Kupunguza au kuondoa kabisa maumivu ya jino kabla ya kwenda hospitali sukutua kwa maji ya chumvi mara 5 kwa siku, siku tatu kisha nenda hospitali

Moshi25

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,410
3,879
Mimi naapa nilikuwa siwezi kula , kunywa wala kulala, meno yametoboka yanauma mno hadi machozi yanakuja mi mwanaume nakaza hakuna kulia, mishipa ya kichwa inatoka kichwa kinauma mno, nikamuuliza msela mmoja boda boda nifanyeje kupata ahueni, sidhani kama alimaliza la saba B.

Mimi nina madigrii yangu sina ujanja, akaniambia chukua mswaki weka dawa, kisha chukua kikombe kikubwa weka maji kisha weka chumvi vijiko sita hadi kumi, piga mswaki, sukutua kwa maji ya chumvi kwa dakika 20 mara tano kwa siku, kwa siku 3, wakati mwingine weka mdomoni maji chumvi kwa dkk kumi, nikafanya hivyo na kupona kabisa,

Nikaendelea kupiga mswaki na maji chumvi mwezi mzima nikiwa poa kisha nikaenda hospital kupata matibabu sahihi. Hivi sasa nikisikia tu dalili za maumivu ya meno nasukutua kwa maji chumvi problem solved.
 
Back
Top Bottom