Kumbe uwaziri unanoga, Nape kielelezo

Nape ananikumbusha ya Wazir Ezekiel Maige na Dr Rutengwe.Nape NNauye amepumzishwa kutoka kwenye uwazir wa habar hivi karibun na Rais wetu Dr Magufuli,baada ya kushindwa kufuata kanuni za utumishi.

Lakini toka Nape atumbuliwe na Rais hajakaa sawa.Nape anaonekana kuchanganyikiwa kabisa.Anaongea vitu vya kitoto kabisa.

Hii inanikumbusha watu wawili waliochanganyikiwa baada ya kuvuliwa uwazir na ukuu wa Mkoa.Ezekiel Maige nae pia alichanganyikiwa kwa muda mrefu sana.Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Rutengwe nae alichanganyikiwa sana na akasema maneno ya ajabu sana.

Fundisho.Hivyo vyeo ni dhamana tu.Nampongeza Rais kwa kuwatumbua ili wajue yeyote aweza kuwa Wazir,Mkuu wa Mkoa.Ukichanganyikiwa baada ya kutumbuliwa unaonyesha udhaifu mkubwa sana wa uongozi .
Magufuli alikataa semina elekezi kwa wateule wake anasema wanajifunza humo humo kazini sasa kuondolewa kwa Nape, Chapombe, mama Kilango na Makatibu wakuu takriban 3 na wateule wengine ni fundisho kwa wateule wengine waliobaki. Kwa lugha nyingine ni elimu kwa vitendo, Semina elekezi or orientation. Hongereni wateule mnaozingatia ma fundisho . Poleni wahanga wa semina elekezi.
 
Binafsi simo kati ya wenye ushabiki na Nape, lakini nimempa marks 100% jinsi alivyokemea 'kunajisiwa' kwa tasnia ya habari. Alikwenda mbali zaidi akasema anayosema anajua yana gharama yake - kama appropriate measures hazitochuliwa basi hakuwa anaona haja ya kuendelea kuwa waziri mzigo. Mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri ilikua ni 'zima moto' asiwawahi wakaaibika, na ndiyo maana hata kusema wamemfukuza ilishindikana. Nape bado ni waziri asiye na wizara na ni shujaa wa zama hizi (si kama huyu aliyechukua kiti chake kila kukicha anahofia maisha yake, utafikiri ataishi milele).

Kukemea nini kilitokea ulichoona wewe kuwa kilikuwa kama watu wameenda vitani?
 
Nape kachanganyikiwa kabisa kutemeshwa uwaziri,atulie tu hayo ndo maisha..!!
 
kwa taarifa yako watu wa mikoa ya kusini hasa lindi na mtwara ukipokewa kwa watu kulala chini na uwakanyage ni heshima kubwa umepewa...........lofa kama wewe huwezi pewa heshima hiyo......
Heshima ya kijinga hivyo??? Kuwakanyaga matako mama zako??? Unamsifia mila za kijinga hivyo?? Kwa hiyo hata wanaokeketwa ni sawa?? Uongee ukweli Nape amekosea sana.. tena akionyeshwa kwenye TV na magazeti. Hiyo dhambi itamnyoosha sana tu!!
 
Nape anataka kuwaaminisha wana ccm na watanzania wote kuwa kazi aliyokuwa akiifanya alikuwa akijitolea kuifanya. Anataka kutuaminisha kuwa wakati ule hakukuwa na watanzania wenye uwezo wa kuifanya kazi ktk nafasi yake. Nape huyu tunamjua tangia enzi zile akiwa mwembamba mithili ya.....,,, amekula pesa za ccm mpaka amevimba kiasi kisichomithilika, kajisahau mpaka anaamini akilini mwake kuwa hakuna ccm bila yeye.
Nimkumbushe Nape kuwa, kazi zote alizokuwa akizifanya kama katibu wa itikadi na uenezi wa Ccm alikuwa akizifanya kwa mujibu wa mkataba wake wa ajira na alilipwa maslahi stahiki kwa mujibu wa mkataba wake wa ajira. Pili, nimkumbushe kuwa, yeye kulala porini, kufanya yote aliyoyafanya, kamwe hakuwezi kumuweka yeye kuwa juu ya mwenyekiti wa chama na Rais wa JMT.
Amesahau kuwa tinga tinga linatengeneza barabara na likishamaliza halitakiwi kupita humo tena na inabidi either libebwe maana litaharibu hiyo barabara endapo litapita. Ukipika chakula si lazima ule. Huo ni uchoyo. Yaani Baba ununue ka kuku halafu wasile wengine. Hicho ndiyo Nape anamaanisha.
 
