kwa nini uamue kula kuacha kula vyakula vyote vya ngano na juisi, faida yake ni ipi

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,381
3,826
Prof Janabi Aliulizwa swali

“Je kwa nini umeamua kuacha kula vyakula vyote vya ngano na juisi pia Umeacha kula vyakula vingi vya Nafaka”?
.
Alijibu hivi:
1. Kutokana na Nature ya Kazi yangu. Naona wagonjwa wengi wanaoletwa hospital kuzibuliwa mishipa ya moyo imejaa mafuta. Nilipotafiti nimegundua “Wanga ni hatari sana tena hata zaidi ya Mafuta tofauti na fikra za watu kuishi kwa kula wanga wanga wanga bila kuwa na woga na uzito wao.

2. Kutokana na Umri wangu na nature ya kazi yangu. Nadhani alimaanisha kwamba kwa sababu “Physical perfomance yake” Imeshuka kwa sababu ya Umri. Na Pia alimaanisha “Metabolic activities uwezo wa mwili kutumia chakula pia unashuka na umri” Sasa ameamua Kuacha ili kuzuia Ongezeko la kasi la uzito wake.
.
Ila kuna wale wanaofanya kazi Maofisini Chai zao ukiingia Ofisini unaweza Kufumba macho. Makreti ya soda, Juisi, Mikate mabunda na mabunda na Bado akiwa amekodolea kompyuta ana “Chips” Kavu Fried anabugia kimoja baada ya kingine au Popcorn...! Akirudi Nyumbani Yuko Hoi anapitia Chips Kuku “Wanga na Zinekaangwa mafuta mabaya” Mwisho wa siku kilo 140kg na Mapigo ya Moyo Yanaanza Kubadilika na Udhuru kazini Unakusonga..!
.
Nilicho Jifunza kwa Profesa Janabi ni kwamba “Yeye kwanza Ameamua Kuusoma mwili wake na akachanganya na Sayansi ya magonjwa na vyakula, Akapata Mfumo wake sahihi”
.
 
Sasa jamani tutakunywa na kula nini nisaidieni
Vegetables, salads..mboga mboga za majani ,kabechi,lettuce

Protein kama samaki,nyama kidogooo,kuku,maharage

Matunda yotee, bamia, ngongwe,karoti, hoho etc

Wanga ...viazi vitamu,ugali wa dona kidogooooo

Snack...korosho,almond

P.s kula ngano isiyokobolewaa ukiweza acha kabisa..apa utakua na mwili mzuri na magonjwa utayaskia kwa wengine
 
Kukwepa yote angalau kila Siku kabla ya kulala shushia beer glasi kubwa moja.

Itasaidia kurekebisha mifumo mingi ya mwili.
 
Hiyo ni kweli kabisa, wanga ikizidi si nzuri kwa mwili.na alcohol kidogo ni nzuri kwa mmemenyo wa vyakula mwilini.
Shida ni pale pump inapofunguka na mshiko upo..
 
Aliyosema Dr unahitaji change of life style, hii haitokei kwa maajabu, inabidi ushirikishe akili, mwili na mfumo wako wa uchumi.

Unaweza kuanza kwa kupunguza nusu ya vyakula vya wanga unavyokula na kuongeza matunda, mboga, nyama na samaki.

Wengi wetu hatuli wanga kwa kupenda, ni hali ya uchumi. Ni rahisi kula ugali mwingi mboga ikiwa kachumbari ya nyanya moja.
 
Back
Top Bottom