figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,484
Habari wakuu,
Rais Magufuli yupo Kurasini Dar Es Salaam kwenye Hafla ya kuwatunuku vyeo wahitimu waliofanya vizuri zaidi Mafunzi ya Uofisa na Uongozi.
Ntawaletea kila kitakachojiri.
======
UPDATES
1127HRS
= Sasa hivi zinaendelea nyimbo za kumsifia rais na kuisifia nchi. Band ya Polisi Moshi ndo inaimba.
1149HRS
Mkuu wa chuo Anton Ruta ndo anaongea sasa
Baada ya itifaki kuzingatiwa anasema;
Nawashukuru wote mliofika na wote waliokubali mualiko wetu.
Mafunzo yamefanyika kwa muda wa miezi 6. Wanafunzi 313 Wakaguzi. 363 ni Maofisa. Wanafunzi wane walifariki.
Walijifunza Haki za binadamu, Sheria na maswala mtambuka.
Wamepata mbinu mbalimbali za kivita huko kilelepori moshi kwa wiki sita.
Chuo hiki kutoa mafunzo ya diproma ya polisi Sayansi ya Sheria.
Hapa chuo tuna changamoto ya Mabweni pamoja na Madara. Tukipata mil 750 tutamaliza hili Tatizo.
UFAULU WA WANAFUNZI
Wanafunzi wamefaulu wote
1157HRS
Simon Sirro anasema;
Itifaki imezingatiwa.
Nawashukuru wote kwa kuja kuungana na sisi.
Nakishukuru rais kwa mambo uliyofanyia polisi. Ujenzi wa makazi ya Serikali. Ukiahidi kitupa Bil 10 mpaka sasa tumepokea Bil 3 na tumejenga nyumba 148. Bado nyumba 400.
Tunashukuru kwa kitupa bil 1 kwa ujenzi wa majengo Mwanza na Msoma.
Tunashukru kwa magari zaidi ya 400.
Bil 50.3 za wazabuni tumezipata na kuwalipa.
Umeboresha masilahi ya Maaskari.
Umepandisha vyeo 3086 na hawa wa leo. Zahati zina upungufu, ndege zetu wengi wamestaafu hivyo maeneo mengi hayana watendaji, tunaomba utusaidie.
Hali ya uhalifu ni shwari. Unyang'anyi wa silaha umepungua 25% 32.6% barabarani matukio yamepungua
Kwa Miezi kumi bil 68.2 zimekusanywa kwenye mapato.
Tunashukuru kwa hawa Maofisa 120 na Wakaguzi 363
Hiki chuo tulipewa 1961, hadi sasa hakijafanyiwa ukarabati. Tunaomba utusaidie.
Tuna uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule wa 2020. Tumejipanga vizuri.
1209HRS
Naibu Waziri Masauni anasema;
Itifaki imezingatiwa.
Rais haujawahi kutuangusha, kila tukikualika unakuja. Tunakushukuru kwa kazi zote unazozifanya, vitendea kazi, mafunzo na tunapofanya vibaya unatupa makavu live. Tunashukuru sana.
Sisi tunaendelea kukuombea kwa Mwenyezi Mungu wewe na familia yako ili uendelee kuwatumikia watanzania.
Tutaendelea kusimamia amani ya nchi hii kwq mujibu wa Sheria.
Wale wote wanaema wataandamani au watafanya mikisanyiko isiyo na tija, ole wao.
Tuimbe kidogo[tutamlinda na kumtetea rais wetu]
Mafunzo unayoyafunga leo ni kwajilibya kuwajenga Polisi wetu kwenye nyanja mbali mbali ambayo yanawezesha kuwa na askari ambao wana nidhamu, Kuimarisha maadili, yataimarisha kasi ya ubunifu na ya kifanya kazi. Uzalendo. Hiki sio kipindi cha maswala ya dili dili.
Nawaasa maofisa wote wa polisi waache kufanya kazi kwa mazoea. Waheshimu viongozi wa kiraia.
Jeshi la Polisi litahitaji vyo zaidi vya kisasa. Kama Wizara tunafikiria mchakato wa kuanzisha chuo Dodoma. Tunaomba rais hili iweze kulifikiria.
Jukumu langu ni kukukaribisha wewe.
RAIS MAGUFULI ANASEMA;
Itifaki imezingatiwa.
Natambua uwepo wa Mwanasheria mkuu na Gavana. Na uwepo wa Mahita. Mahita njoo uwasalimie
Mahita
Wanajeshi safi? Mambo? Sauti kama ileile. Mheshimiwa rais kwanza naomba nikishuru sana. Umeuvunja mwiko. Ni rais wa kwanza kuja kufunga mafunzo kwenye jeshi la polisi. Zamani walikuwa wanasema rais anafunga mafunzo ya Makamishina. Asanteni sana.
