Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,385
- 38,657
Alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, John Pombe Magufuli alitamani kila mradi uitwe kwa jina la Julius Kambarage Nyerere. Ni kama vile aliamini kuwa hakuna aliye bora kati ya Marais watatu wengine waliomtangulia, yaani Ally Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa au Jakaya Mrisho Kikwete.
Hakuna anayebisha kwamba Magufuli alipokuwa Rais wetu, kuna mambo aliyafanya kwa ufanisi na lakini pia isibishiwe kuwa kuna uhalifu pia alifanya. Magufuli alikuwa ni fundi wa kuzuga (Manipulate) akili za baadhi ya watu kiasi kwamba hao watu mpaka sasa wanaamini ni yeye tu aliyekuwa Rais bora kuliko wenziwe wote waliomtangulia.
Nimeona tatizo ni kwamba kwa Mujibu wa takwimu za Sensa za mwaka 2022, wanzania walio chini ya miaka 35 ni sawa na 75%. Kwa maana nyingine wengi wa watu waliopo sasa ni wale waliozaliwa kuanzia mwaka 1987 kuja 2022 wakati sensa inafanyika.
Kwa tafsiri ya Takwimu hizo (HIvi ile sheria ya takwimu ya zama za Magufuli bado iko?) ni kwamba wakati Kikwete anatoka mdarakani mwaka 2015 wengi wa waliozaliwa mwaka 1987 walikuwa wana miaka 28 kushuka chini. Au kwa maana nyingine wao ndiyo walikuwa wapiga kura wa mara ya kwanza mwaka 2005 wakati kikwete anagombea Urais.
Kundi hili kubwa la watanzania (75%) halijawahi kushuhudia Wakati Nyerere, Mwinyi, ama Mkapa wakiwa madarakani. Hawa ndiyo kina johnthebaptist huwafanya mateka kwa kuwaambia kwamba watangulizi wa Magufuli hakuna walichowafanyia watanzania zaidi ya kufilisi nchi.
Kwa kuwa historia imekusudiwa kupotoshwa na kina Countrywide Stroke na wenzao, nchi inakuwa imekwama kwenye kubishana kama Magufuli alikuwa bora kulliko wenziwe na hatatokea tena mwingine kama yeye ama alikuwa sawa tu na wenziwe.
Kutokutunzwa kwa kumbukumbu za nchi yetu, kunasababisha wapiga porojo wa Lumumba ambao walikuwa waimba pambio enzi za Magufuli ambao sasa wamejigeuza kuwa chawa wa Samia Suluhu Hassan, kusema uongo bila ya hofu ya kuumbuliwa.