Kutoka TAZARA: Ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) wazinduliwa rasmi

July 4 mwaka huu Marekani itafikisha miaka 240 ya uhuru, yote tunayoyaona kwenye runinga ambayo yanatuonyesha maisha ya taifa hilo kubwa ulimwenguni, ni kazi ya miaka mingi sana. Tanzania ina miaka 55 ya uhuru, lakini wapo waungwana wanaotaka kuiona nchi hii ikifanana na Marekani ya leo hii!. Wakati Tanzania itakapokuwa inatimiza miaka 240 ya uhuru, nina uhakika hakutakuwa
na mtu ambaye huwakilisha mawazo yake humu jamiiforum ambaye atakuwa bado anaishi.

Lakini hizi flyover zinazojengwa leo ndizo zitakazokuwa ushahidi wa ukubwa wa Taifa letu kwa wakati huo. Tulio hai leo hii tunapata bahati ya kuwa mashahidi wa ujenzi wa nchi itakayokuwa kubwa miaka mingi ijayo.
Huwa ninawashangaa sana wanaopinga miradi mikubwa kwa kisingizio cha fedha nyingi,
ni kweli miradi mikubwa huvutia ufisadi mkubwa, lakini ikisimamiwa vizuri pasipo harufu ya ufisadi, hii miradi mikubwa ni muhimu kwa sababu ukubwa wa Tanzania utakuja kutazamwa siku zijazo na sio leo.

Ni ubinafsi wa hali ya juu kudhani kwamba tunajenga nchi kwa faida ya kizazi cha leo na kesho pekee. Ni ukosefu wa ubinafsi na ni kielelezo cha upendo ikiwa tutatambua kwamba kinachojengwa leo, kitakuja kuwa na faida kwa Tanzania ya miaka mingi sana ijayo.
Safi sana
uliyo yatamka yana ukweli waote
 
Ninapata tabu kidogo kuelewa hili jambo. Kwa miaka 5 hotuba nyingi za JK zilihusu Tazara na ubungo ''flyover''

Ujenzi ulishaanza kama sikosei na kampuni moja ya ulaya. Leo tena kuna uzinduzi sijaelewa hasa nini kinaendelea. Naomba msaada, ina maana miaka 5 iliyopita ilikuwa hadithi tu au lipo nisilolielewa?
Hivi kwa fikra zako, mradi mkubwa kama huu (kwa viwango vyetu) ufanyiwe upembuzi miezi minne? uchorwe miezi minne hiyo hiyo? Ufanyiwe engineering miezi minne hiyo hiyo? Utafutiwe pesa za ndani miezi minne hiyo hiyo? Utafutiwe pesa za nje miezi minne hiyo hiyo? Utafutiwe mkandarasi miezi minne hiyo hiyo? Na, na, na... Miezi minne hiyo hiyo?

Ukipata jibu utaelewa kwanini ahsante Kikwete.
 
Tanzanians (tanzanites) will never stop (or avoid) daydreaming! We've a comedian president who proud of kutumbua majipu pele!
 
Foleni haitokwisha kabisa pale Tazara maana mchoro uko simple sana umewarahisishia waendao na kutoka airport tu lakini wanaotumia mandela road na kulazimika kukunja kushoto au kulia walazimika kusubiriana na wanaonyoosha moja kwa moja.
 
...... binafsi nimeipenda lakini ingepeneza zaidi kama wangeweka njia nyingine nne moja inatoka airport kwenda mandela rd ya pili inatoka mandela rd kwenda city center ya tatu inatoka city center kwenda buguruni na ya nne inatoka buguruni kwenda airport na wandeondoa taa za kuongoza magari hapo ingepengeza kupita maelezo na naama ya flyover ingeleta jibu sahihi.....
 
Foleni haitokwisha kabisa pale Tazara maana mchoro uko simple sana umewarahisishia waendao na kutoka airport tu lakini wanaotumia mandela road na kulazimika kukunja kushoto au kulia walazimika kusubiriana na wanaonyoosha moja kwa moja.
Foleni haitokwisha kabisa pale Tazara maana mchoro uko simple sana umewarahisishia waendao na kutoka airport tu lakini wanaotumia mandela road na kulazimika kukunja kushoto au kulia walazimika kusubiriana na wanaonyoosha moja kwa moja.

Umesema sahihi sana. Ni hatua nzuri lakini haitatatua tatizo kwa kiwango ambacho wengi tulitarajia. Kama ulivyosema, hii imerahisisha kwa wale watokao mjini kwenda airport na kutoka airport kwenda mjini. Wengine wote wataendelea na tatizo la foleni kama zamani.

Kwaajili ya kupunguza msongamano ilistahili lazima kuwepo kwa miduara pale katikati ili kuyawezesha magari yawe na uwezo wa kupanda na kushuka. Ukweli ni kuwa kuna hatua imepigwa japo kiuhalisia zinahitajika angalao flyovers 6 kwa jiji la Dar es Salaam kuweza kupunguza msongamano.
 
Back
Top Bottom