Kumbe Mwanaadamu hamiliki chochote hapa duniani

1 Timotheo - 1 Timothy 6

3 Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,
4 amejivuna; wala hafahamu neno lo lote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya;
5 na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
6 Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
7 Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;
8 ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.
9 Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.
10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
11 Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.
12 Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.
13 Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato,
14 kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;
15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana;
16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.
18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;
19 huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.
20 Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo;
21 ambayo wengine wakiikiri hiyo wameikosa Imani. Neema na iwe pamoja nanyi.
 
Dahh!ni kweli na kile kitendo cha binaadam kuzaliwa mtupu hana akili hata moja tena kichanga kisichojielewa ni uthibitisho wa maelezo yako.
 
Mmmmh Tazama ba mizinga ya Dangote lakini vitu atakavyoenda navyo havivuki elfu arobaini ya bongo
 
Kulingana na maana ya neno kumiliki ni kweli kuwa tunamliki vingi hata akili zetu pia, Ni kweli Mungu katupa akili, dunia na vyote vilivyomo ili tuvimiliki.
 
Nimejitahidi kuumba uhalisia wa Mwanadamu kuhusu maisha yake na mahusiano yake na Mungu, mazingira na roho yake, nimegundua hakuna kitu chochote mwanadamu anachomiliki. Kwa kuanza na roho yake, binadamu kapewa kutoka kwa Mungu, na pia akapewa na mwili ili roho ipate kujihifadhi kuendana na Mazingira. Sikuhishia hapo nikayatazamana mazingira anayoishi mtu huyu nikagundua kuwa yaliandaliwa na Muumba wake ili yamfae katika kumtumikia. Nikamalizia na kuangalia vitu alivyotengeneza na kuvumbua mwanadamu ni matokeo ya matumizi ya akili yake aliyotunukiwa na Muumba wake. Hapo nikaanza kuingiwa na wasiwasi kua ni kipi hasa binaadamu anamiliki katika dunia hii kama roho,mwili na akili inayomfanya ajivune na maendeleo aliyonayo hasa yakiteknolojia, kumbe sio yake bali ni matokeo ya akili aliyopewa na muweza wa wote? Nikapata na mshangao kuwa kumbe binaadamu anapokufa ni huwa roho yake inachukuliwa na anaacha kila kitu alichokuwa nacho! Na kama angekua anamiliki hasa uhai angekua na maamuzi nao, ivyo Mungu ndio mmiliki sahihi ndio maana maamuzi yake kwenye maisha yetu hayapingwi na yeyote au chochote. Nikahitimisha kuwa Mwanaadamu hana kitu zaidi ya kupata upendeleo wa utashi kuliko wanyama wengine na ivyo anapaswa kumtumikia Mungu maana ata Uhai anaoringa nao sio mali yake. Asanteni kwa kuelewa.
Ahsante sana Mkuu streat Anthem .

Umeniongezea kitu.Nitazidi kuisoma kila siku ili inikae kichwani vizuri.Barikiwa sana.
 
Wala sio nyama na damu vilivyokufunulia ufahamu huu mkuu bali ni Roho ya Mungu mwenyezi mwenyewe. This is great understanding!
 
Kitu Pekee Binadamu Anachomiliki Ni Tabia Yake Tu. Ndio Maana Hata Anapokufa Tunaobaki Tunamkumbuka Kwa Matendo Yake.
Kaka nayo sio yako, ni ya shetani au ya Mungu, kwa maana ya kwanda tunda la roho huzaa tabia njema ambayo ni ya Mungu na tunda la uovu huzaa tabia mbaya ambayo ni ya shetani.

Wewe na mimi hatuna chochote chetu vyote tumepandiwa tu.
 
Nimejitahidi kuumba uhalisia wa Mwanadamu kuhusu maisha yake na mahusiano yake na Mungu, mazingira na roho yake, nimegundua hakuna kitu chochote mwanadamu anachomiliki. Kwa kuanza na roho yake, binadamu kapewa kutoka kwa Mungu, na pia akapewa na mwili ili roho ipate kujihifadhi kuendana na Mazingira. Sikuhishia hapo nikayatazamana mazingira anayoishi mtu huyu nikagundua kuwa yaliandaliwa na Muumba wake ili yamfae katika kumtumikia. Nikamalizia na kuangalia vitu alivyotengeneza na kuvumbua mwanadamu ni matokeo ya matumizi ya akili yake aliyotunukiwa na Muumba wake. Hapo nikaanza kuingiwa na wasiwasi kua ni kipi hasa binaadamu anamiliki katika dunia hii kama roho,mwili na akili inayomfanya ajivune na maendeleo aliyonayo hasa yakiteknolojia, kumbe sio yake bali ni matokeo ya akili aliyopewa na muweza wa wote? Nikapata na mshangao kuwa kumbe binaadamu anapokufa ni huwa roho yake inachukuliwa na anaacha kila kitu alichokuwa nacho! Na kama angekua anamiliki hasa uhai angekua na maamuzi nao, ivyo Mungu ndio mmiliki sahihi ndio maana maamuzi yake kwenye maisha yetu hayapingwi na yeyote au chochote. Nikahitimisha kuwa Mwanaadamu hana kitu zaidi ya kupata upendeleo wa utashi kuliko wanyama wengine na ivyo anapaswa kumtumikia Mungu maana ata Uhai anaoringa nao sio mali yake. Asanteni kwa kuelewa.
Hilo ni kweli
 
Leo BINAADAMU amegeuka kuwa mtumwa kwa viumbe kama MBWA... FARASI...PAKA... (Ng'ombe na Mbuzi) kwa kuwapa huduma za kiwango cha juu.

Tazama, ziko nchi bajeti ya kutunza mnyama kama Mbwa... Paka... Farasi n.k.
Gharama ni zaidi ya zile anazo hitaji binaadamu anae taabika na Maji... Madawa... Chakula n.k.

Kwa kweli naunga mkono hoja kuwa DUNIA hii si mahala pa kudumu ama kujivunia kwa mwanaadamu..

Na ndio maana tunaambiwa kuna PARADISO....
Mahala ambapo hakuna atakae kuwa mtumwa kwa mwenzie..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom