Kwa kauli hii ya Waziri, kuna moto unafukuta Diamond Vs Serikali (Hakuna Msanii Mkubwa Kuliko Nchi)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,661
6,395
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amewataka viongozi wa BASATA na COSOTA kuhakikisha wasanii wote wanasajiliwa hususani wale wakubwa ambao mpaka sasa hawajasajiliwa kwani hakuna msanii mkubwa kuliko Nchi.

"Nitoe maelekezo kwa COSOTA na BASATA hatutegemei kusikia wasanii wamesajiliwa wachache, sitegemei kusikia msanii mkubwa hajasajiliwa, tutaanza kuhoji uwezo wa tuliowapa dhamana.

"Jukumu letu sisi serikali ni kuwaunganisha wasanii wote, hakuna msanii mkubwa kuliko nchi, situliopewa mamlaka twende tuwanyenyekee, wanatoa mchango kwa nchi inanufaika na kupitia kodi.

"Tusijifungie maofisini, twende tukawatafute, kwenye nafasi tuweke watu wenye fani ya sanaa, wasanii wakongwe wapo wanaijua sanaa, tuwateue kwenye nafasi mbalimbali hasa za BASATA ili wakasimamie biashara zao, wakasimamie kutafuta wateja, kuangalia walanguzi na haki zao za msingi.

"Mnaponiletea mapendekezo kwenye mabodi, nileteeni majina ya wasanii, kwa mfano Kenya wanaosimamia ni wasanii wenyewe akina Juakali, na sisi tufanye hivyo ili wakalinde haki zao wenyewe ili kuiendeleza tasnia, hawatakubali sanaa ianguke kwani watakuwa wameanguka wao," amesema Mchengerwa.

Chanzo: TanzaniaWeb

========

UCHAMBUZI


Kauli hiyo ya Waziri inakuja ikiwa ni siku chache yangu Diamond Platnumz na wasani wake wote wa lebo ya WCB kutojisajili katika Tuzo zinazosimamiwa na BASATA, pia ni aliziponda tuzo hizo kwa kusema ‘Kama mirabaha hamtupi mtatupa hizo tuzo’.

Mbali na hapo ni siku chache zimepita tangu Diamond alipozungumza kwa nia ya kukosea kuwa kila anaposafiri nje ya nchi hawezi kuruhusiwa hadi alipe Sh 50,000, ambapo alidai kuwa hajui kama hiyo ni kwa wasanii wote au ni yeye pekee ndiye anayefanyiwa hivyo.

Kwa mwenendo huo ni wazi upepo siyo mzuri baina ya taasisi hizo za Serikali na msanii huyo au lebo yake anayoiongoza.

 
mbona Ukraine mchekeshaji amekua kiongozi wa nchi?
US pia ilikua na raisi ambaye alikua mcheza sinema?
Arnold schwarzennegar ambaye ni mcheza sinema ila alikuja kua Gavana wa jimbo la California?
Wasanii wa nchi za dunia ya kwanza huwezi linganisha na hawa wakina Steve Nyerere au Masanja Mkandamizaji.

Kule shule ipo na kichwani wapo vizuri vile vile.

Huku msanii kakulia kwenye kula ugali kila siku usitegemee kamwe awe vizuri kwenye lolote.
 
Mpaka leo hua sielewi tafsiri rasmi ya neno "SERIKALI" Hivi kweli ni sisi watu(Wananchi wote) au ni kikundi fulani cha watu wenye nguvu.. Naona limezoeleka kutumika tofauti nje na tulivyofundiswa.. Nimeshangaa hapo kwenye "Diamond VS Serikali" Nisaidieni wakuu
 
Mchengerwa anafurahisha genge.

Kilq Waziri anakuja na matamko. Hakuna mikakati wala utekelezaji.

Wasanii tuna maoni mengi mazuri wameyafutika kwenye shajara, lakini utasikia kila siku LETENI KERO ZENU.

Wasitufanyie hadaa
Nyiiie mbuzi ndio mliochangia taifa kufika hapa mkinengue baada ya kupewa kofia za kijani ...

Msitupigie kelele mbwa nyieee
 
Mbona Ukraine mchekeshaji amekua kiongozi wa nchi?

US pia ilikua na raisi ambaye alikua mcheza sinema?

Arnold Schwarzeneeger ambaye ni mcheza sinema ila alikuja kua Gavana wa jimbo la California?
Hao wote uliowataja walipita kwa BALLOT PAPER na wakakubalika na waliowapigia kura.

STEVE hajapigiwa kura na hao anaowaongoza Hawamtaki, mbona unachanganya Mambo.

Mifano uliyoitoa haifanani
 
Katiba ya shirikisho la madaktari inasemaje kuhusu hilo?
katiba yao siijui maana mimi sio daktari Ila tamaduni ya muundo wa mashirikisho ipo wazi,

kiufupi shirikisho ni kikundi cha watu kinachotetea maslahi yao binafsi na members wao huwa na kada au maslahi yanayofanana.. Honorary members pia wapo ambao huteuliwa kwa kuangalia utaalamu au mchango wao kwa shirikisho kama Tz Tu ilivyopewa special seat SADC hata kama haikukidhi vigezo gya kijiografia

Kwa hiyo ni ngumu kukuta daktari apewe membership ya Shirikisho la wanasheria maana yeye kutokuwa mwanasheria tayari anakosa kigezo cha kuwa member hivyo atawezaje kugombea uongozi
 
Back
Top Bottom