Rais Magufuli anaendelea...
Waheshimiwa viongozi na ndugu makanda na wakuu wa vyombo vingine vya usalama wakiongozwa na mkuu wa Majeshi. Makamishina wa Magereza, zima moto, uhamiaji, na takukuru.
Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana hapa. Nashukuru pia kwa kunialika kwenye sherehe hizi. Hapa ni mara yangu ya kwanza kuja lakini napafahamu. Jeshi la polisi ninyi ni wakwe zangu. Nimeoa kwenue kambi. Kwahiyo amri amri hizo nmezizoea, wakikuambia mwili legeza unalegeza tu.
Nimefurahi sana kuarikwa. Nimefurahi pia hata ukakamavu wa maofisa waliphitimu. Kozi ilianza na wstu 518 na watatu walifariki nilikuwq najiuliza maswali mengi sana. Katika kozi zote duniani, huwa ni vigumu wote kumaliza. Sio rahisi watu wote kumaliza. Nanyi mtakapokuwa mnakamata watu huko halafu halafu wote wakawa hawana hatia ntashangaa sana.
Wahitimu wameiva kikamilifu. Kumaliza ni swala lingine na kutokumaliza ni swala lingine. Isiwe mazoea kwamba maofisa wote wakija wanamaliza, hata kirudia nako ni kitu kizuri.
Hongereni sana, nami nasema kwa dhati nimetoka kwa furaha nyingi sana kwqmba sasa nina watu 515 walioiva.
Wito wangu kwa wahitimu katumieni vizuri mafunzo na elimu mliyoyapata. Sio cheti bali ni maarifa mliopata.
Wengi wenu mtaenda kupangiwa majukumu makubwa, mnapaswa kwenda kuonekana na kuonesha utofauti wa kabla ya mafunzo na baada ya mafunzo katika kuongoza na kuwabudumia wananchi. Mtaongeza heshima ya jeshi la Polisi kwa Wananchi. Ntashangaa endapo baada ya mafunzo haya ntasikia mnawanyanyasa wa chini yenu na kuwaonea, kukamatwa na rushwa, kubambikia wananchi kesi. Ntashangaa sana.
Mumeimba nyimbo nzuro sana, mkazingatieni mliyoyaimba. Mtu ukisahau jikumbushe kwenye wimbo wenu.
Jeshi la polisi ni taasisi nyeti, sisi wanasiasa mara nyingi tumekuwa tukisema nchi yetu ipo salama, lakini nyinyi vyombo vya usalama ndo vinafanya tuseme hevyo ingawa wapo wanasiasa kila uchwao wanawakejeli lakini ninyi ni watu muhimu sana.
Ni kichaa tu au mtu ambaye hana shukurani ambaye hataona juhudi zenu.
Pale kitibiti Maaskari wetu waliuuawa wamasiasa wetu walikaa kimya. Mimi kiongozi wenu natambua kazi nzuri mnayofanya, msivunjike moyo nawwpongeza sana.
Naadhi ya maaskari ntawwpandisha harakaharaka. Mfano yule wa mwaza na wenzake 27 lazima nimpongeze
Jeshi mwaka fulani watu walichinjwa msikitini watu wakakamatwa, kibiti, arusha, kigoma, mbeya pote mumshughulika. Ninawapenda sana tembeeni kifua mbele.
Tunataka maaskari wote wawe na nyumba nzuri. Mimi nipo pamoja na mimi ndo maana nmeanza kuboresha maswala ya usafiri na nyumba.
Bwana Ruta umeomba Mil 700,nitakuleta Mil 700 hapa ili papendeze. Japo tunahamia Dodoma, hiki chuo kiendelee kuwepo. Naomba nikuambie, hizi nazitanguliza za uchumba, nyingine zitaendelea kuja.
Navipongeza vyombo vyetu vya ulinzo na usalama kwa kushirikiana ma kupendana, endeleeni hivyo kwani hii ni chi yetu. Endeleeni kusimama imara na kuwa macho kwa maadui wa ndani na nje.
Katika kipindi chote IGP nakuelezea, hamjawahi kumuonea mtu. Endeleeni hivyo hivyo.
Jambazi anajipiga risasi huko anakamatwa askari, badala ya kupandisha vyeo na nyota, hapana. Sitaki kuona askari anawekwa ndani kwa makosa ambayo hajayafanya wakati anatekeleza majukumu yake. Ntaendelea kuwatetea.
Vitendo vya uhalifu, mauaji ya vikongwe na albino vimepungua sana. Hongereni sana.
Jeshi la Polisi bado linakabiriwa na changamoto kubwa.
