Inauma sana! Nianze kwa kusema hivyo!
Africa tuna ardhi kubwa yenye rutuba, mbuga za wanyama, madini ya kila aina, misitu ya kutosha, vyanzo vya maji vya kutosha kuanzia Bahari, Maziwa Makubwa, Mito Mikubwa, Mabwawa makubwa , Mbuga za wanyama wa kila aina, Uhuru, Wasomi na siasa safi,lakini bado tunalia njaa, tunalia na kusaga meno, tuna majonzi, tuna stress, tuna hofu na umaskini wa kutupwa kabisa.
1. Uhaba wa hospitali na madawa
2. Uhaba wa madawati na vifaa vya kufundishia
3. Kilimo duni
4. Miundombinu hovyo ya barabara ,reli na maji
5. Maji shida tupu
6. Mishahara ya watumishi midogo mno
7. Ukosefu wa viwanda vidogo vidogo na vya kati
8. Makazi hovyo ya raia wake
9. Ukosefu wa ajira
etc etc.
Ni lazima tuwe na viongozi wenye moyo, wazalendo, wakali na wenye chachu ya kuhakikisha keki za taifa kila mtu anafaidi kwa urefu wa kamba yake. Hatuwezi kuwa na viongozi wa kutuchezea hata kidogo. Tumechoka sana!
Viva viva Rais Magufuli.
Endelea hivyo hivyo. Watasema watachoka