Kwa Tukio lililomtokea Mama yangu 2009, Nimetokea kuuheshimu sana Ukristo na Wakristo wote

Mallia

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
437
1,558
Dini yangu mimi Ni Muislam,ila wazazi wangu Baba ni Muislam na mama ni Mkristo , walifahamiana mwaka 1989 kipindi wanafanya kazi serikalini wakapendana na 1992 wakaoana kwa ndoa ya kiserikali na maisha yakaendelea japo malezi yetu Mzee alihakikisha tunaifuata dini yake watoto wote tumebase kwenye Uislam tokea watoto hadi sasa

TUKIO LENYEWE LILIVYOTOKEA 2009

Ilikuwa ni mwezi wa 7 kipindi hicho nakumbuka ndio nilikuwa namaliza Olevel , Mama ndio alikuwa anajifungua mdogo wetu wa mwisho so katika utaratibu wa kujifungua akapangiwa kujifungua kwa (OP), Alijifungua Hospitali kubwa ya Serikali ipo hapo kibaha mbele ya Mailimoja,Baada ya kujifungua kwa Op akawa hospitali kwa siku chache then akaruhusiwa kwenda nyumbani hivyo akaaza kuuguza Kidonda kile

Kidonda baada ya siku kadhaa kikafunga vizuri ila akawa anapata maumivu makali sana sehem ya ndani alipofanyiwa upasuaji yaani kukawa na kitu kama kinamchoma ndani kwa ndani usiku halali analia tu, hivyo kukawa na safari za kurudi pale hospitali kwa uchunguzi, wakawa wanampa dawa tu ila hawakushtukia nini kinamsumbua,

Mwezi wa 9 2009 nakumbuka ilikuwa ni usiku mama akawa analia maumivu makali akawa anapiga kelele usiku hadi majirani walishtuka ikabidi akimbizwe hospitali nyingine ya Private wakampa kitanda na huduma zote za kwanza ili Asubuhi wampige Xray wachunguze sehem aliyofanyiwa upasuaji ndani kuna nini hadi anapata yale maumivu

kulivyokucha akapigwa Xray, wale madokta wanakuja kuisoma ile Xray wakakuta ndani kuna mkasi ulisahaulika, vile vimkasi vya kufanya upasuaji wale majamaa walionfanyia upasuaji kipindi anajifungua waliusahau ndani alafu wakashona na ndio uliokuwa unamchoma ndani kwa ndani, cha kwanza wale madocta pale kwnye ile Hospitali walishtuka sana na wakaogopa kufanya upasuaji kuuondoa ule mkasi wakashauri mzee aende chap pale kwenye ile Hospitali ya Gov kibaha akawape taarifa wale waliomhudumia bi mkubwa walichofikifanya ili waangalie watafanya nn kuokoa maisha yake

Mzee akarudi pale na mama, ikabidi wampige Xray nyingine wahakikishe wakakuta kweli ndanii kuka mkasi mdogo wameusahau so ikabidi ufanyike upasuaji mwingine kuuondoa ule mkasi tena.

Ulivyofanyika upasuaji mwingine balaa ndio kikaanzia hapo mama baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani kile kidonda kikawa hakiponi baada ya mwezi mmoja kikaanza kutoa harufu kali sana yaani ukiingia chumba cha mama utasema kuna kitu kimeoza or mtu kaanza kuoza akiwa mzima mzima hali ilianza kutisha mzee akahangaka hadi alifilisika, Ikafika kipindi ukichungulia lile donda hadi viungo vya ndani unaviona hali likuwa tete.

Wakawa wakiwatafuta wale madokta waliomfanyia upasuaji wanamkimbia inshort walishajua kifuatacho kwa mama ni kifo kila wakipigiwa simu wakawa wanakimbia, Mzee akienda pale hospitali kuomba msaada wanamkwepa, Mama ikafika kipindi tumboni pale akawa anafungwa kibandeji kupunguza harufu kali maana kidonda kilishaoza kikawa kinatoa usaa na uchafu matumaini yakawa yamepotea

Ilipofika mwezi wa 11 Mama akaaza kuacha kitu kama wosia kwa mzee alishajua anaenda kufa, Mama akawa anamwambia mzee kuwa mimi najua naondoka ila naomba uwaangalie sana hawa watoto, uendelee kuwalea vizuri wasiteseke, Mzee akawa anachanganyikiwa zaidi, ilifika kipindi mzee akawa haendi kazini anashinda na mama tu analia, badhi ya watu walishadhani huenda yupo kwenye saa zake za mwisho watu wakawa wanasubiri Taarifa tu maana hata kumsogelea alikuwa anatoa harufu kali