Mwisho wa ubaya ni
aibu.hatakama Lowasa alikua na kasoro zake,matusi,kebehi na dhihaka nape alizo/ alivyo mfanyia huyu mzee,sio utu kibinaadam,ukizingatia alikua mwenzie kichama.

Isitoshe umri Lowasa ni kama mzazi kwa nape.kinywa cha nape ilibidi kichague maneno,aliyotaka kuyatumia dhidi ya mzee huyu.na jingine goli la mkono !.

Kwa umri wake,wamepora haki ya babu,baba,mama,Dada,kaka ,wakubwa na wadogo zake kwakuisaidia ccm kutawala kwa hila ! Hili halitamuacha hata ahame chama,aachane na siasa au vyama vyote,hili ataingia nalo kaburini.ametumia nguvu zake kudhulumu haki ya wengi.huko kuweweseka ni kudogo tu bado atashangaza sana umma.

itoshe tu ajue,anakula alichoweka ghalani.kwakua alidhihaki na kudhalilisha umma,hanabudi nayeye kukutwa ha hayo.
 
Pamoja na umuhimu wote wa yale matako, jamaa kaishia kuyakanyagakanyaga! Daaah. Kweli tumeumbwa tofauti.
Hakuyathamini kabisa,halafu kusini kule makalio sio tatizo,ndio maana Nape karuhusiwa kuyaponda ponda
 
No way! Tofauti ya Nape na Bashite ni ardhi (Bashite) na mbingu.
hata Nape kuna kipindi mlimchukia sana.. Jaribu ku recall tu. Hata waliomkaribisha Lowassa CDM walisemaga maneno hayo hayo lakini baadaye waliyala matapishi yao..Yeyote anayeonekana anapingana na dola ni shujaa kwa Chadema hata kama anauza madawa ya kulevya..:D:D:D
 
Hizo ni mila za kwao umakondeni, kama wewe ni mtoto wa mjini au uko more 'westernized' pole saana. Wenzio wanadumisha mila.
Mila zingine zimepitwa na wakati.Wewe unaweza kumkanyaga matako mama mkwe wako?Nape alikuwa anatafuta kiki tu
 
Nape nilimuona hana maana alipoamua kuwakanyaga matakoni akina mama watu wazima,anagawanyisha matako kwa kuwakanyaga,asili ya kalio la mwanamke haswa mtu mzima ukilikanyaga lazima litimbwilike.Yule mtoto hana adabu kabisa,na watetezi wa haki za binadamu wanamwita Nape shujaa.Shujaa gani anawakanyaga makalio watu wazima ili apate kiki ya kisiasa
Swadakta maneno yako mkuu - hii inaonesha kuchanganyikiwa
 
Binafsi simo kati ya wenye ushabiki na Nape, lakini nimempa marks 100% jinsi alivyokemea 'kunajisiwa' kwa tasnia ya habari. Alikwenda mbali zaidi akasema anayosema anajua yana gharama yake - kama appropriate measures hazitochuliwa basi hakuwa anaona haja ya kuendelea kuwa waziri mzigo. Mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri ilikua ni 'zima moto' asiwawahi wakaaibika, na ndiyo maana hata kusema wamemfukuza ilishindikana. Nape bado ni waziri asiye na wizara na ni shujaa wa zama hizi (si kama huyu aliyechukua kiti chake kila kukicha anahofia maisha yake, utafikiri ataishi milele).
Kinachojadiliwa ni anachokifanya na kuzungumza baada ya kutenguliwa sio kabla ya kutenguliwa...uko out of point mkuu.
 
Back
Top Bottom