Kwa huu upuuzi hivi nikipiga nitashitakiwa?

Apo solution ni mchepuko tu, hakika michepuko inajua kuliwaza. We tafuta mchepuko unakua ukitoka kazini unaanzia kwa mchepuko unakaaa hadi usiku ukirudi home unakua huna stress kabisa. Narudia tena mchepuko ndo solution.
 
There you are. Na kama umeelewa post yangu, shida imeanzia kwa mke, ambaye asubuhi anakomalia kumwamsha msichana badala ya yeye kuamka, au waamke wote. Nimegombana naye kuhusu hilo lakini somo halieleweki. Yeye anaona msichana anategea kazi na msichana anaona mama hajishughulishi. Mimi nikimgombeza mke, yeye anaona namtetea msichana. Nguo zangu za kuvaa asubuhi sasa hivi nazinyoosha mwenyewe, maji ya kuoga nimetangaza waache ntaoga ya baridi, bombani bafuni, kama ni Nemonia wacha nipambane nayo. Maana nanunua mkaa, kuni na gesi lakini bado unaweza ukaamka maji hayajaandaliwa.
Pole sana lakini badilisha mbinu za kupambana na tatizo lako.
 
Kama kuongea kwa ukali bado hakujasaidia kabla hujaanza mabaya zaidi, tumia upendo. Hata kama una hasira usiioneshe bali muoneshe mkeo upendo wa hali ya juu sana. Ukirudi mpetpet, na hasa ule upendo mlioanza nao. Fanya hivyo kwa Muda wa wiki mbili hivi. Asipobadilika ukikaa kimya bila kumsemesha atabadilika tu. Njia hiyo ndo imenisaidia mimi.
 
Wewe hujaitambua nafasi yako ya Kichwa cha nyumba.Unataka sympath kutoka kwa mkeo na wakati yeye anahitaji umwongoze.Wewe ni mtu dhaifu unahitaji uwe strong.La sivyo mkeo atakuletea mazingaombwe mengi usioyatazamia.
Mzee alishawahi kuniambia, usipokua ngangali mke atakushinda. Komaa, onyesha misimamo na uwe unamaanisha kweli unaposema kitu fulani. Kama vipi yeye ndio akuache wewe tena kwa mbinde sio kirahisi rahisi.
 
Hio kazi rahisi sana.. Kama mkeo hataki kufanya majukumu yake.. Mchukue huyo HG mtwange selfie... Wife atanyooka mwenyewe
 
Kwangu naona usimlaumu msichana wa kazi maana majanga yote anayofanya chanzo kikuu ni huyo mkeo, sikushauri uachane nae bali inakubidi utafute suluhisho la matatizo katika ndoa yako maana naelewa ndoa za kikristo jinsi zilivyo.

Naoma uanze kudeal na housegirl umtimue, kama uliweza kuwatoa wale wafanyakazi wa ndani ambao ni ndugu zako utashindwaje kwa huyu na wakati mwenye mamlaka hapo nyumbani ni wewe?
Mwache kwa mda bila mfanyakazi yeyote ili umchunguze vizuri na ulione tatizo liko wapi.

Baada ya hapo shirikisha watu waliohusika na ndoa yako katika ushauri na jinsi ya kurebisha matatizo katika ndoa yako ili isiingie 'doa'.

Kuwa na maamuzi kama baba wa familia na sio uruhusu mwanamke akuongoze wewe katika maamuzi.
 
Hizi ndoa hizi mnatupa wakati mgumu sana kuamua tuoe au tuache
Mkuu oa ila ukileta mapenzi ya kwenye tamthilia, lazima ndoa ikushinde. Unaweza kua binti mwenye tabia nzuri tu lakini wewe mume ukamuharibu tabia kwa kuendekeza kumdekeza kama mtoto mdogo.
 
Suluhisho hapo ni kucheza na akili za mkeo. Kwanza kula papuchi ya housegirl na fanya makusudi ikiwezekana na mkeo ajue. Then punguza mawasiliano na mkeo yaani fanya kama humuoni hapo home. Am telling you haitachukua hata week huyo mama atarudi kuwa mkeo mtiifu..
 
Ile misemo mizuri na mitamu kama asali kuhusu ndoa kwangu ni kama hadithi fulani hivi. Wakati naingia kwenye mahusiano ya ndoa nilikuwa very optimistic, sasa hivi nimenywea, sina hamu tena.

