Afadhali ya wewe umeongea suala la MSINGI SANA....Mkuu usipende kuchukulia mambo kirahisi hivyo. Hapa mie ushauri wangu aidha wanasiasa wakae chini wayamalize tofauti zao. Hujui nini kiko nyuma ya pazia, unaweza kusema hivyo na viongozi au vyombo vya usalama kupuuzia kuwa ni matamko, ikaja kutokea shida kubwa ambayo itacost muda na maisha ya watu kuisolve. Unajua sasa hivi Mh. Rais alivyoziba mianya ya mafisadi, wauza unga n.k wabaya wake lazima watafute mbinu za kila namna kuhakikisha hafanikiwi. Na Mara nyingi wapinzani ndo hutumiwa kuleta chokochoko. Kwa hiyo usichukulie rahisi tu na kupuuza. Mambo huwa yanaanza kidogo kidogo hivyo. Yasipotafutiwa ufumbuzi mapema yanakuwa makubwa.