Sooth
JF-Expert Member
- Apr 27, 2009
- 3,922
- 5,619
Leo nitakuwa nje ya mada. Ndugu Pasco nikusahihishe japo wewe ni mwandishi mkongwe. Ni makosa kuweka alama ya mshangao(!) pamoja na kituo (.) mwishoni mwa sentensi moja. Weka alama ya mshangao tu, halafu anza sentensi inayofuata kwa herufi kubwa. Pia hakuna haja ya kituo unapomalizia sentensi yako kwa alama ya mshangao.
Mfano:
Sahihi: Nani kasema Magufuli dikteta? Magufuli ni rais poa sana! Ni mtu wa watu.
Isiyo sahihi: Nani kasema Magufuli dikteta?. Magufuli ni rais poa sana!. Ni mtu wa watu.
Mfano:
Sahihi: Nani kasema Magufuli dikteta? Magufuli ni rais poa sana! Ni mtu wa watu.
Isiyo sahihi: Nani kasema Magufuli dikteta?. Magufuli ni rais poa sana!. Ni mtu wa watu.