Mwaka 2007, mke wangu alikuwa mjamzito kwa mtoto wa kwanza, na wakati huo nikapata kazi ya kuajiriwa mkoa wa mbali na nyumbani. By then hatukuwa na msichana wa kazi. Nikaona kwa situation ile, itabidi tuu niwe na msichana wa kazi. Tuliposhauriana mwenzangu akaniambia nimtafute mimi kama nitampata kwetu. Nilimkosa, ila kulikuwa na mtoto wa kaka hakubahatika kwenda sekondari, kaka akaniambia nimchukue tu kama namhitaji kwa malengo kuwa hapo baadaye nimtafutie hata ufundi veta au shule ili ajiendeleze. sikuona ni tatizo.

Nilipomchukua, ikawa yule binti anakorofoshana na mke wangu. Mke wangu akawa anakuja kumshitaki, huku analia sana. Nilipoona issue itakuja kunivunjia ndoa nikamrudisha yule binti nyumbani ili nimsaidie shule huko huko nyumbani. Nikamwambia mke wangu sasa na yeye amtafute wa huko kwao, ikashindikana. Nilipofika nyumbani, mara dada yangu akaning'ang'ania nimchukue binti yake. Nikamwuliza wife akasema bora nije naye tuu maana hakuna namna. Nilimchukua huku rohoni sina amani. Tulikaa hata mwaka haukuisha mambo yakawa yale yale. Nikamrudisha tena. Nikagoma kumtafuta mwingine, nikamwambia mke wangu kama hataki kumtafuta basi tuache.

Akampata wa huko kwao ndo akamleta. Sasa huyu binti ni mkorofi afadhali hata wale wa ndugu zangu, ila mke hataki kumwondoa, anasema atapambana naye. Nikiona mapungufu au uzembe wowote pale nyumbani, nikimwambia mke wangu anasema yeye hahusiki nimwulize binti.Yanai yeye anaona mimi ndo niwe namuamrisha binti wa kazi, badala ya yeye. Nimegombeza mpaka nimechoka wakati mwingine napata hasira za kushusha mkong'oto. Mathalan, inakuwaje binti wa kazi anaamka saa 12 na nusu wakati mimi saa moja kamili natakiwa kuripoti kazini? Maandalizi ya watoto kwenda shule na kupasha maji ya kuoga yatafanyika saa ngapi? Kila siku ugomvi na dereva anayewapeleka watoto shule kwa sababu ya uzembe. House girl anachelewa kuamka na mke naye anachelewa kuamka, wote wanaviziana nani atangulie. Kazini kwangu siyo mbali na nyumbani kiasi kwamba lunch naenda nyumbani mara nyingi, lakini inakuwaje chakula cha mchana hakijawa tayari mpaka saa tisa mchana? Nikila huko kazini kwenye restaurant hataki, anasema hizo hela unazoteketeza huko si tuboreshe hapa nyumbani, lakini naenda nyumbani alafu narudi sijala? Siku zingine nakuwepo nyumbani mpaka saa mbili asubuhi au saa tatu lakini hata chai haiandaliwi, naondoka empty stomach, wakati mahitaji yote yapo nyumbani. Nikimwuliza mke wangu anasema numwulize housegirl. Siku nyingine nanunua matunda mengi ndani lakini hata yanaweza kuozeana ndani, chakula kikipangwa, nisipouliza matunda hayawekwi, ila baada ya siku mbili utakuta ndizi zimeozeana ndani, parachichi zimeshakuwa rojo, wakati siku mbili zimepita matunda hayajaliwa ndani.

Kuna kipindi nilimnunulia simu kama motisha tuu afaye kazi kwa bidii, kumbe ndo ikawa nimemrahisishia ufuska wake, akawa anawachanganya wanaume. Siku moja nikazipata stori mtaani, nikaja kuifuma simu yake, anadate na wanaume kama wanne hivi. Nikataka nimtimue, mke wangu anamkingia kifua. Nikasema ataondoka, yeye anasema haondoki. Anyway, nina mengi moyoni, mengine hata nashindwa kuandika hapa. Natamani tu niwe nachelewa kurudi nyumbani nikifika nikute wamelala.
What can i do jamani haya maisha gani? Hivi nikipiga si nitashtakiwa.


