabarani, kwa dereva aliyefunzwa , barabara inazungumza nae juu ya yeye aliendesheje gari lake kwa eneo husika, kaka hulijui hilo? Kama kulikuwa na mtelemko na korongo, mita kadhaa nyuma barabara ilishamwambia, ugeni wa barabara si kings tena ndio sababu ya kuwa makini, nadhani umenielewa.
Hata kulijua gari lako ni sehemu ya majukumu ya muhimu ya dereva, daily checkups.
Mungu yupi mbaya huyo apangaye mipango miovu kama hii, hivi kweli huwa tu nasimamia tunayoyaamini? Hivi unaweza unalia na kusononekea mpango wa Mungu?Mipango ya mungu tu
Hakuna uzembe wowote hapo isikuwa ni ajali yenyewe tu wala si muda wa kumtafuta mchawi ni nani,
Halafu hii tabia ya kila tatizo linalotokea barabarani tuache kuwalaumu madereva tu....ajali ni ajali kama imeandikwa itatokea itatokea tu hata aendeshe dereva wa aina gani au miundombinu ya barabara ikawa bora kiasi gani.
Hivi ni mara ngapi tunawalaumu manahoza na malubani kwa uzembe wa ajali tena zinazoua malaki ya watu?
Au wao ndo sio wazembe au ajali zao hazitokani na uzembe?
tumlaumu nani
Hizi kanuni za uongo ni za kuridhishana na kufarijiana tu, eti ajari haina kinga, nani kasema.Tusimsingizie Mungu kila wakati.
Aina za Ajali:
-Misfortune Accident
-Accident due to Intention
-Recklessness na
-Negligence
Kwa sehemu waliyopatia ajali kama nilivyoshuhudia naweza sema kama hakukuwa na hitilafu yoyote kwenye gari (misfortune) ni uzembe kwasababu tokea mteremko mkali ulipoanzia dereva alishatembea kama mita 350 au 450 na mbele kidogo kwenye culvert ajali ilipotokea kuna corner simple lakini matata kama hamna umakini na korongo kubwa upande wa dereva lilipo angukia coster na inaonyesha kabisa kuwa kuna mteremko mkali mbele na road traffic sign ipo kabisa pale yaani exactly na ilipotokea ajali.
Napita mara kwa mara pale kwa kupanda magari ya abiria na kwa kuendesha gari au pikipiki nathibitisha madereva wapo rough sana pale huwa ni roho mkononi na sijui kwanini wanakuwaga na haraka pale coz ni kama 2 KMS mteremko wote na mpaka Karatu mjini ni 4KM tu kutokea pale.
Tusisingizie barabara maana ni nzuri sana na pana.
1 walimu.mkuu dereva na walimu wanauzembe gani?
Acts of God= Majole caseHuu msemo ulishapitwa na wakati, ajali zote zina kinga. Siku hizi dunia inaangaikia majanga ya asili, acts of God, sio ajali tena. Hatufuati sheria wala kanuni, halafu tunasingizia ajali haina kinga, za wapi hizi.
Adhabu ya nani sasa wakati mwenye kusababisha ajali alikufa pia.yeye ndo alipaswa kukataa kama amebebeshwa abilia wengi kuliko uwezo wa garisalaam,
Baada ya kushuhudia vilio vya hisia humu jukwaani,na watu wakiweka msimamo kua ni uzembe wa watu.
Naomba tu mtwambie ni ADHABU gani hasa wapewe hawa watu wazembe inayoendana na upotevu wa uhai wa hawa watoto.
NB wale wanaomini ni MUNGU,naomba mtulie kwanza.