Kwa wafanyabiashara: Unatangazaje biashara yako kwa wengine?

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,999
23,374
Kwanza napenda kusema na kukiri wazi mimi ni mmoja wa wale waliokua wakiamini katika msemo ambao watu wengi sana hupenda kuutumia kwamba kizuri chajiuza,kibaya chajitembeza huu msemo ni kweli unafanya kazi 100% hasa unapojiamini vitu unavyouza ni GENUINE 100%.

Kwenye huo msemo nataka leo wote tuwe kwenye upande wa kibaya chajitembeza sote tufanye kwamba bidhaa zetu ni mbaya hazijulikani hivyo tuamue kuzitangaza na kuzifanya nzuri,leo nitaongelea aina moja ya tangazo ambayo gharama ya hili tangazo gharama yke kila mtu anaimudu kuanzia mfanya biashara wa chini mpk wa juu kabisa.

wafanyabiashara wengi huamini Wapita njia/wateja wengi hupenda kusoma sana na ndio mana kila mfanyabiashara wa tigo pesa/duka la nguo/duka la vinywaji/duka la dawa/duka la viatu/duka la vipodozi nk nk biashara zote unazozijua hakuna mtu kafungua frem Halafu akaweka tu mzigo ndani Akaacha kuchora kwa nnje

wengi huchora kwa nnje huduma wanazotoa ndani au zinazopatikana hapo walipo lakini leo nataka kuwambia kitu wafanyabiashara wenzangu kwamba katika watu 100 wanaojua kusoma wapo 40 na wasio jua kusoma wapo 60,Chukua hiyo kutoka kwangu leo nakwambia.

sasa nataka kukwambia kitu wateja unaowapata leo sio wengi sana kwasababu ume deal na wale wateja 40 tu umewaacha wateja 60 waliobaki,sasa tunawapataje hawa wateja 60 waliobaki? tunawafahamishaje kuwa hapa dukani/ofisini tunatoa huduma flani?

SPEAKER ZA MATANGAZO

hizi speaker ni msaada mkubwa sana wa biashara zetu,hizi speaker zina faida kubwa sana lakini watu wengi hawaziweki kwenye hesabu wakati wanapofungua biashara zao,mimi mwenyewe nilikuwa sielewi siri iliyo ndani ya hizi speaker lakini sasa naelewa nataka niwashtue wenzangu ambao hamjashtuka.

Ukienda kariakoo au kwenye masoko makubwa au baadhi ya mduka utakuta wanatangaza kwa hizi speaker kazi wanazofanya au bidhaa walizonazo,lakini nataka kuwambia hizi speaker si kwa ajili ya huko mjini tu hizi speaker ni kwa biashara zote kuanzia wauza genge/tigo pesa/mama ntilie,nk nk

Nunua speaker yako mjini zipo za bei tofauti lakini usitake mbwembwe wala kuwa kero kwa wafanyabiashara wa pembeni yako nunua ndogo tu inauzwa 60,000 hii speaker ina uwezo wa kukaa na charge masaa zaidi ya matatu lakini pia hii speaker inatumia umeme kwahyo wewe ambaye upo sehemu yenye umeme ni swala la kuchomeka tu kwenye umeme kisha kazi inaendelea.

images.jpg


Nunua flash yko au memory weka kwenye card reader kisha chukua hiyo smartphone yako jirecord tangazo lako la dk 1 hakikisha tangazo lako halizidi dk 1 ongea kwa ufasaha kitu unachokifanya hapo kazini kwako.

Mfano: nachukulia mimi ni wakala wa tigo pesa/mpesa/bank

karibu ujipatie huduma za tigo pesa,mpesa,airtel money,halopesa,TTCL PESA pamoja na huduma nyingine zote za bank kama CRDB,NMB,EQUITY na nyingine zote Karibu karibu sana Tupo wazi mpaka saa 3 usiku.Karibuni sana.

Baada ya kurecord tangazo lako utalitia kwenye flash/memory yako kisha utachomeka kwenye ki speaker chako utaweka hapo nnje kisha wewe tulia zako dukani/sehemu yako ya kazi subiria utaona wateja wataokuja.

hii speaker itakusaidia kukuletea wateja wengi kuliko hayo maandishi au bango uliloweka hapo nnje ya ofisi yako,hayo maandishi kwanza yanasomwa mchana tu usiku hamna anaesumbua macho yake kuyasoma,lakini pia hayo maandishi sio kila mtu anaweza yasoma.

lakini ukiweka tangazo lako kwenye hizi speaker litakuletea wateja mchana mpk usiku wateja watakuja wengi kwani wanaosikia ni wengi kuliko wale wanaojua kusoma hivyo wale wateja wasiojua kusoma wakisikia tangazo lako utawaona wao wenyewe wakijileta kufata huduma yako.

Kama umekaa tu ukiamini wateja wameshajua biashara unayofanya kwasababu upo hapo ulipo muda mrefu sasa haujitangazi zaidi ya hayo maandishi hapo nnje na hilo bango hapo juu nataka ufahamu wateja unaowapata leo sio wengi kama ukiamua kuweka speaker ya tangazo hapo nnje kwako.

Usipuuze kama huna haka ka speaker kakanunue kaweke kisha kaa wiki 1 tu mauzo yakiwa yale yale kama ilivyokua kabla hujaweka hii speaker Rudi niite niambie Controla ulinidanganya nikapoteza hela yangu,nitakurudishia hela ya speaker uliyonunua nitaichukua mimi wewe ntakupa hela yako.




maxresdefault.jpg
 
Okay! I never knew....
Kwa hiyo spika ndio unauza shilingi ngapi?
 
Back
Top Bottom