Kimsingi mkeo ndiye mtu wa karibu sana na wewe katika maisha yako ya kila siku, kama mmependana kwa dhati ni dhahili hata uaminifu utakuwepo kwa kila upande. Pia hata kama uaminifu hakuna sioni mantiki ya kuficha salary slip au kumficha kipato chako mkeo au mmeo ni kutokujiamini na kutokomaa kifikra, Kwa sababu kwa namna yoyote ile mimi mwenye mshahara ndiye mwenye maamuzi ya mwisho nikwa namna gani kipato changu kitatumika. Ingawa tunaweza jadili au kushauriana nikwa namna gani tutumie huo mshahara, endapo siridhishwi nitakataa ushauri/maoni yako. Hivyo sioni sababu ya kumficha mkeo/mmeo mshahara au kipato chako. Lakini pia tusisahau kujadili ni nini kinasababisha wanandoa wengi kutokupenda kuweka wazi vipato/ mishahara yao kwa wenzi wao. Hapa nitaorodhesha baadhi tu.
1.Baadhi ya wanandoa kuwa na matumizi ya kificho na yasiyo kuwa na tija kwa familia.
2. Baadhi ya wanawake hupenda akabidhiwe mshahara wote na yeye ndiye awe mwamuzi wa kila kitu ndani ya nyumba na hata nauli na mahitaji madogomadogo binafsi mwanaume awe anaomba kutoka kwake.
Hizo ni baadhi tu ya sababu lakini zipo nyingi zaidi ya hizo.