Kulikuwa na upungufu wa tani 44,342 za nafaka mwaka 2021/22

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
426
684
Mwaka wa fedha 2021/22 ulikumbwa na uhaba wa nafaka kama ambavyo imeripotiwa na Benki Kuu ya Tanzania kuwa katika mwaka huo kulikuwa na uhitaji wa chakula tani 9,537,752 hata hivyo tuliweza kuzalisha tani 9,493,410 ambapo tofauti ni tani 44,342.

Suala la kuwa na upungufu wa chakula limeripotiwa kwa mwaka 2021/22 tu maana miaka mingine yote kulikuwa na surplus ya zaidi ya tani laki moja.

Taarifa hizi ni kwa mujibu wa Annual Report ya BoT iliyotolewa December 2022.

Kimsingi, mwaka 2021 ndio ulikumbwa na madhara makubwa ya COVID-19 ambapo sekta ya kilimo iliathiriwa sana kwa ukosefu wa pembejeo

Aidha kwa upande wa bei za jumla ya mazao, Maharage ndio yamekuwa na bei kubwa zaidi kuliko mazao mengine kwa mwaka 2021/22. Gunia la kilo 100 la maharage liliuzwa kwa Tsh 179,894.5 bei ambaye imeizidi mtama, mahindi na mchele.

1672835517342.png


Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom