Kwa kauli hizi, Mwigulu amepotoka ajisahihishe

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,863
5,694
Kwa kauli aliyoitoa Mh. Mwigulu kuwa kuuawa Kwa wafuasi Wa CCM sio ugaidi Bali ni mauaji ya kisiasa amepotoka na atasababisha mtafaruku zaidi Kwa maoni yangu.

Hapa atahamisha hisia kuwa kuna mauaji yanafanywa na kundi fulani la watu na kusababisha eidha kundi jingine kulipiza kisasi au kujihami ni jambo baya sana Kwa usalama.

Alipaswa kabla hajatoa taarifa hiyo aeleze wazi wahusika ni akina nani na sio kutoa maoni ya kuhisi wakati kama huu mgumu ambao hatujui nani muhusika na watu wanaangamia.

Kwa nilivyo muelewa Mwigulu anatuaminisha kuwa ugaidi hauwezi Lenga kundi la watu fulani tuu, ni lazima lilenge watu wote ndio tuite ugaidi huo sio mtazamo sahihi.

Magaidi walilipua ubalozi wa Marekani hapa nchini na Kenya Kwa wakati mmoja mbona balozi zingine hazikulipuliwa na tulikubali kuwa hilo lilikuwa tukio la kigaidi?

Ukiacha hilo Bomu lililipuka ktk mkuta wa CHADEMA na kuua watu watatu katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani pale Arusha lakini ktk mikutano mingine iliyofanyika siku ile ile hapakulipuka mabomu mbona hatukuambiwa yalikuwa mauaji ya kisiasa? Na wahusika hawajakamatwa mpaka Leo.

Mimi sipingi kuwa nani anahusika au nani hahusiki, nachoeleza ni kuwa ktk hali tuliyo nayo Kwa sasa tujizuie kuongea sana badala yake tutafute Ukweli kwanza tusije tukaingia mtego mbaya zaidi Wa sisi Kwa sisi halafu tukawaacha maadui wakapita katikati yetu salama.
 
Hii ni kauli iliyowahi kutolewa na aliyewahi kuwa nguri Wa siasa za upinzani Tanzania Dr Slaa,

Nikihusianisha na yanayotokea huko Pwani na kauli ya waziri Wa mambo ya ndani basi Dr slaa hakukosea kabisa

Na kikwete aliposema MCC kumejaa mafisi hakukosea
 
Mkuu umenistua na kichwa cha habari..kumbe unaongelea past. Huyu wa sasa wala hakaribiani na huo mtazamo!
 
Siyo jambo la kushangaa sana majibu mepesi mepesi kutoka viongozi ambayo wapo madarakani kwenye hoja nzito. Namshangaa sana Waziri husika rafiki yangu Mwigulu Nchemba bado ameendelea kung'ang'ania madaraka wakati majukumu ya kazi yamemshinda bado ndugu zetu wanaendelea kupoteza maisha mpaka sasa.
 

Aondoke tu
 
Huyu Dr Slaa wa sasa hana tofauti na Polepole na Kabudi wa sasa.




"Siyo vizuri kuongea wakati wa kula"
 
Kwa kauli aliyoitoa Mh. Mwigulu kuwa kuuawa Kwa wafuasi Wa CCM sio ugaidi Bali ni mauaji ya kisiasa amepotoka na atasababisha mtafaruku zaidi Kwa maoni yangu.


Very shallow thinking, lakini haya mambo yangekuwa rahisi kushughulikia kama hiyo wizara ingeongozwa na mwenye taaluma ya uaskari maana mambo hayo yanahitaji sana kufikiri na kutafiti kwa kina kitaalamu kabisa.

Lakini kwa sasa, kuna uwezekano mkubwa askari wanashindwa kumshauri vilivyo waziri kwasababu ya mashinikizo ya kisiasa badala ya tafiti za kiintelijensia ambazo kama waziri husika angekuwa ni askari basi angeongea lugha moja na hao askari watendaji badala ya mchumi ambaye kwanza anatakiwa apewe exposure ya mbinu za kijeshi ndipo afanye maamuzi

Vilevile waziri anatakiwa kuwasikiliza zaidi wataalamu badala ya kusimamia msimamo wake, vinginevyo itafika watamwacha aboronge ili ajitumbue mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…