Kwa serikali kuwafanyia "Capacity building" ACT pongezi zinastahili.

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Ki msingi ukitizama siasa zetu zilivyokuwa zikienda unaweza kuona wazi kuwa kuwa taifa limejaa wanasiasa au viongozi wa mitaani.

mwanasiasa au kiongozi wa mitaani ni yule mtu anayejilea mwenyewe na siku moja anakurupuka na fikra zake ambazo yawezekana zisiwe na dira ya kusukuma maendeleo ya watu mbele bali kutizama kwa juu juu na kuchukua maana ya juu juu.

mfano ukimchukua mtoto aliyekulia mitaani ambako maisha ni kunyanganyana ukamtuma akauze "ice cream" akikuta mwenzake anauza sana anachowaza ni kuchukua maji machafu pale mwenzake anapotazama pembeni amwage maji machafu kwenye ice cream za mwenzake ili wateja wazichukie na wanunue zake.

Hii inaitwa fitina.

lakini ukimchukua mtoto aliyelelewa katika familia akafundishwa maadili ukamtuma akauze ice cream, akikuta mwenzake anauza sana anachowaza ni jinsi gani anaweza kutengeneza ice cream tamu zaidi ili wateja wavutike kwake.

hii inaitwa ushindani.

ki msingi siasa zetu zimejaa fitina kwa sababu tuna wanasiasa wa mitaani wanaochukulia siasa ni kupingana bila kujua unatakiwa upinga ukiendelea kusukuma maendeleo ya taifa mbele na kwa kuwa fitina hazisukumi maendeleo mbele, fitina ni mwiko katika maendeleo ya taifa.

ACT wazalendo wameonyesha kuwa na misingi ya kujua maana ya siasa kwa pale serikali inapofanya jambo la kuwanufaisha wananchi wanasimama na kuunga mkono na pale wanapoona serikali inafanya jambo la kuwatia hasara wananchi wanasimama na kupinga.

hizi ndizo siasa na si siasa za kueneza chuki kwa wafuasi wako wachukie mwenye itikadi na wewe na hii haina tofauti na fitina za kumwaga maji machafu kwenye ice cream.

Jukumu la serikali kulijenga taifa kimaadili na kiuchumi hivyo kuwapa wapinzani hawa wanaoonekana kufanya siasa safi ni jambo la kupongeza.

Lakini pia yeyote atakayejaribu kutumia chuki, ulaghai, fitina na mengine kama mtaji wake wa siasa huyo apigwe tu.

kama taifa tukiacha mbegu hizi ziendelee kuota kama hazitatutesa sisi zitakuja kuvitesa vizazi vyetu huko mbeleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…