Changamoto ya sayansi na technology. Zamani hatukiwa na wizi wa kimtandao, utakatiahaji fedha, itekaji binadamu, madawa ya kilevya nk. Keshi la Polisi tubuni mbinu mpya za kupambama ma uhalifu wa kisasa. Polisi msipobadilika hamtaweza.
Baadhi ya askari wanashindwa kifsnya kazi kwa ueledi na mujituma.
Askari wanabambikia kesi, wanachelewesha kesi, wanapokea rushwa nk. Uvundo wa yai moja bovu ni mkali kulikp halufu ya mayai mengi mazima. IGP nakuomba uchukue hatua kwa askari wanaochafua jeshi letu.
Serikali inatambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na jeshi la polisi nchini.
Niombe jeshi la Polisi, Musiuze maeneo ya jeshi likiwemo jeshi la Polisi. Eneo la Oysterbay pamemegwa hata ukitaka kujenga eneo unakosa. Haya maeneontuyaache tuyatunze, yataendelezwa hata miaka inayokuja. Nlijua hapa mumeshauza, chuo lazima kiendelezwa, lazima pawe pakubwa tu. Msiuze.
Hizi hela mil 700 mlizoomba kabla ya ijumaa ijayo ziwe zimeletwa.
Na zile Bil 7 zilizobaki IGP alizosema, kabla ya Ijumaa ziwe zimefika ila nitafuatilia matumizi.
Pale Magereza Ukonga nilitoa hela wajenge nyumba hakuna kilichofanyika na hela zimeisha. Ndo maana nikafanya mabadiliko haraka haraka. Nmeshamwambia Kamishina wa Mahereza afuatilie hizo hela zimepotelea wapi. Kama wamezifunga wazifungulie kwani zimefungwa vya kutosha. Kama zipo TBA itajulikana.
Natoa wito kwa jeshi la Polisi kusimamia vigezo vyake katika ajira mpya. Wengi hawana sifa, unakuta ni ndugu. Unakuta OCP au RPC ana ndugu yake alifeli huko anasema mleteni huku. Watu kama hao wanakosa nidhamu kwa sababu anakuwa anajua kuna mtu anamlinda. Unakuta hana wito wa askari aliingia kwa kukosa wito.
IGP aliniomba ajira mpya, nikasema ajira mpya ntampa waliotoka JKT ili kusudi wale wenzao wanataka waingizwe mgongo wa nyuma wasiingie. Hakuna aliyepenya. Hata naibu waziri wa Mambo ya ndani alileta watu wake 11 waingie jeshini lakini hawakufanikiwa kuingia Jeshini. Na alifikiri sijui, nlifuatilia kweli
Wapo watu wenye degree ni makoporo na degree zao. Jeshi la polisi sio degrww bali wito. Jeshini ni nidhamu uvumilivu upendo na kuvumiliana.
Nafahamu mlikuwa hampendi mchaka mchaka.
Vyombo vya ulinzi na usalama jipange kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi. Panueni wigo wa kutengeneza hata sare za majeshi mengine. Nataka maaskari wangu wapendeze na sare nzuri. Swala la viwanda mbuni hilo. Hatabkiwanda chankutengeneza Vatu, maji, nafaka.
Kila siku mnakiwa supplied mchele na watu wengine badala ya kuwa supplied na Magereza.
Magereza na kiwanda cha kitengeneza viatu. Ntashangaa majeshi mwngine yakiagiza viatu nje. Nataka uelekeo mpya wa jeshi letu. Barabara nyingi nchi nyingine zinajengwa na majeshi.
Tumebakiza siku chache kuingia mwa wa uchaguzi 2019, uchaguzi mara nyingi unavunja amani na nchi. Simamieni maadili kuhakikisha chaguzi hizi zinaisha salama.
Jeshi la Polisi kuna kero ndogo. Wapo baadhi ya Maaskari wanahamishwa bila malipo. Posho hawalipwi. Walioenda Kibiti hajalipwa wakati majeshi mengine yamelipwa. Hizo kero ndogo ndogo nakuomba uzimalize IGP.
Kuna maaskari wanashika watuhumiwa wanapigiwa simu na ofisa wa juu na kumuambia muachilie huyo.
Kuna askari hivi karibuni walishika matuhumiwa wakachoma visu mkasema hamjawatuma. Hao maaskari watibiwe ikibidi nje ya nchi na huyo aliyewachoma kisu akamatwe. Kila askari afanye wajibu wake. Polisi ameona jambazi, asimkamate hadi umtume?
Mambo ya ndani kitengo cha fedha. Najua Nyamhanga yupo hapa. Kitengo cha fedha hakijakaa vizuri. Kunamalalamiko mengi. Nakuomba IGP na Wizara mkakiangalie viziri kitengo cha fedha. Hata fedha zinazotumwa na Serikali hazitumwo kwa wahusika. Sina sehemu nyingine pa kuliongelea hili.