Ilipofika mwezi wa 12 nakumbuka ilikuwa ni Tarehe 20/12/2009.. Hii siku kulikuwa kuna mkutano wa Injili pale viwanja vya Biafra kinondoni kuna mtumishi ambae huwa anafanya semina sehem nyingi Tanzania hii siku ndio alikuwa anasemina na maombezi pale Biafra, kabla ya hii tarehe nakumbuka mama alimwambia mzee ampeleke kipindi hicho mzee akawa kama hataki ila ikabidi anyooshe mikono juu ilipofika hiyo siku ikabidi wamwandae vizuri then tukampeleka

Baada ya semina ndefu ikafuata kipindi cha maombezi, yule Mwalimu akasema namnukuu " naambiwa na roho mtakatifu kuwa yupo mama mmoja katikati yetu anasumbuliwa na kidonda na hakiponi kama yupo apite hapa mbele" akayarudia hayo maneno kama mara 2, Ikabidi mama anyooshe mkono juu maana hata kutembea kupanda jukwaani hakuweza

Ikabidi yule mtumishi amsogelee karibu kisha akamwambia asimame,akaaza kuomba akimshika kichwani, kati kati ya maombezi kwa mshangao lile libandeji alilokuwa amefungwa Mama Tumboni kuzuia harufu lilkakatika pale pale kimiujiza kisha likadondoka chini,maana alikuwa amevaa kitu kama joho skuizi wanayaita madela, baada ya hapo akajihisi mwili mzima kama umepatwa na baridi kali kisha akakaa akawa kama amepoteza faham

Kuja kushtuka akakuta watu wanampepea baada ya hapo yule mtumishi akamwambia mama Imani yako itakuponya Amin, baada ya hapo tukamrudisha Mama nyumbani

Mshangao ukaanza wiki iliyofuata lile Donda pale tumboni likaanza kukauka kimaajabu, ile harufu ikakata kidonda kikaanza kufunga chenyewe kila mtu akawa anashangaa kinachoendelea, ilipofika tarehe 15 mwezi wa 1 mwaka 2010 kile kidonda kilikuwa kimeshafunga kabisa kimaajabu na hakuna mtu ambae aliamini kuwa atapona hadi leo wale madokta walishikwa na mshangao kuwa aliwezaje kupona lakini sisi tunasema ni Mungu tu

Kwa sasa Mama ni mzima wa afya kabisa na yule mtoto aliejifungua now ana afya njema na sasa yupo Form one anapiga kitabu akiwa na Afya Njema kabisa, nafurahia sasa bado naita Mama, Alhamdulilah

Na baadhi ya Ndugu ambao walishaanza kudhani kuwa mama anaenda kufa naowajua kuna baadhi kama 6 tushawazika ila mama leo ana afya tele

Kunazia hapo kwa haya mambo yaliyotokea yalibadili sana maisha yangu na misimamo yangu kuhusu wakristo japo sometime unakuta unamezeshwa sumu mara wale Makafiri, niskiaga mtu anamuita Mkristo kafiri huwa namskitikia sana

Miujiza ya hawa wanaoitwa Makafiri ndio leo inanifanya naita mama, mama yangu kaponyeka kimaajabu

Nikikuta sehem mkristo au kanisa huwa naheshimu sana yaani kitu huwezi kiheshimu hadi yakukute ila kwa hili kila mtu abaki na imani yake ila kila mmoja aheshimu imani ya mwenzie yapo mambo ya kweli kwenye hizi imani mm ni shahidi,

Ukimtukana mtu kafiri unatakiwa ujue kuwa hakuna mwislam aliyekufa akarudi kukupa taarifa kuwa huko peponi wapo watu wa aina gani ukishalijua hilo basi heshimu sana imani za wengine Maisha baada ya kifo ni Siri kubwa na mitihani ya maisha ndio inatufanya tujue ukweli hukusu hzi Dini

Asanteni..
 
Ni meishia kusoma pale nilivo ona kwamba ulipeleke maombini, ni ka kuona kijana mpuuzi, ingekua hivo hata kwenye theater za hospitali kungekua na maombezi tu,........mtoto wakiume anae amini maombezi ya walokole ana vyashilia vya jinsia ya kike.
Aisee bora uache kukashifu watu hayajakukuta matatizo wewe siku yakikupata utatafuta njia zote duniani bila kujali dini,kabila,kipato n.k
 
Ni meishia kusoma pale nilivo ona kwamba ulipeleke maombini, ni ka kuona kijana mpuuzi, ingekua hivo hata kwenye theater za hospitali kungekua na maombezi tu,........mtoto wakiume anae amini maombezi ya walokole ana vyashilia vya jinsia ya kike.
Mimi nafikiri hapa umeteleza chief.
Linapokuja swala la imani, mimi hua najizuwia sana kutoa maneno makali ama kumsemea vibaya anae amini kile ambacho mimi siamini.
 
