Kwa anaejua hili anisaidie (injini za Magari za Kichina)

itagata

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
210
71
Nimekua natumia gari aina ya Pajero kwa Muda sasa na imejitokeza likapata matatizo ya Injini yake (4D56), nimejaribu kununua injini zimefika 3 mpaka sasa lakini zote zinasumbua baada ya miezi miwili au mitatu toka kuzifunga. Imefika kipindi sasa nimekata tamaa nafikiria kuweka injini aina nyingne tu, lakn kuna mdau mmoja kaniambia kuwa kuna injini kama hizo (4D56) za kichina zinakuwa mpya kabisa zinauzwa kwa bei ya chini ambazo naamini naweza kudumu nayo hata kwa miaka 3 hivi. Hivyo basi naomba kama mtu anataarifa sehemu zinakopatikana hizo injini anijuze ili nifanye mchakato wa kuzitafuta. Asanteni.
 
Badilisha fundi wako na mtiririko wake, Tafuta fundi mwingine, hata hapa JF unaweza kupata mafundi wazuri, taja Mkoa/ Wilaya ulipo.

Sijui umenielewa?
 
Nashukuru kwa ushauri kwa sasa nipo Singida
 
Kiukweli pajero ikishaanza kusumbua haitengenezeki ila ukiweka used ya japan inadumu ila kiujumla huku kwetu zinasumbua
 
Sasa dawa yake ni nini? Maana sasa injini hii ni ya 3 sasa na inasumbua pia
 
Mbona 4D56 ni injini ngumu sana kuharibika?, ulinunua used pale ilala/Shaurimoyo?, inakupasa uende na Fundi ili akukagulie injini nzuri
 
Ni kweli ni injin ngumu, lakn sijui nina bahati mbaya maana zinanisumbua sana kaka, ya kwanza iliyokuja na gari ndio imedumu sana lakn hizi za kununua zinanisumbua sana.
 
Nenda na fundi, fundi kweli kweli akukagulie kabla ya kuinunua.
 
Ni kweli ni injin ngumu, lakn sijui nina bahati mbaya maana zinanisumbua sana kaka, ya kwanza iliyokuja na gari ndio imedumu sana lakn hizi za kununua zinanisumbua sana.
Kwa nini hukuifanyia overall hiyo ya kwanza?, mablock yote unayo?, unaweza kuirebuild na ukapata engine ya kukusukuma hata miaka matatu minne

Hizo ulizozipata zina shida gani?, locker shaft?
 
Ya kwanza block nzima, ya pili rocker shaft inajam mpaka inakata timing belt, hii ya 3 ndio ina mlio kama vyuma vinatafunana ndani
 
Pole sana kaka, mimi nina Picup L200, Double cabin, niliinunua 2005, engine ilikuja kunizingua 2010, ilikuwa imekata Locker shaft, nikaifanyia marekibisho, na ikawa inadunda, lakini 2011 nilipata visenti nikanunua engine nyingine used Ilala, ilikuwa ya Basi tena auto lakini niakipachika kwenye pickup yangu manual na inafanya kazi mpaka sasa vizuri

Pamoja na hayo mambo ya engine naona pia una shida ya mafundi wazuri, kusema ukweli hiyo gari huwa naiita punda, ni engine ngumu mno, hazitumii mafuta sana, zinahimili hali zot
 
utanunua engine kutoka mpaka mbinguni mkuu.badilika hapo hapo ulipofikia?? why hizo engine zote ziwe majanga??

hapo kuna mambo unakosea au huwa unaenda kutaka vya kunyonga?? vyakuchinja huwezi??
 
Hahaaaaaa! Vya kunyonga ndio vipi kaka?
 
Jamani bado sijapata msaada niliouomba, naombeni tena kwa anaejua hii kitu anisaidie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…