Habarini wakuu!!
Niko dilema kidogo wakuu juu ya hii ajira iliyopo mbele yangu.
Nilikuwa nafanya kazi ktk ofisi moja ya mama wa kihindi ikiwa kama ni kampuni ya familia
Nilifanya kwa muda wa mwezi mmoja bila maelewano yoyote ya mshahara, baada ya mwezi mmoja kuisha alinipa laki moja nilipokea kishingo upande
Niliendelea na kazi baada ya siku kadhaa nilimuuliza kuhusu makubaliano ya mshahara akasema atanipa 150,000, kiukweri nilishindwa kukubaliana nae nikasepa.
Baada ya miaka miwili kuachana nae mwez wa nne kantafuta na kuniambia ananiitaji ofisini nikaenda tukaongea akanipa offer yake ambayo ni 200000 na ku ahidi kuongeza ndani ya miez mitatu
Tatizo lina kuja ni hayo mazingira ya ofisi mambo yanayofanyika humo dah nakosa amani na sina raha kabisa nikiyafikiria matukio hapo nyuma ndani ya mwezi ule niliofanya yananipa wakat mgumu kwenda kuanza iyo kazi. Mambo yenyewe ni
Wanachoma hudi kilasiku
Kulishana vyakula vya ajabu
Mara mtalazimishwa mle nazi as refresher khaa, najiuliza sana vitu kama nazi ofisini inakuwaje
Sometime kutukanwa mbele ya staff wote.
Kufanya kazi siku sita za week kwa pesa madafu.
Na kilicho nichoshaga siku moja niliingia ofsini boss akaja na yy alivokuwa anaingia ndani akaanza kufanya kitendo cha kuesabu esabu ktk ngazi kwa muda kama wa dk tano kama mtu anae chora kitu chini na ukizingatia ni mjini kabisa tena bila uoga, nilichoka
Pia kuna siku member wa familia mmoja ni mdada ni sehemu ya staff akaenda mbele ya mlango na kuanza kufanya kitendo kama cha kutengeneza nywele zake lakin niligundua kuna vitu alikuwa anapaka ktk masikio na ktk nywele zake, nisiwachoshe matukio ni mengi
Nisaidie wadau mm nimechoka kabisa na nashindwa kwenda kuanza hiki kibarua cha huyu mama wa kihindi,,,nijuzeni ni sehemu ya tamaduni zao au ndo ushirikina, sitoweza enjoy na hii kazi kwa mwendo huo. Nipeni mawazo yenu niweze kwenda hatua nyingine, ushauli wenu utanipa mwongozo wa kuamua kwenda kupiga kazi au nimpotezee. poleni kwa kuwachosha kwa urefu wa hii habari
Thanks.