Ni meishia kusoma pale nilivo ona kwamba ulipeleke maombini, ni ka kuona kijana mpuuzi, ingekua hivo hata kwenye theater za hospitali kungekua na maombezi tu,........mtoto wakiume anae amini maombezi ya walokole ana vyashilia vya jinsia ya kike.
Hapana bro, usiendekeze chuki na ushindani wa kidini kila mahali. Mtu kaleta ushuhuda wa kile ambacho Mungu amemtendea mama yake we unakuja mshambulia. Binafsi nimeona watu wakiombewa na kupona. Sijui ni kujitoa fahamu au makusudi, Yesu alikuwa kwa jinsi ya mwili duniani ila hakuweza kuzunguka kila sehemu kuponya watu Israel yote. Hapa namaanisha nini? Uponyaji upo ila huwezi kuponya watu wote Tanzania au mkoa au eno unapoishi.

Mimi naishi kijijini, tunaona watu wanaenda Mahospitalini kuombea watu na watu wanaponywa huko huko. Bro, toka moyoni mwangu udharau na utukane, Mungu yupo na uponyaji wa Kimungu upo mkuu. Sema sana ila omba yasikukute.
 
Mwambie mama alioza hadi ukicbungulia lile donda unaonda viungo vya ndani acha tu alitisha sana alioza ni Mungu tu
Huyo ni Muislam na mara nyingi ana kashfu Ukristo naye ni kupinga kila kitu. Dunia ni ngumu sana hii na kuna vitu kwa jinsi ya kibinadamu haiwezekani na hadi madokta wanakuambia kama una Mungu muite akusaidie. Nimeshuhudia kwa macho yangu mambo mengi sana Mungu akitenda pitia maombezi. Dunia hii watu wana shida sana kama.wewe u mzima shukuru Mungu na usilete ujuaji.
 
Ni meishia kusoma pale nilivo ona kwamba ulipeleke maombini, ni ka kuona kijana mpuuzi, ingekua hivo hata kwenye theater za hospitali kungekua na maombezi tu,........mtoto wakiume anae amini maombezi ya walokole ana vyashilia vya jinsia ya kike. "Soul diseases are treated spiritually and physical diseases are treated biologically" don't mixup things plz nyie walokole mna kua na wrong absolute belief kitu ambacho ni hatari katika jamii zetu za kiafrica
Huko mahospitalini Mungu pia anatenda kazi kupitia hao madaktari na manesi, ama unazani ni madaktari ndio huponya? Tafakari maneno/fikra zako kabla hujazitoa hadharani kama Ibrahim ni baba wa imani nacc wato tu watoto wake kwanini uchukie imani ya nduguyo? Je hujioni kama wewe ndio unamatatizo?
Tafakari njia zako matatizo yanatabia ya kukupeleka sehem ambazo hujawahi kuzania.
AMANI IWE NAWE.
 
MWAKASEGE
Bado tunao watumishi ambao bwana anawatumia wao kutenda kazi yake na Bwana Mungu wa Majeshi anajivunia wao.
Pamoja na kwamba tunasemwa sana na kujisema wenyewe pia lkn bado ukristo ni sehem salama zaidi
Ni sahihi Ukristo ni sehemu salama na hata sasa wapo ambao hawajapata goti kwa Baali. Wapo wanaotumikia mungunkwa mioyo na dhamira njema kabisa.
 
Hapana bro, usiendekeze chuki na ushindani wa kidini kila mahali. Mtu kaleta ushuhuda wa kile ambacho Mungu amemtendea mama yake we unakuja mshambulia. Binafsi nimeona watu wakiombewa na kupona. Sijui ni kujitoa fahamu au makusudi, Yesu alikuwa kwa jinsi ya mwili duniani ila hakuweza kuzunguka kila sehemu kuponya watu Israel yote. Hapa namaanisha nini? Uponyaji upo ila huwezi kuponya watu wote Tanzania au mkoa au eno unapoishi.

Mimi naishi kijijini, tunaona watu wanaenda Mahospitalini kuombea watu na watu wanaponywa huko huko. Bro, toka moyoni mwangu udharau na utukane, Mungu yupo na uponyaji wa Kimungu upo mkuu. Sema sana ila omba yasikukute.
Maisha haya bro sikia tu kwa watu. Kuna mtu mmoja nilimwomba alikuwa na donda ndugu mguuni. Aiseeee, Muacheni Mungunaitwe Mungu tu. Ni kweli duniani kuna watu wana mateso sana.
 
Back
Top Bottom