Tatizo ni kwamba wee unalia lia hovyo kama Mwanamke na ndiyo maana mke wako hakuhushimu, hauwezi kutatua matatizo, hilo dhaifu kubwa sana!
Mwanamke siku zote huwa anamjaribu Mwanamume kwenye mambo mbalimbali na ndiyo maana hata umasaini kabla ya kuoa inabidi uue Simba kwanza sababu ni kujaribu ukidume wako kama wewe ungeshaua Simba sidhani kama ungekuja humu unalalamika kama mwanamke, na hii ndiyo sababu ya mke wako kufanya anayofanya kwa kifupi ameshakudharau na ninakuhakikishia ataanza kumbea nje kwani mwanamke anajitaji mwanaume strong na siyo kama wewe, wewe ni dhaifu kwa hali ya kawaida haukupaswa hata kuoa, nina uhakika utarudi tena ukilalamika hapa kwamba mke wako anapigwa bolo nje, kuomba ushauri!
 
hii inaitwa "married to two women". nimecheka sana ati unasema ikitokea mistake unatakiwa umuulize huyo clichy, na wewe ulivyo kiazi unaendelea kuentertain ujinga wa mkeo....kabla ya yote inabidi ujue kuwa jipu ni wewe mwenyewe na unabidi utumbuliwe...nashindwa kuelewa ati mke analala mpaka sa mbili halafu unamlaumu clichy au huwa mnalala vyumba tofauti na mkeo
 
Kaka unaonekana huna upendo kwa mkeo. Kinacho tokea huyo dada ndio anachukua nafasi yako kwa mkeo. Na inaonekana yule msichana wa kwanza ulikua unampa nafasi sana ndio maana mkeo akamchukia. Dawa hapo jaribu kumpenda huyo dada wa kazi uone moto wake kama hata ondoka hata baada ya siku moja. Usitake tuu kufanyiwa mambo bila kuwekeza kwenyw upendo.
 
kama unayosema ni kweli mkuu UNAMWANAMKE MPUMBAVU NA YUPO TAYARI KUBOMOA NYUMBA YAKE........

yafuatayo fuatilia:
house girl anajua madudu ya mkeo labda anachepuka na mchepuko hg anamjua.. may be wanenda wote kwenye mamabo mabaya sasa hapo lazima wife amkingie kifua
mkeo ni hajitambui wala ajielewi ..
mkeo anamchepuko anao uheshimu wewe ni spare tu.....
kaa na mkeo mueleze kinaga ubaga na matokeo ya hayo anayofanya ikishinidkana kaa kimya kula ofisini kunywa chai ofisini...
usimpige kama unandugu unao waamini jaribu kuwaeleza aongee na mkeo...
house girl anawavuruga ay be kishirikina ..
 
Pole sana ndugu yangu, kuna msemo kuwa kuishi na mwanamke ni Sanaa, yaani haihitaji kuwa professional saaana ndio uishi nae bali uwe msanii wa namna flani hivi ndio utamudu, Ishu ya Housegirl ni kizungmkuti maana hata mimi nimeshapitia/napitia almost the same situation, tuliwahi kuwa na HG mbaya kweli yaani alituchonganisha hadi ndoa ikayumba sana (usione tunacheka tuna mengi mioyoni) cha kushangaza alimkingia kifua hadi basi, sasa anataka kumrudisha na mimi sitaki arudi lakini nikaona nisigombane na mke wangu, nasubiri amlete kasha nifanye juu chini nimtafune hata kiuongo uongo tu hali najenga mazingira ya yeye kujua kuwa nimemtafuna HG wake. usihangaike na HG na Mke wako play your part, kuna mahali kwenye bible kuna maneno yanasema hivi, ni
17Kisha akamwambia huyo mwanamume,

“Kwa kuwa wewe umemsikiliza mkeo,

ukala matunda ya mti ambayo nilikuamuru usile;

kwa hiyo, kwa kosa lako ardhi imelaaniwa.

Kwa jasho utajipatia humo riziki yako,

siku zote za maisha yako.

MAANA YANGU NI KWAMBA SIO KILA KITU NI CHA KUMSIKILIZA MKEO
 
Baba umelegea ndio maana wanakuchukulia oya oya kua tough aisee

Siku moja onyesha action hapo tafuna masufuria kadhaa mwaga vijiko vyote chooni vunja vunja meza tv na viti halafu ondoka na watoto week ukirudi wamenyooka
asisahahu kuvunja na yale mayai mkewe anayoatamia
 
Man up . .
Wanakuchukulia poa,
Badili mfumo wa hapo nyumbani kuanzia na wife wako

Vitu unavyoleta havitumiki mpaka vinaharibika, stop providing labda hawaviitaji

Husipende kuongea sana, wanakudharau zaidi ndo wanawake tulivyo. . Amka asubuh jiandalie Maj, ikiwezekana pika chai yako, nyoosha nguo zako, nenda kazini. . Mchana husirudi kula, ukitoka kazini, ukirudi spend time na watoto wako, lala
yes yes yes akifanya hivi lazima akili imkae sawa mwanamke.. ataanza umepata mchepuko mfyuuuu
 
na ww bwege tu ! ukila mgahawani mpaka umwambie mke wako? ungekuwa karibu ningekuzaba vibao !
 
Back
Top Bottom