Askari ni kazi ya kujitolea. Hata kwenye maandiko wamezungumzwa maaskari. Majeshi yana heshima zake.
Mimi nipo pamoja na ninyi katika raha na shida. Kamwe sitawaacha.
Nimefurahi sana kwa kunikaribisha. Serikali yangu ipo pamoja na ninyi na hii ni kwa majeshi yetu.
Mungu wabariki wahitimu wetu Mungu wabariki jeshi letu. Nashukuru sana.
Habari zaidi...
Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametaka askari wa Jeshi la Polisi kutoshtakiwa kutokana na makosa yanayojitokeza wakati wakitekeleza majukumu yao ikiwamo kutuhumiwa kuua wahalifu.
Akizungumza jana wakati wa sherehe za kufunga mafunzo kwa askari wa jeshi hilo katika Chuo cha Taaluma za Polisi, Kurasini jijini hapa, Rais Magufuli huku akiahidi kuwa nao bega kwa bega alisema askari wanafanya kazi kubwa ya kuimarisha usalama wa nchi.
Alisema wakati mwingine askari wamekuwa wakishtakiwa kutokana na makosa ambayo hawajayafanya wakati wakitekeleza majukumu yao ikiwamo kutuhumiwa kuua wahalifu na kwamba kufanya hivyo ni kuwavunja nguvu wale wanaojitoa kwa ajili ya Taifa.
“Nataka Jeshi la Polisi linalochukua hatua sio askari anaenda anachukua hatua anashtukia amewekwa ndani, askari amekwenda kupambana na jambazi bahati mbaya jambazi likijipiga lenyewe risasi likafa kule unakuja unamshika askari, hapana,” alisema.
Rais Magufuli ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu alisema askari wa namna hiyo wamejitoa muhanga kulinda amani ya nchi hivyo ni lazima waongezewe vyeo ili kutoa motisha kwa wengine kujitoa kwa ajili ya Taifa lao.
Katika mahafali hayo, jumla ya askari 513 walihitimu kozi za mofisa na wakaguzi wasaidizi wa Polisi baada ya kumaliza mafunzo ya miezi sita huku Mkuu wa chuo hicho, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Anthony Rutta akisema watatu walifariki dunia wakiwa mafunzoni.
Aahidi kutoa Sh6 bilioni
Mbali ya kuahidi kutoa Sh700 milioni kwa ajili ya kuboresha chuo hicho ili kukabiliana na changamoto za miundombinu ikiwamo majengo, Dk Magufuli pia aliahidi kutoa Sh6.3 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 148 za askari wa jeshi hilo.
Hiyo ni baada ya Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Simon Sirro kueleza kuwa kuna tatizo la makazi kwa askari na kwamba kati ya Sh10 bilioni alizoahidiwa, amepokea Sh3.7 bilioni.
Sambamba na kutoa ahadi hiyo alitoa angalizo, “Kule Magereza, nilitoa pesa kwa ajili ya kujenga nyumba za askari pale Ukonga halafu hazikujengwa, ndiyo maana nilifanya mabadiliko harakaharaka pale nisingevumilia,” alisema.
Alimuagiza Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike aliyekuwapo katika sherehe hizo kufuatilia fedha hizo ili zitumike kama ilivyopangwa.
Stahiki za askari
Rais Magufuli alisema haridhishwi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani hususan kitengo cha fedha kutokana na kuwapo na malalamiko miongoni mwa askari ya kudai stahiki zao.
Alisema malalamiko hayo yamewafanya baadhi ya askari kukosa ari ya kazi na kutoona faida ya kazi hiyo huku wakikosa pa kusemea.
“Hizi kero ndogondogo zinawavunja nguvu maaskari, watu wanahamishwa hawalipwi, kuna baadhi ya posho zao hawalipwi, wapo walioenda Kibiti lakini hawakulipwa lakini inawezekana wanaokusaidia hawakuelezi,” alisema.
Aliwataka viongozi wa wizara hiyo na IGP Sirro kuanza kuzishughulikia mara moja kasoro hizo.
Rais Magufuli alisema pamoja na jeshi hilo kujitahidi kudhibiti uhalifu nchini, kuna baadhi ya askari wasio waadilifu ambao wamekuwa wakipokea rushwa huku wengine wakiwabambikizia kesi wananchi jambo ambalo alisema si tu linalichafua jeshi, bali hata Serikali.
Aliwataka askari wa vyeo vya juu kutotumia nafasi zao kuingilia utendaji kazi wa askari wa chini ikiwamo kuwataka wawaachie baadhi ya wahalifu wanaowakamata.